Pre GE2025 Masauni: Sativa hatoi ushirikiano wa kutosha kwa Jeshi la Polisi
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu, mnamuelewa kweli Masauni?

Sativa baada ya kufika tu hospitali alihojiwa kwa masaa matatu kabla sijakosea akieleza yote, polisi wakiwepo pamoja wanaandishi wa habari halafu anakuja kutuambia Sativa anaongea kwenye mitandao ya kijamii! Masauni anajielewa kweli?

Huyu naye ni mwingine wa kutengua!

Pia soma: Sativa: Naendelea na matibabu siwezi hata kufungua mdomo, yakimalizika nitatoa ushirikiano wanaotaka

====

"Ili suala la Sativa liende haraka ni muhimu yeye mwenyewe atoe ushirikiano, ushirikiano wake bado ni mdogo katika kulisaidia jeshi la polisi kupata taarifa za yaliyomkuta

"Kitenge: Lakini alishasema alipelekwa Osyterbay, kwanini msianzie hapo?

"Wewe ndiye muhusika wa lile tukio, wewe ndio unajua kwamba umekamatwa nan ani, yukoje, baada ya kutoka hapo nikaenda wapi, kwahiyo eleza vyombo husika, usieleze kwenye mitandao ya kijamii. Mimi si ndio Waziri wa Mambo ya Ndani, basi mwabie aje wizarani kwangu, aje anieleze mimi."

Sativa alihojiwa na polisi kule Katavi alipotupwa na watekaji, na taarifa ya polisi ikatuambia ameshambuliwa na kitu chenye ncha kali kwenye taya.

Sasa huyu Masauni anataka Sativa ahojiwe na polisi mara ngapi? kwanini wasifanyie kazi ile taarifa ya kamanda wa polisi Katavi aliyetuambia wanaendelea na uchunguzi?

Kwa maana hiyo kumbe hata uchunguzi wa kipolisi juu ya lile tulio la kutekwa Sativa bado haujaanza?!
 
Wakuu, mnamuelewa kweli Masauni?

Sativa baada ya kufika tu hospitali alihojiwa kwa masaa matatu kabla sijakosea akieleza yote, polisi wakiwepo pamoja wanaandishi wa habari halafu anakuja kutuambia Sativa anaongea kwenye mitandao ya kijamii! Masauni anajielewa kweli?

View attachment 3056106
Hawako serious
 
Sijui kwanini great thinkers mnatumia nguvu zenu na akili zenu kujadili ishu kama hizi. Kila mwenye akili timamu anajua wazi serekali haina utashi wala haja kuchunguza haya na simply kwa sababu inaweza kuwa nyuma ya maujinga yote haya.

Katika mazingira kama haya mnategemea Masauni aseme nini?

Ilikuwa ujinga hivi hivi wakati wa Lisu kwamba hatoi ushirikiano sasa na leo wanarudia ujinga huo huo tena.

Hata mtoto wa darasa la tatu anajua kabisa who is behind all these shit
 
Kama hatoi ushirikiano aachwe atapeleleza kesi yake mwenyewe.
 
Na ana mtaka
Sativa alihojiwa na polisi kule Katavi alipotupwa na watekaji, na taarifa ya polisi ikatuambia ameshambuliwa na kitu chenye ncha kali kwenye taya.

Sasa huyu Masauni anataka Sativa ahojiwe na polisi mara ngapi? kwanini wasifanyie kazi ile taarifa ya kamanda wa polisi Katavi aliyetuambia wanaendelea na uchunguzi?

Kwa maana hiyo kumbe hata uchunguzi wa kipolisi juu ya lile tulio la kutekwa Sativa bado haujaanza?!
Ana mtaka aende Ofisini kwake....akamuhoji yeye tena?!!!!Masauni anaweza kuwa ndiye mtekaji...Ripoti ya Polisi- Katavi, hana imani nayo.
 
Wakuu, mnamuelewa kweli Masauni?

Sativa baada ya kufika tu hospitali alihojiwa kwa masaa matatu kabla sijakosea akieleza yote, polisi wakiwepo pamoja wanaandishi wa habari halafu anakuja kutuambia Sativa anaongea kwenye mitandao ya kijamii! Masauni anajielewa kweli?

View attachment 3056106
Hawa Wazanzibari wana dharau sana!!
 
Kipenzi chetu Imam Hussein aliuwawa kikatili sana Karbala ili kulinda na kuutetea uislamu. Nasi Allah katupa Tawfiq. Lakini cha kuhuzunisha Sunni hawamuenzi Imam wetu wanamdhihaki kumtukana nakutudhihaki.

Allah mwenyez Mungu mwingi wa rehma ampe qaul thabeet kipenzi chetu Imam.
 
Masauni hiyo Wizara imempwaya vibaya mno.Hata kwa kumwangalia na kumsikiliza jamani: Anatoa maelezo ya kuunga unga na kubabia babia...ni staha tu ya anaye muhoji...
Huyu naye yupo ccm na serikalin kimapokeo, hawana jipya Hawa wa hivi
 
Back
Top Bottom