Tetesi: Masha kumrithi Mbowe uenyekiti CHADEMA

Status
Not open for further replies.

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Masha kumrithi Mbowe uenyekiti CHADEMA.

Huu ndio ukweli japo mchungu, Mbowe utashukuriwa kwa kufanikisha yote hasa ujio na uratibu wa Lowassa kugombea uraisi lakini sasa ni wakati wenye nacho wanajipanga kufanya yao. Kuna mambo mawili ya kuchagua, aidha kuingia kwenye mchuano au kutangaza kuachia ngazi katika uchaguzi mkuu wa chama 2018 au 2019. Ni jambo moja tu ujue safu ya viongozi wa ngazi za chini kuanzia vijiji,mitaa,kata,wilaya,mikoa na Taifa ndani ya CHADEMA ambao kimsingi baadhi yao ndio wenye jukumu la kuchagua Mwenyekiti wa Taifa watatokana na kundi la marafiki wa Lowassa, watamsikiliza mkuu wao.

Kwanini Masha?
Ni msomi wa sheria na mwenye uzoefu wa kufanya kazi serikalini kama waziri mwandamizi na mwanasia na zaidi ndiye anayekubalika na TeamEL hususan waliokuja CHADEMA na hata wale wanaotafuta kimbilio la kisiasa baada ya mabadiliko ndani ya CCM kuwatupilia mbali kutokana na tuhuma mbalimbali.

Nini madhara endapo mpango huu ukifanikiwa?
Ni dhahiri wahafidhina wanaoishi kwa kuvumilia ujio wa EL kama akina Tundu,Mnyika,Mdee nk watafurukuta bila mafanikio na huenda safari hii Tundu akawa muhanga wa ‘katiba mbovu’ aliyoitunga ambayo itamnyima haki ya kwenda mahakamani na hivyo kuamua kutafuta mustakabali nje ya CHADEMA au kubaki kimya bila kitu.

Zitto na ACT kuibuka kidedea?
Huenda hoja ya ufisadi ikaibuka tena na mara hii majeruhi wapya wa siasa za Chadema wakimuona Zitto kama kimbilio huku wakieleza majuto kushirikiana na TeamEL ili angalau kupata umaarufu na huruma ya wananchi angalau kupata ubunge,udiwani nk. ‘katika siasa hakuna adui wa kudumu,wala rafiki wa kudumu’’ haya ndio maneno yatumiwayo na matapeli wa kisiasa ili kuficha aibu ya uovu wao waliotekeleza kweupe!.

Unaruhusiwa kufanya rejeo.
 
Chadema ikipona kwenye uchaguzi wao wa ndani, haitavunjika tena!Lakini sioni kama watapita salama, maana yale mapapa yamekaa kwao na waliokipigania chama awali wanaishiwa pumzi taratibu huku wengine wakiamua ku-mute kabisa
 
Ahsante kwa Utabiri Feki usio na Mashiko,
Naona unawania mikoba ya Sheikh Yahya
 

Naona wewe ndiyo uchukue form
 
Mtakufa mkiiacha CHADEMA ikielekea kuipeleka Tanzania nchi ya ahadi,nanyi hamtoiona.
 
Huko ACT amefanya nini?Afande Sele amesema ni wanafki yaani "Popo".
 
Nchi ya ahadi aiji kwa kupokea Makapi na Mafisadi sanasana mna beba laana.
 
Hakuna kikaragosi yeyote CDM mwenye uwezo wa kumtoa Mbowe kwenye uenyekiti.

Mbowe ni Alpha na Omega kwenye uenyekiti.

Atatawala na ataendelea kutawala....yale macho yake yana uwezo wa kuona wanasiasa wenye mvuto kutoka CCM.

Mwaka 2020 ataleta usajili bora kabisa kutoka CCM na Lowasa atatoswa.

Na wanachama watapiga kura ya wazi ( kwa vidole.....japo kwenye BMK walishinikiza kura za siri) kutimiliza hitaji la Mbowe.
 
mɓowe endelea mpaka tutakapoidondosha ccm. uwezi kuishia njian kama dr mihogi. mbowe tumekula ng'ombe mzima kasiro mkia wanyanyasaji wakaondoka
 
Ushauri wa mwanaccm juu ya kupata kiongozi Chadema, maajabu!
Ni sawa na Salary Slip awashauri Ccm wamchague Livingstone Lusinde kuwa Katibu mkuu baada ya Kinana kuachia ngazi Mwezi ujao kwa kuona chama kinaendeshwa kienyeji.
Sababu za kumpendekeza Lusinde iwe ni kwa kuwa anahanasisha kuwaua watafiti wa Maendeleo jimboni na kuonyesha dhahiri Anatimiza adhima ya chama chake kutopenda Maendeleo hivyo anafaa kuwa katibu mkuu
 
Huu muda unaopata wa kutabiria upinzani na kuukashifu, ungekuwa unautumia kujadiliana na makada wenzako changamoto za serikali kushindwa kuinua elimu ya nchi hii hata Mungu angekubariki na ingekuwa afya kwako, kuliko sasa unavyo endelea kujijazia nyongo mwilini kwa watu ambao hata hawatambui uwepo wako duniani.
 
Mkuu, kwenye gazeti la HabariLeo la siku ya leo Lusinde eti karipotiwa kulaani mauji ya watafiti.Habari iko katika ukurasa wa mbele.
 
Mkuu, kwenye gazeti la HabariLeo la siku ya leo Lusinde eti karipotiwa kulaani vifo vya watafiti.Habari iko ukurasa wa mbele.
Too late, imeshajulikana tayari kuwa vifo vile vya wale watafiti vilihamasishwa na kauli zake.
Nasubiri bungeni nimsikie Halima Mdee akiuliza swali "serikali inachukua hatua gani kwa wabunge wanaowaambia wananchi kuwa watafiti ni wanyonya damu?"
 
Kwani jamani Lusinde ana mapungufu gani kisiasa? Narudia kisiasa?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…