Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 16,003
Masha kumrithi Mbowe uenyekiti CHADEMA.
Huu ndio ukweli japo mchungu, Mbowe utashukuriwa kwa kufanikisha yote hasa ujio na uratibu wa Lowassa kugombea uraisi lakini sasa ni wakati wenye nacho wanajipanga kufanya yao. Kuna mambo mawili ya kuchagua, aidha kuingia kwenye mchuano au kutangaza kuachia ngazi katika uchaguzi mkuu wa chama 2018 au 2019. Ni jambo moja tu ujue safu ya viongozi wa ngazi za chini kuanzia vijiji,mitaa,kata,wilaya,mikoa na Taifa ndani ya CHADEMA ambao kimsingi baadhi yao ndio wenye jukumu la kuchagua Mwenyekiti wa Taifa watatokana na kundi la marafiki wa Lowassa, watamsikiliza mkuu wao.
Kwanini Masha?
Ni msomi wa sheria na mwenye uzoefu wa kufanya kazi serikalini kama waziri mwandamizi na mwanasia na zaidi ndiye anayekubalika na TeamEL hususan waliokuja CHADEMA na hata wale wanaotafuta kimbilio la kisiasa baada ya mabadiliko ndani ya CCM kuwatupilia mbali kutokana na tuhuma mbalimbali.
Nini madhara endapo mpango huu ukifanikiwa?
Ni dhahiri wahafidhina wanaoishi kwa kuvumilia ujio wa EL kama akina Tundu,Mnyika,Mdee nk watafurukuta bila mafanikio na huenda safari hii Tundu akawa muhanga wa ‘katiba mbovu’ aliyoitunga ambayo itamnyima haki ya kwenda mahakamani na hivyo kuamua kutafuta mustakabali nje ya CHADEMA au kubaki kimya bila kitu.
Zitto na ACT kuibuka kidedea?
Huenda hoja ya ufisadi ikaibuka tena na mara hii majeruhi wapya wa siasa za Chadema wakimuona Zitto kama kimbilio huku wakieleza majuto kushirikiana na TeamEL ili angalau kupata umaarufu na huruma ya wananchi angalau kupata ubunge,udiwani nk. ‘katika siasa hakuna adui wa kudumu,wala rafiki wa kudumu’’ haya ndio maneno yatumiwayo na matapeli wa kisiasa ili kuficha aibu ya uovu wao waliotekeleza kweupe!.
Unaruhusiwa kufanya rejeo.