..je umetoa droo na timu gani?
Naunga mkono hiyo sentensi yako. Kweli kabisa hata Mimi naona hapo ndo kwenye tatizo. Na Kwa nchi yetu naongezea "Na kwenye uwanja gani?" Simba siyo ya kuvuja jasho kutafuta Sare na KMC Kwa Mkapa.
Nafikiri kuna point muhimu wanayo mashabiki na wanachama wa simba nayo ni namna timu inavyoperform uwanjani, wanachezaje, je wanakosa matokeo dhidi ya timu ya aina gani, ni hoja ya msingi sana wanayo, usajili waliofanya kmc na walioufanya simba auendani na uhalisia wakiwa uwanjani, kufungwa ama kudroo ni jambo la kawaida kwenye soka lakini je umetoa droo na timu ya aina gani na ukiwa unacheza mpira wa aina gani ndio hoja ya msingi msitoke nje ya hoja
Ajibu kwa Maswali yako ni hivi, Kwanini Simba haiparfome na haipati matokeo kwa timu dhaifu? Jibi ni tatizo la kiufundi simba haina benchi dhabiti lenye mipango dhabiti la kiufundi, ndani ya mwaka mmoja mmekuwa na makocha wangapi?
Kwanini Simba hawana benchi dhabiti? kwasababu simba haina management dhabiti ya kiuongozi, Management haina mipango ya muda mfupi na mrefu ya kuisuka timu baada ya kuuza wachezaji waliifikisha timu kwenye mafanikio.
kwa kwanini? Kwasababu Mo ambaye ndiye mfadhili wa simba ni mjanja mjanja alikuwa na lengo la kuitengeneza simba kweli ikapata imafanikio mwisho wa siku akauza wachezaji chama, miqson wakati bado timu ilikuwa inawahitaji,
Wanasimba walitegemea, management wangewauza wachezaji then wasajili wachezaji quality zaidi, ila kwasababu ni janja janja mkaokoteza wachezaji kwa gharama ya mapambio matokeo yake ndiyo hata mnayoteseka nayo sasa.
Suluhisho kwa sasa,
Mkubali mlikosea, acheni timu ipate matokeo yoyote bila kunyoonsheana vidole mjue panapovuja vizuri, msimu ujao mrekebishe.
Angalizo kama hatutabadili jinsi tinavyoendesha timu zetu hasa simba yanga, maumivu yatatuhusu sana, tupambambanie mabadiliko, tuache utegemezi kwa watu/mtu, mabadiliko hayo yatawavuta wafadhili sio kama sasa.