Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Naona nyuzi za mashabiki wa Simba humu jukwaani zimekuwa nyingi, zikijimwambafai kuifunga Yanga Jumapili. Najua mashabiki wenu wanajiamini kupita kiasi baada ya kuwafunga Ihefu ya Angola na kuingia makundi na wanaona tayari kikosi chao ni bora kuliko cha Yanga baada Yanga kutolewa na Al Hilal.
Napenda kuwapa tu angalizo, Tembo anaweza kukonda lakini hawezi kulingana sisimizi hata siku moja. Yanga pamoja na kutolewa kwenye Klabu Bingwa na Al Hilal bado ni timu yenye kikosi bora kuliko timu yoyote ile hapa Tanzania.
Simba pamoja na kuingia makundi bado wana kikosi cha kawaida sana ukilinganisha na Yanga. Kwahiyo linapokuja suala la kukutana timu hizi mbili labda uwe umejitoa ufahamu. Kuanza kujimwambafai kwamba unakwenda kumfunga Yanga kwakuwa tu umeshinda mechi yako iliyopita, utakuwa unaingia choo cha kike na utakuwa unajitafutia msongo wa mawazo na presha zisizokuwa na maana.
Matokeo yake ni kuzimia uwanjani, kwakuwa umeweka matarajio makubwa kwenye jambo ambalo haliwezekani kirahisi kama unavyofikiria.
Kumbuka mnaenda kucheza na Yanga bora na siyo De Agosto wala Bata Bullets, kuweni makini na furaha yenu maana inaanza kuvuka mipaka.