Mashabiki Simba wanatamani supu pia, wanashindwa kusema

Mashabiki Simba wanatamani supu pia, wanashindwa kusema

Wewe shabiki wa timu kama usipopewa supu unywe na timu Yako upata nini kutoka kwenye timu Yako? Hasara mwanzo mwisho. Kama timu zinarejesha kwa jamii kwanini iwe shida kurejesha kwa wanachama na mashabiki? Yanga wako sahihi sana kunywa supu kutoka kwenye club yao baada ya kununua jezi, kutoa viingilio, kusafiri na timu, kulipia uwanachama, kulipia Yanga app, na kutembelea social media za timu. Mambo Yote haya yanamgharimu shabiki na mwanachama wa Yanga, Kuna ubaya gani club ikarejesha japo kidogo kwa watu wao hawa?

Hata mashabiki wa Simba wanatamani kwelikweli Ile supu lakini mo amekaza fuvu, anadai anapata hasara. Pesa wanazotumia Yanga kunywa supu ni Ile inayopatikana kwenye kitengo chao cha habari TU. Safi sana Yanga kwa ubunifu, Iko siku Simba wataliiga jambo hili. Shakini hawezi kutoka kapa mwanzo mwisho wakati anaona wako watu wananeemeka kwa kutumia jasho lao.


View: https://youtu.be/eIMS935Oiag?si=2HRXdlwd5Q8yFod8

Nani atamani kula vibudu wewe mlugaluga?
 
Mo eti anaponda kuhusu supu hajui kwamba supu inaunganisha familia ya yanga, (jamii), Yanga sc soup day is there to strengthen the yanga family
Sasa ndiyo iwe supu ya vibudu? Mtapata kimeta shauri yenu
 
Anawafanya wajinga wanasimba. Yeye ananenepa na mashabiki wanakonda. Mwanachama anunue jezi, tiketi, bando na kuishangilia timu lakini asiambulie hata maji ya kunywa. Yanga wako sahihi sana, Tena waifanye ya kudumu Kila mwaka kuwe na siku ya kunywa supu pale makao makuu na matawi yanayoonhoza kulipa ada zao na kununua jezi.
Supu ya vibudu ya siku moja inawatoa ufahamu mnaona mumepewa kitu cha maana.
 
Back
Top Bottom