Tuwe Wakwelii...
Luis Enrique ametumia karibu kiasi sawa cha pesa ndani ya miaka miwili pale PSG kama ambavyo Mikel Arteta ametumia katika kipindi cha miaka sita pale Arsenal.
Lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya mazingira yao wawili:
Enrique alirithi kikosi kilichojaa wachezaji nyota. Hakuhitaji kujenga kikosi upya.
Arteta alikabidhiwa timu iliyokuwa inaporomoka — na ilibidi ajenge kila kitu kutoka mwanzo.
Kwa hiyo, je, ni haki kulinganisha mafanikio yao moja kwa moja bila kutazama hali ya klabu zao?
Historia Inathibitisha: Vilabu Vikubwa Huwekeza Mapema
Kama bodi ya Arsenal ingeamua kweli kushinda makombe, tungeona uwekezaji mkubwa, wa dharura — kama ule uliofanyika katika vilabu vingine vinavyojua wanachotaka.
🔵 Chelsea – Kipindi cha Abramovich (2003)
Walitumia zaidi ya £205M ndani ya misimu miwili ya kwanza.
➡️ Matokeo: Ubingwa wa EPL na Kombe la FA mwaka 2005.
🔵 Manchester City – Kipindi cha Sheikh Mansour (2008)
Karibu £230M ndani ya misimu miwili.
➡️ Matokeo: FA Cup mwaka 2011.
Lakini Mashabiki Wengine wa Arsenal Wanalalamika...
"Arteta katumia £800M ndani ya miaka 6 OMG!!”
Kweli? Mnamaanisha nini?
Matumizi makubwa yaliyosambazwa kwa miaka mingi hayaonyeshi njaa ya mafanikio.
Yanaonesha kuwa bodi haijali sana kushinda mataji — bali inalenga utulivu wa kifedha.
Hapo ndipo tofauti kubwa ya fikra inaonekana:
🔴 PSG: Wanataka ushindi sasa — na wanachukua hatua bila kusita.
⚪ Arsenal: Wanalenga kudhibiti bajeti na "kufunika mapengo" — si kubeba makombe haraka.
Mashabiki wa Arsenal Wapaswa Kusema Hili Waziwazi
Lazima tutambue: mafanikio hayasubiri. Vilabu vyenye njaa ya ushindi huwekeza kwa kasi na uthubutu.
Tazama mifano:
Liverpool: Wameshinda EPL na sasa wamesajili Frimpong na Wirtz — kwa bajeti kubwa, wakilenga kurejea kileleni.
Man City: Walitumia karibu £200M kwenye dirisha la Januari ili kuokoa msimu.
Real Madrid: Wao huongeza ubora kila dirisha la usajili bila kusita.
Wakati huo huo...
Sisi Arsenal bado tunabishana kuhusu mishahara ya Gyökeres na Sesko.
Mazungumzo hayaishi. Hatufanyi maamuzi unaoendana na malengo makubwa.
Chanzo Romano