Mkuu kwenye ukweli tuwe wakweli. Mimi ni shabiki wa simba lakini aina ya ushabiki wa Manala siupendi kabisa. Ushabiki wa Manara unaleta uhasama kati ya mashabik wa Simba na Yanga.
Ni zaidi ya miaka 80 hizi timu zipo lakini kwa miaka hiyo yote hatukuwa na uhasama wa aina hii. Tulikuwa na utani lkn siyo uhasama. Ilikuwa timu ya nje ya nchi inakuja na ikitokea ikaishinda yanga wana simba tumekuwa tukiishangilia humo humo uanjani. Lakini nje ya uanja hatukuwa tukionyesha ushabiki.
Lakini kwa sasa ushabiki unaanzia nje ya uanja. Na chanzo cha yote haya ni Manala. Namuomba manala afanye ushabiki wa utani kama tulivyozoea kwa miaka yote lkn aache ushabiki wa kashifa. Vinginevyo akae pembeni asitujengee uhasama kwa wananchi wa nchi moja.