Mashabiki wa Ronaldo njooni huku

Mashabiki wa Ronaldo njooni huku

Naona Mnamzungumzia Messi Wakati DiMaria ndo Kaipa Ubingwa Argentina.
 
Ureno ana kombe la Euro tangu 2016,ambapo Argentina akija kushiriki Euro competition anaishia kwenye makundi hata 16 bora hafiki
Mbona kombe la dunia 2014, aliingia fainali pamoja hawakuchukua ila Messi akawa mchezaji bora wa mashindano.
 
Haya Sasa Messi huyooo kabeba kombe akiwa na timu ya taifa

Mlikua mnamuona Messi si lolote na wala si chochote kwa C.Ronaldo,kwasababu C.Ronaldo alishinda EURO mkawa mnamponda Messi kwakua hajashinda taji lolote akiwa na timu yake ya Taifa

Najua mtataka Messi afanye Kama Ronaldo kuhama Hama ligi [emoji23] huu ni upuuzi nawaambieni hivi MESSI hahitaji kuhamia ligi yoyote ile ili athibitishe uwezo wake.

Sasa sisi team Messi tunawadai ninyi team Ronaldo Balon'Dor ya 6 na tunataka mchezaji wenu aipeleke timu yake ya taifa fainali tu za kombe la dunia.

Daadeki zenu nyinyi.

View attachment 1849190
Mkuu!!! Debate imefungwa rasmi Leo na Mfalme wa soka hapa Duniani, Messi10. Team CR7 waandike maamivu ktk maisha Yao yote.

Ballon D'or yake ya 7 (the King [emoji146] Leo Messi10) ashaiweka kibindoni tayari. Kinachofurahisha zaidi lakini itabaki kuwa fedheha kwa wapenzi wa CR7 ni kwamba idadi ya Ballon D'or (7) ambazo Mfalme Messi10 atakuwa amewahi kushinda ndiyo namba ya jezi ya CR7 (rival wa Messi10 wao wanaita).

Hivyo, CR7 ktk maisha yake yote atabaki kuibeba idadi hiyo mgongoni mwake kuitangazia Dunia kuwa ni Mfalme Messi10 pekee ndiyo ambae amewahi kushinda Ballon D'or mara 7 .

Nawashauri haters wa Mfalme Messi10 na CR7 mwenyewe wamwombee tu Messi10 (fundi wa kweli) ashinde Ballon D'or ya 8 mwakani (2022) ili wakiuepuke kikombe hiki cha fedheha na Penaldo wao katika maisha Yao.... Otherwise waandike maumivi katika maisha Yao yote.

Johan Cruyff (mataalam wa tiktaka duniani) aliwahi kumtabiria Mfalme Messi10 kuwa "probably he may win 5, 6 or 7 Ballon D'or... Sasa haters wa Penaldo ni nani hata wabishane na mwasisi wa soka la kuvutia hapa Dunia.... Kenchy type!!! Daaadek zao...
 
Kwakuwa nyinyi mlishabeba World Cup siyo?
Siyo lazima tushinde Mzee lakini kama imeandikwa wewe ni nani hata uzuie aisee.... Mlisha kariri kwamba Messi10 hawezi chochote akiwa na timu ya Taifa.

Nakuwekea kumbukumbu sawa hapa...

Messi10 ameshinda world[emoji289] cup akiwa na under 20 timu ya Taifa.

Messi10 ameifikisha Argentina kwenye fainali za mashindano makubwa mara 5.

Fainali 4 za Copa America (ikiwemo hii ya 2021 aliyobeba ndoo). Fainali 1 ni world cup v Germany 2014.

Halafu timu Penaldo utawasikia mkibana pua zenu Messi10 hamana kitu. Wakati Mungu alimhurumia tu ndugu yenu atangulie kushinda Euro ili mbane pua weeeee kwani kama Mfalme wa soka Messi10 angekuwa ameshinda Toka wakati huo Mungekuwa mmepata wapi muda kubanabana pua zenu...
 
Messi mchumba tu
Hii picha inakata ngebe zote!!! Daaadek
Screenshot_20210711-100608_1.jpg
 
Watching someone saying Messi isn't better inachekesha...
Fainali za Copa America Mara 4..
Kombe la Dunia Mara Moja

Na bado anakwenda kuongeza ballon Dor ya 7....
Definition of a pure player..
watamkana kwa kubanabana pua zao... Lakini mioyo Yao itawaambia kimya kimya kuwa Mfalme wa soka ni mmoja tu naye si mwingine Leonel Messi10....
 
Fainal CR7 alikua majeruhi!!!?

Sema alitolewa nje baada ya kupata majeruhi bwana tim mess bwanaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kelele nyingi na huyo ndujeru wenu utadhani kashinda kombe la dunia.

Messi hana Maajabu. Ni wa kawaida sanaa.

Total football ya Barcelona ndiyo iliyombeba sanaa.

Achana kabisa na fighter asiyeogopa msitu CR7. Mzee wa popote kambi.
Yule ni balaa jingine kabisa
Hahahaha mmepatikana this time... Wewe mwite majina yote lakini ndiyo hivo Dunia imeshatambua kuwa Mfalme wa kweli ni Messi10...

Ndugu yenu si huwaga anaiga kutoka kwa Mfalme Messi10... Basi aige na ushindi wa Ballon D'or 7 ili mwendelee kubanabana pua zenu .. kenchy type!!!
 
Kwakweli huyu jamaa nilikuwa namuombea abebe hii kitu,maana mashabiki wa yule mpuuzi mwenye mpira wa kulazimisha walikuwa wanamnanga Messi kwa kutobeba kombe akiwa na Argentina.

Halafu jamaa kajitahidi sana kuliko huyo Penaldo.Kaifikisha timu fainali 3,ikiwemo ya World Cup (sijui ni lini Ronaldo atavaa medali ya mshindi wa 2 wa WC ?). Kwenye Copa America iliyoisha leo Messi ama kafunga au katoa assist kwenye kila ushindi iliopata Argentina. Yule 'Mr.Misifa' anayaweza haya?
Waaambie mkuu,LM ni kiumbe mwngine achana na huyo anaetafuta likes Insta ka Sepenga
 
Fainal CR7 alikua majeruhi!!!?

Sema alitolewa nje baada ya kupata majeruhi bwana tim mess bwanaa😂😂😂😂

Kelele nyingi na huyo ndujeru wenu utadhani kashinda kombe la dunia.

Messi hana Maajabu. Ni wa kawaida sanaa.

Total football ya Barcelona ndiyo iliyombeba sanaa.

Achana kabisa na fighter asiyeogopa msitu CR7. Mzee wa popote kambi.
Yule ni balaa jingine kabisa
Kambi ya penati😂😂
 
OFFICIAL: Cristiano Ronaldo wins THE EURO 2020 GOLDEN BOOT AWARD

Cristiano Ronaldo becomes the FIRST PLAYER in the history to finish top scorer in the Champions League, Premier League, La Liga, Serie A, and Euros
1626073914968.jpg
1626073926639.jpg
 
Team Messi msisahau goal la ushindi alifunga Di Maria

Ki messi kilikua kinaruka ruka tu uwanjani
 
Google ya Buza hii hivi wewe Kati ya Messi na Ronaldo Nani anaichezesha timu yake?

Nani akikosekana kwenye timu timu yake haipati matokeo?

Hamuoni hata haya kusema eti Messi yupo kwenye timu ambayo amezungukwa na wachezaji wazuri haya angalia Man of the match,Goals na maasist yakutosha na Messi ndo anatengeneza nafasi nyingi Barcelona

Ronaldo mzee wa tapins to yeye ndo anategemea wachezaji wenzake wamfanyie kazi yeye amalizie tu
 
Kiufupi wote wako vizuri

Lakini mimi huwa naangalia sana hadi zile clips wanazofanyaga training kwenye camps zao

Nimegundua Ronaldo ni mtu anayetrain sana na anayetumia nguvu nyingi sana kujifunza mpira kwa kufanya mazoezi kwa muda mrefu hata akiwa nyumbani kwake wakati Messi huwa hatumii nguvu na wala siyo mtu wa mazoezi sana

Na hata Ronaldo naturally ni right footed ila hiyo kuchezea miguu miwili ni ile alijilazimisha tu kujua kutumia na left foot ila Messi hajataka hata kupoteza muda kujifunza kutumia right foot yeye na ule ule mguu wake wa kushoto amefanya maajabu mengi

Pique aliwahi kuulizwa nani ni bora kati ya Ronaldo na Messi akasema "to me Ronaldo is the best of all humans but Messi is not human" (in football obviously) yaani hapo ni sawa na kusema "Ronaldo is the king of football but Messi is the god of football"

Mbappe aliwahi kunukuliwa akisema "i wish i had Neymar's right foot, Messi's left foot, Ronaldo's mentality and Buffon's class" ili kuwa the best footballer the world has ever seen

Na kuna mdau mmoja aliwahi kusema "nguvu za Ronaldo mwili mzima ni sawa na nguvu za mguu wa kushoto wa Messi"

Kwahiyo kwa kifupi naweza kusema kwamba Ronaldo anaujua mpira ila Messi mpira unamjua

Ila mimi wote nawakubali na ni shabiki yao wote maana wote maajabu yao nimeyaona
 
Messi+iniesta+xavi is greater than cr7 + ozil+di maria + modric+Kareem

When u simplify

Messi is greater than cr7+di-maria+Kareem
 
Back
Top Bottom