Mashabiki wa Simba wanalalamika kuwa hata tajiri wa Simba Mo anaishi kiujanja ujanja. Inaonekana hata fedha ya usajili wa wachezaji hatoi kwa kiasi kinachotajwa.
Mo aliwahi kusema kuwa alitoa bilioni 3 za usajili wa wachezaji. Ni muda muafaka sasa atoke hadharani amtaje liyemkabidhi hizo bilioni 3.
Kumfukuza Mangungu peke yake lkn tajiri mbabaifu Mo kuendelea kubakia hawezi kutatua tatizo
Hata hivyo nawalaumu mashabiki wa Simba kichelewa kugundua huu ujanja ujanja wa Mo.
Kigwangala alipohoji juu ya uwekezaji wa Mo mwaka juzi mashabiki hawa hawa walimuandama sana Kigwangala na kumlinda Mo. Leo kiko wapi?