Mashabiki wa Simba na Yanga Wangekuwa Wanaijenga Nchi, Tanzania Ingekuwa Singapore: Taifa la Wapumbavu wasioelewa dhana ya Vipaumbele

Wao 1 Sisi 6
1738430637004.jpg

Yaani tunashinda halafu mleta mada anatusimanga
 
Ukweli mtupu.
Madhara yake hatutayaona Sasa.

Huwa nashangaa Sana Jitu linasimama Bungeni linaanza kuongea kwanza Usimba na Uyanga.

No hard feelings, ila kama Taifa tumepoteza sana mwelekeo Kwa kuweka kipaumbele kwenye mambo yasiyo na Tija.
 
Kila mwaka, kila msimu, kila mechi – Simba na Yanga. Mashabiki wanapiga kelele, wanavunja viti, wanalia, na wengine wanashindwa hata kulipa kodi za nyumba kwa sababu ya klabu wanazoabudu kama mungu wa mitala. Soka? Hapana, huu ni upumbavu wa kiwango cha kimataifa.

Wanavalia jezi, wanajichora nyuso, wanajipaka rangi, wanajitolea sadaka kwa timu ambazo hazijui hata majina yao. Wakati mchezaji anahamia klabu nyingine kwa dau la mamilioni, mshabiki mjinga yupo hapa akihangaika na 'ushikaji wa damu' wa timu yake. Eti "Simba damu!" au "Yanga mpaka kufa!" Umefanya nini kwa jamii yako zaidi ya kupiga kelele na kubishana vijiweni?

TIMU ZIMEJAA VIONGOZI NA WAWEKEZAJI MATAPELI

Haya sasa, hebu tuzungumze kuhusu uongozi wa hizi timu. Yaani, ni kama kaburi la azimio la wezi na matapeli. Huko Simba, tulisikia kuna mwekezaji aliyesema ameweka bilioni 20. Mpaka leo, hakuna bank statement, hakuna ushahidi wa pesa hizo, lakini mashabiki bado wanabishana ovyo kwenye mitandao. Ukitaka kuona ujinga wa kitaifa, angalia watu wazima wanavyochambiana kuhusu pesa ambayo hata haijawahi kuthibitishwa kuwepo.

Huko Yanga nayo, kila siku ni maneno matupu—"ah, sasa hivi tumeimarika, huu ni mwaka wetu!" Kila mwaka ni huo huo, lakini madeni hayalipiwi, wachezaji wanadai mishahara, na viongozi wanakula hela zao kimyakimya huku mashabiki wakifurahia ahadi za hewa.

Katika nchi zilizoendelea, timu zinakuwa na uwazi wa kifedha. Ukiambiwa fulani amewekeza kiasi fulani, kuna ripoti rasmi, kuna taarifa za benki, na mashabiki wana haki ya kujua pesa hizo ziliingia lini na zinatumika vipi. Lakini hapa kwetu? Ni maigizo ya vichekesho vya mitaani.

MPIRA UMEKULA MUDA NA ATTENTION YA TAIFA

Tanzania ni nchi maskini. Tuna matatizo ya elimu duni, huduma mbovu za afya, ukosefu wa ajira, na maendeleo duni ya viwanda. Lakini cha kushangaza, meza za majadiliano ya kitaifa zinatawaliwa na Simba na Yanga badala ya kujadili mustakabali wa nchi.

Wiki kadhaa zilizopita nilikaa sehemu fulani nikiwa napambana na hamu ya kunywa bia (nimeacha ulevi lakini ni changamoto ya siku kwa siku). Nilisikia makelele kutoka bar ya jirani. Ingawa sio mpenzi wa mpira, niliamua kujongea nione kinachoendelea. Nikaambiwa Yanga ipo ICU, hivyo nikakaa kuona hatma ya mtani wa jadi.

Lakini baada ya muda mfupi, interest ya mechi hiyo iliyeyuka kabisa. Badala yake, nikaanza kufanya observation ya jamii iliyokuwa hyperfocused na hiyo mechi. Nilitazama nje ya ile bar na kugundua kuwa sehemu nyingine tatu pia zilikuwa zimekusanya makundi makubwa ya watu wakiangalia mechi kwa umakini mkubwa. Kwa mara ya kwanza, nikaelewa jinsi dola mbalimbali duniani zinavyotumia michezo na burudani kama DAWA ya kupumbaza akili za watu; lundo hili lote la watu linashindwa kujikusanya kutafuta suluhu ya kuongezeka kwa gharama za maisha lakini litakusanyika kila baada ya muda fulani kuangalia watu 22 wakigombania mpira kwenye nyasi.

MAANA YA “ROMAN CIRCUS” NA “MKATE NA TAMASHA”

Nadharia hii ina mizizi yake katika msemo wa Kirumi panem et circenses, au “mkate na tamasha,” ambapo viongozi wa Kirumi walikuwa wanatoa burudani za bure kama njia ya kuwanyamazisha watu ili wasishughulike na masuala nyeti ya kisiasa na kijamii.

Mchambuzi Bill Cooper aliwahi kusema:
"Ni kama tamasha la Kirumi. Mfalme anafanya nini watu wanapoanza kuhoji na kupinga sera zake? Anawatuma kwenye tamasha! Analeta tamasha, analijaza uwanja mkubwa, na anaanza kutupa Wakristo kwenye simba. Anapanga mashindano ya magari ya farasi. Anapanga michezo ya mpira. Na michezo mingine ya kuwashughulisha watu na mambo ambayo hayana maana katika taswira nzima ya dunia."

Katika mtazamo huu, michezo na burudani siyo tu kwamba zimekuja kwa bahati, bali ni mbinu iliyopangwa kwa makusudi ili kufunika changamoto halisi zinazokumba jamii. Wananchi wanapojikita kwa bidii kwenye burudani hizi, hawatakuwa na nafasi wala ari ya kuhoji masuala makubwa kama uongezekaji wa gharama za maisha, haki zao za kijamii, au uwajibikaji wa viongozi wa kisiasa.

ATHARI ZA UTAMADUNI WA UNUNUZI NA BURUDANI

Mbali na michezo, tunao utamaduni wa ununuzi, ambao umechochewa sana na matangazo ya kibiashara na vyombo vya habari. Watu wanasisitizwa kununua bidhaa mpya, kutamani vitu ambavyo kwa kweli haviongezi thamani ya maisha yao, na kufuata mitindo mipya ili waweze kuonekana wamefaulu au kufikia kiwango fulani cha jamii.

Hii ina maana kwamba badala ya kufikiria kwa makini jinsi ya kuboresha maisha yao na ya jamii kwa ujumla, watu wengi wanabaki wakiwa wamenaswa katika mduara wa kununua na kumiliki. Matokeo yake, wanatumia muda mwingi na rasilimali zao katika kufuata hali ya umaarufu na matumizi, wakifumba macho kwa masuala ya msingi yanayohusu maisha yao ya kila siku na ufanisi wa jamii wanamoishi.

Hali hii ni mbaya kiasi kwamba kuna watu wapo tayari kugombana na kuvunjika miguu kwa ajili ya timu zisizowajua. Kipa akiteleza na kufungwa goli la kipuuzi, ghafla taifa linatetemeka. Yaani, mtu hana mbele wala nyuma, lakini kwa sababu tu timu yake imeshinda, anasherehekea kana kwamba maisha yake yamebadilika. Ujinga upi huu?

Katika nchi zilizoendelea kama Ujerumani, Uingereza, au hata Marekani, michezo ina nafasi yake, lakini mjadala wa kitaifa hauishii tu kwenye ligi za soka. Wanajadili teknolojia mpya, maendeleo ya uchumi, mustakabali wa elimu, na mwelekeo wa taifa. Sisi je? Tuna fursa gani nyingine za majadiliano ya maana? Hakuna, kwa sababu Simba na Yanga zimekula akili za wengi.

TAFAKARI NA KUAMKA

Kila mtu ana haki ya burudani, lakini inapofika hatua ambapo taifa zima linapumbazwa na michezo huku changamoto halisi zikizidi kuwa kubwa, ni lazima tujiulize maswali magumu. Hivi kweli huu mpira unatusaidia nini kwa kiwango hiki? Kama watu wanaweza kujikusanya kwa ajili ya mechi, mbona hawawezi kujikusanya kwa ajili ya kudai haki zao?

Simba na Yanga zitacheza, zitashinda, zitafungwa, lakini ujinga wenu unabaki pale pale. Mwisho wa siku, hakuna anayewajali – zaidi ya ujinga wenu wenyewe.

Tafuteni pesa, fanyeni maendeleo, msijitumbukize kwenye ujinga wa Simba na Yanga kana kwamba maisha yenu yanategemea mechi za ligi kuu. Mtaamka lini?
Nakuunga mkono 💯 na hii inachangiwa na vyombo vya habari. Wana- promote sana michezo na miziki kuliko vitu vingine vya maana.
Watu wanashabikia mpira ya ulaya utafikiri wana ubia huku.
Ukitaka kujua mchango wa vyombo vya habari katika jamii, angalia vijana wanavyohangaika na mziki, ku-bet. Kutwa kucha radio za binafsi hata za umma ni kipromote yasiyojenga jamii.
 
📌📌Ukifatilia kwa karibu mashabiki wote wa mpira wanamatatizo ya akili.Hivyo mpira kwao ni kichaka cha kutolea stress zao.

Watanzania wengi wamejikatia tamaa ya maisha.Hasira zote wanazihamishia kwenye mambo ya kipuuzi kama ulevi,ngono,kamari na ushabiki wa mpira.
 
Kesho kuna harusi ya Aziz Ki na Hamisa Mobeto..usipange kukosa katika kisimbuzi cha Azam chanell ya Zamaradi TV...
Just for refreshment mpendwa...
Life ni zito kuwa serious sana..wengine ni washabiki humu tuu JF..ukikutana na sisi huwezi kusikia tunazungumzia mpira...tumejiwekea mipaka...
 
ORGASM ya ushindi wa timu haina tofauti na ya K ya mwanamke au madawa ya kupumbaza. Ni addictuon kama addiction zingine na inapumbaza mwili sawa na tendo la me na ke. Kama hujawahi pata ORGASM hio utaona mpira ni upuuzi. Kuuepuka hio org au furaha basi mtu asipende mpira sawa na kuepuka K ili asiwe addicted na org ya K.
Niliipata ORG hio mechi ya FRANCE VS ARGENTNA its very dangerous unaweza vua nguo mbele ya kadamnas.
Sasa kama mashabiki kindaki ndaki huwa wanaipata hio hali mara nyingi basi hawata acha hio DOPAMINE ACTIvATION.
 
Kila mwaka, kila msimu, kila mechi – Simba na Yanga. Mashabiki wanapiga kelele, wanavunja viti, wanalia, na wengine wanashindwa hata kulipa kodi za nyumba kwa sababu ya klabu wanazoabudu kama mungu wa mitala. Soka? Hapana, huu ni upumbavu wa kiwango cha kimataifa.

Wanavalia jezi, wanajichora nyuso, wanajipaka rangi, wanajitolea sadaka kwa timu ambazo hazijui hata majina yao. Wakati mchezaji anahamia klabu nyingine kwa dau la mamilioni, mshabiki mjinga yupo hapa akihangaika na 'ushikaji wa damu' wa timu yake. Eti "Simba damu!" au "Yanga mpaka kufa!" Umefanya nini kwa jamii yako zaidi ya kupiga kelele na kubishana vijiweni?

TIMU ZIMEJAA VIONGOZI NA WAWEKEZAJI MATAPELI

Haya sasa, hebu tuzungumze kuhusu uongozi wa hizi timu. Yaani, ni kama kaburi la azimio la wezi na matapeli. Huko Simba, tulisikia kuna mwekezaji aliyesema ameweka bilioni 20. Mpaka leo, hakuna bank statement, hakuna ushahidi wa pesa hizo, lakini mashabiki bado wanabishana ovyo kwenye mitandao. Ukitaka kuona ujinga wa kitaifa, angalia watu wazima wanavyochambiana kuhusu pesa ambayo hata haijawahi kuthibitishwa kuwepo.

Huko Yanga nayo, kila siku ni maneno matupu—"ah, sasa hivi tumeimarika, huu ni mwaka wetu!" Kila mwaka ni huo huo, lakini madeni hayalipiwi, wachezaji wanadai mishahara, na viongozi wanakula hela zao kimyakimya huku mashabiki wakifurahia ahadi za hewa.

Katika nchi zilizoendelea, timu zinakuwa na uwazi wa kifedha. Ukiambiwa fulani amewekeza kiasi fulani, kuna ripoti rasmi, kuna taarifa za benki, na mashabiki wana haki ya kujua pesa hizo ziliingia lini na zinatumika vipi. Lakini hapa kwetu? Ni maigizo ya vichekesho vya mitaani.

MPIRA UMEKULA MUDA NA ATTENTION YA TAIFA

Tanzania ni nchi maskini. Tuna matatizo ya elimu duni, huduma mbovu za afya, ukosefu wa ajira, na maendeleo duni ya viwanda. Lakini cha kushangaza, meza za majadiliano ya kitaifa zinatawaliwa na Simba na Yanga badala ya kujadili mustakabali wa nchi.

Wiki kadhaa zilizopita nilikaa sehemu fulani nikiwa napambana na hamu ya kunywa bia (nimeacha ulevi lakini ni changamoto ya siku kwa siku). Nilisikia makelele kutoka bar ya jirani. Ingawa sio mpenzi wa mpira, niliamua kujongea nione kinachoendelea. Nikaambiwa Yanga ipo ICU, hivyo nikakaa kuona hatma ya mtani wa jadi.

Lakini baada ya muda mfupi, interest ya mechi hiyo iliyeyuka kabisa. Badala yake, nikaanza kufanya observation ya jamii iliyokuwa hyperfocused na hiyo mechi. Nilitazama nje ya ile bar na kugundua kuwa sehemu nyingine tatu pia zilikuwa zimekusanya makundi makubwa ya watu wakiangalia mechi kwa umakini mkubwa. Kwa mara ya kwanza, nikaelewa jinsi dola mbalimbali duniani zinavyotumia michezo na burudani kama DAWA ya kupumbaza akili za watu; lundo hili lote la watu linashindwa kujikusanya kutafuta suluhu ya kuongezeka kwa gharama za maisha lakini litakusanyika kila baada ya muda fulani kuangalia watu 22 wakigombania mpira kwenye nyasi.

MAANA YA “ROMAN CIRCUS” NA “MKATE NA TAMASHA”

Nadharia hii ina mizizi yake katika msemo wa Kirumi panem et circenses, au “mkate na tamasha,” ambapo viongozi wa Kirumi walikuwa wanatoa burudani za bure kama njia ya kuwanyamazisha watu ili wasishughulike na masuala nyeti ya kisiasa na kijamii.

Mchambuzi Bill Cooper aliwahi kusema:
"Ni kama tamasha la Kirumi. Mfalme anafanya nini watu wanapoanza kuhoji na kupinga sera zake? Anawatuma kwenye tamasha! Analeta tamasha, analijaza uwanja mkubwa, na anaanza kutupa Wakristo kwenye simba. Anapanga mashindano ya magari ya farasi. Anapanga michezo ya mpira. Na michezo mingine ya kuwashughulisha watu na mambo ambayo hayana maana katika taswira nzima ya dunia."

Katika mtazamo huu, michezo na burudani siyo tu kwamba zimekuja kwa bahati, bali ni mbinu iliyopangwa kwa makusudi ili kufunika changamoto halisi zinazokumba jamii. Wananchi wanapojikita kwa bidii kwenye burudani hizi, hawatakuwa na nafasi wala ari ya kuhoji masuala makubwa kama uongezekaji wa gharama za maisha, haki zao za kijamii, au uwajibikaji wa viongozi wa kisiasa.

ATHARI ZA UTAMADUNI WA UNUNUZI NA BURUDANI

Mbali na michezo, tunao utamaduni wa ununuzi, ambao umechochewa sana na matangazo ya kibiashara na vyombo vya habari. Watu wanasisitizwa kununua bidhaa mpya, kutamani vitu ambavyo kwa kweli haviongezi thamani ya maisha yao, na kufuata mitindo mipya ili waweze kuonekana wamefaulu au kufikia kiwango fulani cha jamii.

Hii ina maana kwamba badala ya kufikiria kwa makini jinsi ya kuboresha maisha yao na ya jamii kwa ujumla, watu wengi wanabaki wakiwa wamenaswa katika mduara wa kununua na kumiliki. Matokeo yake, wanatumia muda mwingi na rasilimali zao katika kufuata hali ya umaarufu na matumizi, wakifumba macho kwa masuala ya msingi yanayohusu maisha yao ya kila siku na ufanisi wa jamii wanamoishi.

Hali hii ni mbaya kiasi kwamba kuna watu wapo tayari kugombana na kuvunjika miguu kwa ajili ya timu zisizowajua. Kipa akiteleza na kufungwa goli la kipuuzi, ghafla taifa linatetemeka. Yaani, mtu hana mbele wala nyuma, lakini kwa sababu tu timu yake imeshinda, anasherehekea kana kwamba maisha yake yamebadilika. Ujinga upi huu?

Katika nchi zilizoendelea kama Ujerumani, Uingereza, au hata Marekani, michezo ina nafasi yake, lakini mjadala wa kitaifa hauishii tu kwenye ligi za soka. Wanajadili teknolojia mpya, maendeleo ya uchumi, mustakabali wa elimu, na mwelekeo wa taifa. Sisi je? Tuna fursa gani nyingine za majadiliano ya maana? Hakuna, kwa sababu Simba na Yanga zimekula akili za wengi.

TAFAKARI NA KUAMKA

Kila mtu ana haki ya burudani, lakini inapofika hatua ambapo taifa zima linapumbazwa na michezo huku changamoto halisi zikizidi kuwa kubwa, ni lazima tujiulize maswali magumu. Hivi kweli huu mpira unatusaidia nini kwa kiwango hiki? Kama watu wanaweza kujikusanya kwa ajili ya mechi, mbona hawawezi kujikusanya kwa ajili ya kudai haki zao?

Simba na Yanga zitacheza, zitashinda, zitafungwa, lakini ujinga wenu unabaki pale pale. Mwisho wa siku, hakuna anayewajali – zaidi ya ujinga wenu wenyewe.

Tafuteni pesa, fanyeni maendeleo, msijitumbukize kwenye ujinga wa Simba na Yanga kana kwamba maisha yenu yanategemea mechi za ligi kuu. Mtaamka lini?
Uchambuzi wa mpira kutwa nzima ni mpango wa CCM kuwawezesha watawale kwa rahazao.
 
Dunia ndivyo ilivyo,Mambo ya maana Huwa hayana kipao mbele!
 
Back
Top Bottom