Mashabiki wa Simba SC tumechoka masimango, tunarudisha msaada wenu matibabu

Nategemea kutoka sasa Manara atakuwa amejifunza faida za kuwa na mdomo mchafu.

Yaani unamuibia ng'ombe Mmasai ukitegemea akikumata atakupeleka polisi? Nigga?
 
Hautakuwa uamuzi sahihi kwa sababu: 1.Zilizochangwa ni Shilingi milioni moja, lakini upendo, huruma, imani na uungwana uliooneshwa kwa fedha hizo hauwezi kupimika kwa pesa. Wema uliotangulia hakuna cha kuulipa. 2. Waliochanga pesa hizo ili zirejeshwe siyo waliopokea hizo milioni moja za awali, na wala aliyepewa fedha hizo hakuomba kwanza ridhaa ya hao wanaomchangia sasa hivi kabla ya kuzipokea. 3. Kuna uhakika gani kuwa hao wanaosemekana kutoa masimango ndiyo waliochangia hizo milioni za awali? 4. Aliyekabidhiwa huo mchango wa milioni moja aliwahi kutoa shukrani kwa wote waliochangia matibabu yake. Kurejesha fedha hizo hakutafuta shukurani hizo, na kwa hivyo kama ni masimango hayawezi kufutika kwa kurejesha hizo fedha.

Waingereza husema ’you can not unring a bell’. Kutoa mchango aliopewa na washabiki kwa ajili ya wagonjwa wengine hakutafuta ukweli kwamb aliwahi kusaidiwa hizo milioni moja. Na haitamaanisha kwamba amewarejeshea waliomchangia hiyo fedha. 5. Kurejesha fedha hiyo ni kutibu dalili za maradhi (symptoms), si maradhi yenyewe. Atafute sababu za masimango hayo, na akishaijua aifanyie kazi. 6. Sababu anaweza kuipata hata kwenye maelezo yake tu, pale anaposema hakuzaliwa huko alikokutaja. Kauli kama hizo ndiyo huzaa jawabu zisizopendeza, ambazo huishia kutafsirika kuwa ni masimango. 6. Kauli za hawa wanaoitwa wasemaji wa vilabu zinatia aibu mpira wa Tanzania, kwa sababu kwanza zinawanyima wenye nafasi zao kufanya kazi zao (makocha waseme nini kama maelezo ya kiufundi yanamalizwa na wasemaji? n.k), kadhalika yanachochea vurugu dhidi yao pale maelezo yao yanapokuja kuwa tofauti na matokeo uwanjani, isitoshe ni kinyume na maadili kwa sababu majvuno yao yanaondoka kwenye kuwa utani na kuelekea kuwa kejeli, dharau, udhalilishaji na mara nyengine kuwa matusi kabisa. Yote hayo yanafanyika huku washabiki wao wakifurahia. Lakini wao wanapojibiwa kejeli, dharau, manyanyaso na matusi hayo washabiki haohao hujifanya kutoelewa ni kwa nini. 7.

Thobias Kifaru, Jerry Muro, Masau Bwire, Haji Manara, Antonio Nugaz ..... nani haijapata msukosuko kutoka kwa wapenzi wake au wa wapinzani wao pale majigambo, kebehi na jeuri zao zinapokuwa ni tofauti na matokeo ya mechi husika? Lini Jaffar Idd wa Azam amekutana na misukosuko hiyo? Hatujiulizi kwa nini? 8. Kuna yeyote kati yetu anayejua msemaji wa Real Madrid, Bayern Munich, Juventus, Man City au timu yoyote kubwa ya Ulaya? Hawa wa kwetu wametoa wapi mtindo huu?

Washabiki tuwatake wasemaji wetu wasivuke mipaka katika kauli zao, ili na wao wasivukiwe mipaka wakati wa kujibiwa. Msemaji au timu yake anapohisi ametukanwa na msemaji mwengine. Hilo ni rahisi kutokea kwa sababu tofauti baina ya kejeli na tusi ni ndogo mno. Kinachofuata ni yeye naye kujibu alilolihisi kuwa ni tusi. Wazee wetu hawakuwa wamelewa pale waliposema ‘akutukanaye hakuchagulii tusi’.
 

Usikurupuke soma Mistari kwa Makini!

Hoja si kuchangiwa hapa! Point ni kwamba Yeye alichangiwa na WASHABIKI WA YANGA lakini shida ni pale anapojitokeza Mtu akajisifu kwenye Mitandao kuwa Kamtibu yeye kama yeye

Manara yeye mwenyewe anakubali kuwa Kachangiwa na Washabiki wa Yanga ambapo hata huyo Jerry Murro mwenyewe hakujuwa huo mchango ulianzaje!

Lakini leo anajitapa kuwa eti alitoa yeye hela za kumtibu.
 
Kweli usemalo Mkuu na kwa kipindi kile ubavu wa kutopokea hakuwa nao si unaona alivyokuwa kadhohofika.

Mashabiki wa 5imba wazungumze wanavyozungumza ila mwisho wa siku anajifurahisha tu huyo na itabakia siku zote kwamba katika kupona macho yake na mkono wa YANGA BABALAO upo.
 
Hajaomba msaada wenu halafu hiyo hela ni group tu la whatsapp ya Yanga walichanga na haikuwa hela iliyotoka as official help kutoka Yanga

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa Mtani mbona unakataa halafu unakubali. Lol.

Kama lilichanga group la Yanga mbona hela alisema anazirudisha kwa Uongozi wa Yanga na si kwa hilo group?

Kubalini tu kwamba na sisi ni sehemu ya hapo alipo.
 
Mk Mambo mengine yanakera ...huu Sasa so utani!
Sema wewe. Hapa ndio ujue dhahiri alishikwa pabaya na utani hauwezi.

Nimeona sehemu kumerushwa picha akiwa pale Jangwani halafu anadai wazee wamemsihi asizirudishe. Sasa si wehu huo alionao.

#WashauriwaManaramuwemnatumiaakili.
 
Kwahiyo iyo 1M iliyochangwa na Vyura Fanboys ndiyo pekee iliyompeleka India au?

Vyura akili zao fupi sana.
Hiyo hela ilikuwa ni sehemu ya yeye kumfanya aende huko India.

Wala akili zetu hazina Ufupi wowote Mtani. Manara ndio ana akili fupi.
 
Mmmh!! Mbona kama na wewe umeingia chaka Mtani.

Sasa nawaza kama aliyejitokeza kumkashifu si sehemu ya waliochanga anazirudisha za nini sasa? 🤔🤔

Tuseme tu Manara akili zake anazijua mwenyewe kwa kweli.
 
Wee koma wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KAULI YA MANARA HIYO "Heri nego kavu na utulivu kuliko karamu ya Mfalme na machafuko ‘Bible’
Nilikwenda mwenyewe mchana huu klabuni Yanga,bahati mbaya sana sikuwakuta viongozi wa klabu, Wazee niliowakuta nje baada ya kuwaeleza nimekuja kukabidhi pesa za masimango walinisihi sana nisifanye hvyo na wakaniambia yule ni mgeni hapa mjini na hajui tamaduni zetu na kuniomba nisirejeshe hata thumni.

Nimefundishwa kuwatii wazee, na ntarejea kwa Wanasimba walionikabidhi pesa zao,,,busara itawashauri tupeleke hospitali kwa wagonjwa wasiojiweza, ikiwapendeza tutafanya hvyo!!

Kwetu nimefundishwa uungwana,,kwetu nimepata malezi bora,,kwetu wazazi wangu walinijaza na Jeuri ya kutokubali kuonewa wala kunyanyaswa, halafu mm sijatoka Mbwinde,,hilo ni Muhimu sana na ndio maana naweza kuwa Msemaji pekee naweza kwenda klabu nyingine tena mchana kweupeeeee."

TUKISEMA HUYU JAMAA HAFIKIRI KABLA YA KUTENDA MUWAGE MNAKUBALI.

SASA HUKO HOSPITALI ATAKAKOZIPELEKA NDIO ITAKUWA IMEFUTA KUSAIDIWA NA HILO MNALOLIITA KUNDI LA YANGA?

#MBUMBUMBUATABAKIAKUWAMBUMBUMBUTUSIKUZOTE.
 
Unafuatilia lakin sakata hili au unakurupuka tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni hivyo, kwa nini hiyo hela asimrejeshee huyo Muro, hata kama ni kwa Tigopesa?
 

Tatizo lako ni kwamba unatanguliza mashambulizi bila ya kueleza hasa hiyo point yako ni nini!

Katika hiii post yako hasa umekusudia kueleza kitu gani?
 
Kama ni hivyo, kwa nini hiyo hela asimrejeshee huyo Muro, hata kama ni kwa Tigopesa?

Hiyo hela Muro haimhusu sasa arushiwe yeye kama nani?

Pesa imechangwa na mashabiki wa Yanga ambao hata yeye manara hawezi kuwatrace na kiwajuwa ni kina nani na ni wangapi.

Kwahiyo ndiyo wakati uwezekano wa kuwatafuta akawarudishia hela haupo ndiyo akaona bora azirudishe Klabuni kwao.
 
Tatizo lako ni kwamba unatanguliza mashambulizi bila ya kueleza hasa hiyo point yako ni nini!

Katika hiii post yako hasa umekusudia kueleza kitu gani?
Nimekusudia kueleza kwamba huyo Manara wenu aache kukurupuka.

Sababu yote yanayotokea alipaswa kuyafikiria kabla na sio kusubiria eti ashauriwe sijui wamsihi wazee tena wa Timu ya wananchi 😎 kwamba asirudishe hiyo pesa. Lol.
 
Huo ndio Umbumbumbu alio nao Manara sasa mana hata hiyo Klabu itashangaa anapeleka hiyo pesa nani kamdai mana walishasema Jerry Muro yote anayoyasema na anayoyafanya anayafanya kama shabiki na Mwanachama wa Yanga na si sehemu ya kauli za Klabu ya Yanga.

Hivyo nyie wenye upeo muwe mnamshauri huyo Manara wenu.

Tunajua alipigwa za chembe ila angetumia utu uzima wake kufanya utatuzi. Teh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…