Mashabiki wa Simba tuache kiburi cha mafanikio!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Imagine leo Simba pamoja na mafanikio ya kila aina ikiwemo ushindi na mpira safi leo alafu kuna mashabiki wanalalamika kwamba kocha kwanini hampangi Phiri!

Kweli game ya bonanza, pamoja na mafanikio yote tunaanza kuhoji kwanini leo Phiri hajacheza? Hivi tunajiona sisi ni zaidi ya Barcelona? Hivi tunafikiri kocha haoni maoni yenu ya kifala? Mnataka tubadili kocha tena kizembe kisa Phiri hajapangwa?

Hapa niwasifu mashabiki wa Yanga, kiukweli wamejaa ukomavu ambao ni wa kipekee sana. Hivi tungegeuza upande leo Simba kungekalika kweli? Pamoja na hamasa tuliyonayo mashabiki wa Simba lakini tumejaa ujinga wa kushangaza sana!

Tuache ujuha, ujinga, na upunguani! Hatuna timu ya dhahabu kiasi ya kufanya tujione tunapaswa kufanya miracles za mbinguni. Tuuunge mkono timu na viongozi na kuacha malalamiko ya kipuuzi hasa kwa kocha.

Hii ni kwa mashabiki maandazi!!!.

Simba #nguvumoja
 
Bora mnaoona mafanikio na kasoro. Wengine wameona mazuri pekee kiasi cha kutaka Kila mchezaji acheze utadhani kulikuwa na Kombe.
 
Hakukua na sababu za Saido na Kibu kucheza muda wote ule!
Saido ni kati ya wachezaji walioharibu move toka kipindi cha kwanza, control na pass zake ni za hovyo
 
Hakukua na sababu za Saido na Kibu kucheza muda wote ule!
Saido ni kati ya wachezaji walioharibu move toka kipindi cha kwanza, control na pass zake ni za hovyo
Wewe ni moja ya shabiki maandazi. Hivi ungekuwa shabiki wa Uto si ungezikwa Mayele kuondoka? Imagine Simba waondoke wachezaji tegemeo tena waende Azam na Yanga, MO angepokea matusi mangapi?

Imagine Yanga wana matumaini na akina Skudu pamoja na mchezo mbovu mno siku ya wananchi. Acheni ushabiki maandazi.
 
Kocha wenu hana sababu yoyote ya kumweka nje phiri dk zote 90' kwenye friend metch na kumwanzisha Kibu.
Kocha wenu ana penda wachezaji wenye matumizi makubwa ya Nguvu ndio maana hata Ngoma hawezi kuwa ana mwanzisha ata Chama ana bahati mashabiki wali mpambania la sivyo tungesha msahau.
 
Tatizo la coach na sub ...
Coach na Phiri, Kibu na Saido halijaanza jana, toka msimu uliopita alikua hivyo!
Ni haki washabiki wa simba kutoa maoni yao( kulalamika). Kama Phiri hafai wamwache aondoke! Hakukua na sababu yoyote ya Msingi ya Saido kurudi Sec half, Ni mchezaji mwenye makosa mengi uwanjani.
 
Maswala ya kumuacha Phiri wewe hayakuhusu......
Kama shabiki, Unachotakiwa kujudge Ni performance ya timu.
Sio kwanini fulani na fulani hawachezi.
 
Mechi yenu imeishaje leo?
 
We umepita kwa kila mwanachama wa uto kusikiliza maoni yao baada ya mayele kuondoka?.
Ukweli kocha amezidi..inamaana hakuona kuna haja ya kufanya sub mapema kumtoa kibu au saidoo..kama ilikua ni bonanza kwanini asimpange Phiri ali arejee katk hali yake baada ya majeraha? Ni maoni na mtazamo wetu...kocha amezidiiiiiii amezidiiiii
 
Moses bila kupambaniwa na mashabiki hatoboi, kocha ameonesha dhahiri hamtaki.


Tangu aumie hajawahi kumuamini tena pamoja na kiwango bora sana alichoonesha kabla hajaumia.

Kama sio matakwa ya kocha kumuweka benchi Phiri, basi uchawi wa misitu ya Congo uko kazini
 
This is maturity. mashabiki ndiyo wanaziharibu teams zetu. Uongozi umefanya nafasi yake, mashabiki wakahamasika na kujitokeza kwa wingi, kwanini wasimuache coach afanye kazi yake?
 
Mashabiki hawafanani....

Nikiwa mchawi wa mafanikio ya Simba kiupekee kabisa nachukua nafasi hii kuwapongeza watani zetu....

Hakika leo ulikuwa ni UNYAMA MWINGI katika maeneo mengi....

Nitaongelea kuhusu ndani ya dimba....

Yule Che Malone yulee...jamaa yuko "composed" sana...akili nyingi ,uwezo mkubwa wa markings"...nguvu anazo....mguuni ana vitu mno...hakika INONGA atapumua kucheza "Jihad" pekee....

Mzamiru....

Silioni pengo la jamaa yetu JONAS MKUDE(Jiwe walilokataa waashi)....

Kiungo Punda atapunguziwa kuhaha....pale kati kwa sasa ni [emoji91]...

Jamaa yetu Kennedy ajiangalie sana kuhusu yule "Job" wa SSC(H Kazi)....Hamis mwingine mmempata [emoji1787]

Eti CCC hana mbiooo....uongo mtupu [emoji1787][emoji1787]

Kumbe jamaa huwa "anaspeed" panapohitajika tu na si kama yule jamaa yetu wa zamani Nchimbi [emoji1787][emoji1787]

Luis Jose M mguuni bado ana vitu...ninamuona amejiongezea uzoefu na hwenda tusione akiwa anakimbiakimbia sana kama kipindi cha nyuma(hapa wenye MBANGO) wawe makini napo sana[emoji1787][emoji1787] ila mechi chache zitampunguzia "uzito" alionao sijajua ni UROJO wa Misri na kutokuwepo uwanjani sana ?[emoji1787][emoji1787]

Kongole watani zetu kwani ukimlaumu Onana kwa mbwembwe nyingi katika SIKUKUU yenu basi na umkumbuke jamaa yetu M.Makudubela [emoji1787][emoji1787]

Kongole watani zetu[emoji106]

#MamaAnaupigaMwingi[emoji109]
 
Phiri aende kwa Mganga wa Lavalava amtoe gundu
 
Mbona mapema hivi
Hata Ngao ya jamii haijachezwa
 
huyu kocha anaua viwango vya wachezaji, mchezaji akitoka nje akiwa anapangwa lazima ataitwa timu ya Taifa na akiitwa ni faida pia kwa timu.
anachofanya kocha sio sahihi hata kipa hakutakiwa kucheza muda wote, hata Manura alitumia kwenye mechi ambayo ilikuwa si lazima acheze. Kwa kifupi kocha anazingua.
 
Hili la kocha kumuacha Phiri anazingua.

Angewaonesha maahabiki mtu wao, mbona mechi sio ya kimashindano ile na pia aliimudu.
 
Hii ya Phir kwakwel inaumiza imagine hujapangwa kwenye mechi zaushindani halafu kwenye mechi yamaonesho pia hupangwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…