Mashabiki wa Simba tuache kiburi cha mafanikio!

Mashabiki wa Simba tuache kiburi cha mafanikio!

Shida ya phiri haina tofauti na manula, team haitoi taarifa za kueleweka.

Nilikuwa naangalia mpira nikiwa kazini wakati wanamtambulisha manula kila mtu anasema lake, mwingine anasema kaumia mguu alikuwa anatembelea magongo, mwingine anasema kaumia mkono, mwingine nyonga.

Na pamoja kutambulishwa hatujui atakaa nje mda gani.

Lawama zinapaswa zielekezwe kwanza kwa management ya simba maana unaweza kuta phiri uturuki ilikuwa ni sehemu ya mazoezi lkn bado anahitaji mda hivyo huku tutabaki kusumbuana kumbe bench la ufundi lina yake.

Pia mliotaka aachwe nanyi mkumbuke bado ana mkataba na karibia nusu ya mwisho ya msimu alikuwa nje sasa sijui mlitaka abebwe akiwa mgonjwa na nani.
 
Wakuu,

Imagine leo Simba pamoja na mafanikio ya kila aina ikiwemo ushindi na mpira safi leo alafu kuna mashabiki wanalalamika kwamba kocha kwanini hampangi Phiri!

Kweli game ya bonanza, pamoja na mafanikio yote tunaanza kuhoji kwanini leo Phiri hajacheza? Hivi tunajiona sisi ni zaidi ya Barcelona? Hivi tunafikiri kocha haoni maoni yenu ya kifala? Mnataka tubadili kocha tena kizembe kisa Phiri hajapangwa?

Hapa niwasifu mashabiki wa Yanga, kiukweli wamejaa ukomavu ambao ni wa kipekee sana. Hivi tungegeuza upande leo Simba kungekalika kweli? Pamoja na hamasa tuliyonayo mashabiki wa Simba lakini tumejaa ujinga wa kushangaza sana!

Tuache ujuha, ujinga, na upunguani! Hatuna timu ya dhahabu kiasi ya kufanya tujione tunapaswa kufanya miracles za mbinguni. Tuuunge mkono timu na viongozi na kuacha malalamiko ya kipuuzi hasa kwa kocha.

Hii ni kwa mashabiki maandazi!!!.

Simba #nguvumoja
Na wanaolalamika wengi ni Utokolo ilimradi tu kutoa dosari kwenye tamasha la Simba.
 
Na wanaolalamika wengi ni Utokolo ilimradi tu kutoa dosari kwenye tamasha la Simba.
Wapumbavu wengi badala ya ku focus na mambo mema yaliyotokea leo wanalia na kukosekana mchezaji mmoja. Hawahawa wakitaka kocha aingie kwenye mfumo wa chama! Mashabiki wajinga
 
Ni haki yao maana saido anacheza hovyo sana na mashabiki wanaamin phir ni zaidi ya saido kifup kocha ataendelea kulaumkwa
 
Hakukua na sababu za Saido na Kibu kucheza muda wote ule!
Saido ni kati ya wachezaji walioharibu move toka kipindi cha kwanza, control na pass zake ni za hovyo
Assist zote mbili katoa saidoo
 
Wewe ni moja ya shabiki maandazi. Hivi ungekuwa shabiki wa Uto si ungezikwa Mayele kuondoka? Imagine Simba waondoke wachezaji tegemeo tena waende Azam na Yanga, MO angepokea matusi mangapi?

Imagine Yanga wana matumaini na akina Skudu pamoja na mchezo mbovu mno siku ya wananchi. Acheni ushabiki maandazi.
Mkuu Skudu kivipi unasema kacheza mchezo mbovu siku ya mwananchi?
 
Hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya timu, yeyote acheze au asicheze bado timu itabaki kitu cha muhimu zaidi. Sio Chama, sio Phiri, sio anyone... siku zote ni Simba Sc kwanza.

Hizi kelele kwanini fulani hachezi ni mihemko tu ya kupuuza, jambo la muhimu zaidi ya yote kwenye timu, siku zote, ni ushindi pekee, wala sio uwepo wa mchazaji fulani uwanjani.
 
Hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya timu, yeyote acheze au asicheze bado timu itabaki kitu cha muhimu zaidi. Sio Chama, sio Phiri, sio anyone... siku zote ni Simba Sc kwanza.

Hizi kelele kwanini fulani hachezi ni mihemko tu ya kupuuza, jambo la muhimu zaidi ya yote kwenye timu, siku zote, ni ushindi pekee, wala sio uwepo wa mchazaji fulani uwanjani.
Imagine kuna watu wanamlalamikia Kibu! Hivi bila Kibu na Boko kufunga lazima tuwatukane? Mbaya zaidi sisi washabiki wa Simba ndio tunaovunja moyo wachezaji.

Imagine game ya Yanga siku ya wananchi ilivyokuwa mbovu lakini hukuona wakilalamika kijinga. Wameondoka vifaa vyao tegemeo huoni wakitukana viongozi wakisubiri mechi zianze. Sisi Simba sasa! Dah!
 
Ni haki yao maana saido anacheza hovyo sana na mashabiki wanaamin phir ni zaidi ya saido kifup kocha ataendelea kulaumkwa
Saido anacheza vibaya kivipi mkuu ebu tueleweshe.
 
Phiri ni bonge la player bahati mbaya Sana amekutana na kocha makolokocho..
 
Phiri ni bonge la player bahati mbaya Sana amekutana na kocha makolokocho..
Naamini kocha analazimishwa kupanga wachezaji fulani fulani. Kwa mfano Bocco hata kuwepo kwenye wachezaji 30 wa kusajiliwa hakustahili. Lakini kocha analazimishwa amweke na pia aingie uwanjani kucheza mechi. Kwa hali yoyote Bocco halinganishwi na yeyote kati ya Moses Phiri au hata Habibu Kiyombo aliyetemwa.
 
Sasa basi wote tukasomee ukocha tukafundishe timu yetu wotee,manake kila mtu kocha sasa.
 
Back
Top Bottom