Mashabiki wa Simba tujiandae kisaikolojia!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wanalunyasi,

Ni vizuri kuambiana ukweli wengine msije kufa kwa pressure game na Asec. Timu yetu mpaka sasa haina kocha mkuu wala kocha wa fitness.

Timu inafanya mazoezi na waalimu ambao kwa muda huu mfupi huku wakiwa wanajua wanashikilia bomba kwa muda mfupi ni ngumu kuwa motivated!

Tunahamasishwa kwenda uwanjani bila viongozi kuonesha nia na commitment mpya baada ya kipigo cha aibu dhidi ya watani. Kwenye press zao wanajitetea tu bila kukubali kuwajibika pia.

Matatizo ya Simba kiufundi msitegemee mabadiliko makubwa sana kwa muda huu mfupi. Juma Mgunda angeweza kutusaidia kwa program fupi lakini hawa waliopewa timu tujiandae.

Swala la kocha mkuu ni dharura, linapaswa lifanyiwe kazi kidharura. Kama funds zipo kupata kocha bora sio tatizo ila kama budget ni kikwazo lazima itatuchukua muda mrefu na kutugharimu.

Game na Asec haina dalili nzuri mpaka sasa. Viongozi wetu wachangamke na pia wawe na data base ya makocha wakubwa wenye vigezo ili kutafuta kocha isiwe kama anatokea sayari nyingine.
 
Asec wanakuja wakijua wanaenda kucheza na timu kubwa iliyo shiriki AFL ko wataweka kikosi cha maangamizi.

Mwamedi pesa ya AFL kaingiza kwenye biashara zake za juisi tegemeeni kuletewa kocha muajentina wa bei chee kama ilivyokuwa kwa mbrazili yulee,
 
Una hoja usikilizwe.

Inasikitisha sana kuona wachezaji wa Simba wanafanya mazoezi ya viungo kwa kuangalia mazoezi ya kwenye videotape. Hapohapo benchi la ufundi, chawa, kamati za roho mbaya za kuwasaidia hao ASEC zipo hapa hapa Dar.
 
Wanatudanganya eti Simba ni bora kuliko Mamelody
 
Hawa Asec wa sasa hawana mpira wowote Simba akifungwa na hawa utakua ni uzembe mkubwa sana. Wanafungwa fungwa tu huko ligi ya kwao. Kwakifupi kwenye kundi la Simba akikaza anaongoza hilo kundi kuelekea robo fainali. Pamoja na ubovu wa Simba kwa sasa na kukosa kocha lakini sioni timu ya kuisumbua Simba kwenye kundi lao. Simba atakwenda robo fainali tena kwa kishindo kikuu
 
Itakua wamewekeza kwenye fitina za nje ya Uwanja.
Watawasingizia EBOLA wachezaji tegemeo wa ASEC ili wawafunge kiulaini.
 
Wamefikaje makundi?
 
Kama we ni mwana Simba,basi ndio sababu wanaSimba wengine wanatukanwa ni mbumbumbu kwa ajili ya watu kama wewe.
Kama wewe ni utopolo,hakika umefuzu kwenye uchawi mkuu.Badala ya kufurahia goli 5 wewe unakuja huku kuanza kuroga ili wachezaji waingie uwanjani na akili yako?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nafikiri bado Wana simba hawataki kusema ukweli kutokana na kuwa muddy kaitoa mbali na kuifikisha hapo japokuwa ni kwa muendelezo wa miaka 4 hivyo imepanda kiwango ila mimi naweza sema kutokana na juhudi binafsi za wachezaji, sapoti ya wana Simba, morali na hata uongozi wa babra apewe maua yake. Baada ya kuuza wachezaji wakubwa, wazuri na waliokuwa wanajituma matokeo yake kwa Sasa simba ina shida maana huenda baada ya hela kuingia simba basi MUDDY kaamua ajirudishie maana ni juhudi zake binafsi na sio hawa wamiliki wa 51% ambao hawana msaada wala kutoa hela. Mapendekezo yawe hivi.
1. Kufikia malengo, simba iamue kuwa kuanzia Sasa wachezaji wawe wanatoka nje ya nchi jirani hizi za Rwanda,burundi,kenya,uganda tuachane nao na twende huko Nigeria, ghana, Benin, South Africa, nk
2. Timu iweke mapendekezo ya kuanzishwa kwa kadi zenye hadhi maalum kuanzia za million, million mbili hadi hata 5 ili hawa wakitoa hizo hela basi kila mwaka hawatakuwa tena watoe hela za kiingilio bali ni Free pass na wawe wanaruhusiwa kwenda na timu nje ya nchi nk.
3. Watu wengine wawe wanalipia michango ya uanachama kwa njia za kadi ambazo zinaweza kuwa attached na bank kwa ajili ya kuchaji hela zao na kulipa ada zao, na hata tickets kama wako nje ya nchi au kulipia kupitia kadi zao.
4. Pia kwa watu walioko nje ya nchi nao wanaweza pata kadi zao kupitia hata kwa mawakala au utaratibu ufanyike ili wapate kadi na kulipia michango yao.
5. Walau hao wenye hadhi maalum hao watakuwa wanapata bonuses mbali mbali kama kupiga picha na wachezaji, kupata mialiko mbali mbali ya simba, kupewa jezi pindi zikija nk
6. Kujua idadi ya watu wao na michango na hata kuanzishwa kwa kadi hizo zitumike hapo hapo uwanjani ambapo akiweka kadi inaprint anaondoka.
7. Kuwepo na renewable kila mwaka.
8. Pia kuwepo na vitu vingine viwe advertised kama funguo, viatu, nk
9. Awepo afisa biashara ambae atakuwa na wajibu wa kuratibu masuala ya kibiashara kwa kutafuta wadhamini tu ndani na nje ya Tanzania nafikiri hapo tunaweza kuza Brand ya Simba.
10. Kwa kuwa simba inajitangaza pia kupitia jezi yake, Basi afisa biashara awe anatangulizwa kwenye nchi husika and then kuratibu jezi za timu ili iwapo timu inacheza basi wale washabiki wawe na jezi.
Hapo timu inaweza kuza Brand yake,kupanda kwenye chati ya timu ambazo zina hela na pia kusajili wachezaji wa bei mbaya.

Sasa kumwachia muddy kila kitu hapo wanachama wanafeli Sana na kusubiri tu kuchagua viongozi sio vizuri.

Suala la kumuuzia jamaa muddy hisa 49% napo naona kama wangewauzia watu wawili kwa kiasi cha walau billion 25 kwa nusu hisa za MUDDY na yeye atoe billion 25 ingekuwa vizuri Zaidi.

Nasikia kuwa BHAKRESA aliitaka simba ila akachomolewa kisa atakuwa na timu mbili wakati Azam ni timu ya watoto wake.

Tofauti na nilichosema,tutaishia kununua wachezaji wa buku buku,kufungwa Hovyo na muddy kutukanwa na kutaka kuiacha timu. Wachezaji wanaotakiwa Simba ni wengi na wengine wanataka ili kuonyesha makali yao ila inapokuja kwenye hela MUDDY ni mbahili na pia kuna wapigaji Sana. Tuambie kipa asie na kiwango, kocha asie na kiwango, wachezaji wazawa akina chilunda na wenzake wa bei rahisi wako wapi kama sio benchi?
Wachezaji akina okra,akra,yule beki nimesahau jina lake,na Sasa wanawaleta akina adebayor, manzoki ambao ni Free agent na hawachezi mpira kwa muda. Muddy kutoa hela ni shida ngoja ifungwe tu maana hata kumfukuza huyo kocha ni kuficha mambo yao na wachezaji wamesema ishu ni posho zao hawapewi,try again na mangungu nao wanakaa kwenye uongozi kwa sababu gani?kocha angebaki tu. Nasikia hata kocha wanaemtaka anataka hela nyingi kila wakigusa matokeo yake mgunda anarudishwa. Anyway ngoja huyo Barbra arudi tuone
 
Mwenyekiti mangungu Hadi muda huu hajaongea chochote huu si ujinga kabisa.
Hawa viongozi wameamua kuiua Simba.
Na sisi mashabiki tunasema ole wap tufungwe ndo watajua tukoje, yutawasaka nyumba Hadi nyumba, kitanda kwa kitanda

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Wanawahamasisha muende uwanjani ili wapate mapato na sio kutoa hamasa maana wanajawajua nyie mashabiki mpaka mchezaji apige chenga ndo mnashangilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…