Mashabiki wa Simba tujiandae kisaikolojia!

Mashabiki wa Simba tujiandae kisaikolojia!

Asec wanaongoza league ya kwao,pili ni moja ya timu iliyojaa vijana wadogo. Sasa ule ugoigoi wenu mkipoteza mpira hamuwahi recover mpira mnatembea,mtapigwa nyingi. Msimu huu kwenye mechi zote ulizocheza cleansheet hazidi tatu,kila mechi unamuhusu magoli.

Hapo lazima muwe na utimamu wa mwili,ili muweze kushindana na timu iliyo sheheni vijana wadogo la sivyo,mmejitahidi sana droo.
Naunga mkono hoja 👍👏
 
Hawa Asec wa sasa hawana mpira wowote Simba akifungwa na hawa utakua ni uzembe mkubwa sana. Wanafungwa fungwa tu huko ligi ya kwao. Kwakifupi kwenye kundi la Simba akikaza anaongoza hilo kundi kuelekea robo fainali. Pamoja na ubovu wa Simba kwa sasa na kukosa kocha lakini sioni timu ya kuisumbua Simba kwenye kundi lao. Simba atakwenda robo fainali tena kwa kishindo kikuu
Hahahahahaha, sawa
 
Nawalaumu saaaaana wanachama wenzetu waliomchagua Mangungo kuwa mwenyekiti kwani huyu yupo hapo kuitumia Simba kama ngazi ya kupandia kupata ubunge. Kila mwanachama wa Simba ambaye alimpa kura Mangungo ajue anahusika na anguko la Simba.
Mangungu ni mjumbe mwenye kura moja tu kwenye bodi ya Simba, kama Asha Baraka. Sallum Abdallah Mhene (Try Again) ndiye Mwenyekiti wa bodi ya Simba.

Na hiyo Bodi ndiyo inayoendesha Simba kwa mujibu wa Katiba. Na mabadiliko haya ya katiba tuliyapitisha wanachama wote, siyo Mangungu.

Lawama zako peleka panapohusika.

Ova
 
Mangungu ni mjumbe mwenye kura moja tu kwenye bodi ya Simba, kama Asha Baraka. Sallum Abdallah Mhene (Try Again) ndiye Mwenyekiti wa bodi ya Simba.

Na hiyo Bodi ndiyo inayoendesha Simba kwa mujibu wa Katiba. Na mabadiliko haya ya katiba tuliyapitisha wanachama wote, siyo Mangungu.

Lawama zako peleka panapohusika.

Ova
Sasa huko kunakohusika ni wapi b…?
Nimecheka sana

Mbona mna hasira sana jamani? Mnagombana wenyewe kwa wenyewe!
 
Sasa huko kunakohusika ni wapi b…?
Nimecheka sana

Mbona mna hasira sana jamani? Mnagombana wenyewe kwa wenyewe!
Mkuu waonee huruma bado wana maumivu, subiri bhas wapone kwanza.
 
Sisi Kama Asec tunaendelea kuratibu ulozi wenu... Mlango tutapitia ule wa nyuma km yanga ili tuwakande 4+😅
 
Ilikuwa kosa kubwa kumfukuza kocha na kutuhumu wachezaji bila ushahidi kwa kusikiliza kelele za washabiki oya oya. Nilionya kuwa japokuwa iliuma kufugwa goli tano lakini tukumbuke tuko kwenye ligi, tuangalia yajayo matokeo yake ndiyo haya. Nina uhakia asingefukuzwa kocha mchezo na Namungo tusingedondosha poin mbili ambazo ndiyo zimempa ubingwa utopolo.
Ligi bado mbichi, uto hajawa bingwa bado.
 
Asec wanakuja wakijua wanaenda kucheza na timu kubwa iliyo shiriki AFL ko wataweka kikosi cha maangamizi.

Mwamedi pesa ya AFL kaingiza kwenye biashara zake za juisi tegemeeni kuletewa kocha muajentina wa bei chee kama ilivyokuwa kwa mbrazili yulee,
Kwamba isingekuwa hivyo Asec wangepanga kikosi B au unamaanisha nn unaposema kikosi cha maangamizi
Yaani kwa uelewa wako ulifikiri Simba itamfunga Asec Mimosas kwa kuvizia apange kikosi kibovu?? [emoji849]
 
Ligi bado mbichi, uto hajawa bingwa bado.
Mshindani wa uto kwenye ubingwa ni Simba tu,sasa kwa trend hii ya Simba kushikana uchawi kila siku unafikiri uto atashindwaje kufaidika na vita hii ya ndani kwa ndani inayoendelea Simba?
 
Yani hakuna kipigo kitaniumiza kama kilichopita cha watani wa jadi, nilishindwa hadi kutoka nje ya geti.
Hata tufungwe ngapi kwa sasa sitoumia kwasababu ndicho ninachokitegemea kitokee maana Uongozi ni kama haupo na timu hamna.
Pole sana mkuu.
 
Back
Top Bottom