Mashabiki wa Simba tupo kwenye kipindi kigumu, Tunahitaji mabadiliko lasivyo tutaburuzwa hadi 2030

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
nimechoka na hii timu, Ndani inatuunguza, nje inatubabua. Huu msimu tulitegemea tutaanza kwa matumaini ya kuvunja mwiko wa vipigo mfululizo kutoka kwa watani lakini kidonda kimetoneshwa upya, tumeweka rekodi ya kufungwa mara ya sita mfululizo, hii ni aibu .

vipigo mfululizo vya derby vinafanya tuwe kichekesho kwa majirani zetu, tunaonekana MDEBWEDO.

Mimi si tu shabiki wa Simba ni shabiki wa mpira, napenda soka kwa jumla. Lakini sasa hivi, kila nikiona timu pinzani zikipiga ball safi, moyo wangu unaungua. Na nikiona Yanga wanashinda, nafsi inateketea.

Kocha wetu naye tumvulimie mara ngapi ? Wenzake watatu wamebadilishwa wote wanamfunga, Mashabiki tunasuffer mara mia zaidi yake. Tumekuwa tukimuomba nini? Timu kushinda mechi moja tu derby roho zipoe. Si zaidi, Lakini hata hilo limekuwa taabu. Na cha kusikitisha zaidi, mashabiki wa Yanga wanafurahia, wanatembea kifua mbele, sisi tunabaki na midomo imekauka.

Hii klabu kubwa ya Simba imegeuzwa kichekesho. Yanga wanatumia mechi dhidi yetu kama njia ya points za bure, Yaani wakipoteza huko points 3, wanajisemea, “ahh tukienda kucheza na Simba tutapata pointi.” Hii ni aibu kubwa kwa timu yenye historia kubwa kama yetu.

Sasa sielewi viongozi wanasubiri nini? mashabiki wanajitoa, wawekezaji wanatia pesa, lakini matokeo bado ni fedheha tupu. Hivi kwanini tusichukue hatua mapema? hata huu msimu hauna dalili nzuri, Msimu unaendelea kuwa giza, na bado tunaambiwa “subirini, ni mchakato.” Huu mchakato unatuua polepole.

Huwezi kuachana na klabu yako, lakini kila siku unajisikia majuto. kilichobaki ni kukumbuka mafanikioya Simba iliyokuwa peak 2018 hadi 2022, maana kama ni kufika fainali shirikisho hata Yanga walishafika hakuna kipya.

Ni fedheha. Ni mateso. Na ukweli ni kwamba tupo kwenye wakati mgumusasa hivi, Lakini hatuwezi kuachana na Simba. Tueipenda wenyewe acha itutese.

Tumegeuzwa timu ya kusikitikiwa lakini hatutaki huruma, tunataka ushindi. Simba tunahitaji Reforms, tunahitaji sajili nzuri, uwajibikaji kwa viongozi, vinginvyo hawa Yanga watatubabua mpaka 2030
 
nimechoka na hii timu, Ndani naungua, nje inatubabua. Huu msimu tulitegemea tutaanza kwa matumainilakini tayari watani washatukanda, tena ni mara ya sita mfululizo, naona kifo cha ukubwa wa Simba.

vipigo fululizo vya derby vinafanya tuwe kichekesho kwa majirani zetu, tunaonekana MDEBWEDO.

Mimi si tu shabiki wa Simba ni shabiki wa mpira, napenda soka kwa jumla. Lakini sasa hivi, kila nikiona timu pinzani zikipiga ball safi, moyo wangu unaungua. Na nikiona Yanga wanashinda, nafsi inateketea.

Kocha wetu naye tumvulimie mara ngapi ? Wenzake watatu wamebadilishwa wote wanamfunga, Mashabiki tunasuffer mara mia zaidi yake. Tumekuwa tukimuomba nini? Timu kushinda mechi moja tu derby roho zipoe. Si zaidi, Lakini hata hilo limekuwa taabu. Na cha kusikitisha zaidi, mashabiki wa Yanga wanafurahia, wanatembea kifua mbele, sisi tunabaki na midomo imekauka.

Hii klabu kubwa ya Simba imegeuzwa kichekesho. Yanga wanatumia mechi dhidi yetu kama njia ya points za bure, Yaani wakipoteza huko points 3, wanajisemea, “ahh tukienda kucheza na Simba tutapata pointi.” Hii ni aibu kubwa kwa timu yenye historia kubwa kama yetu.

Sasa sielewi viongozi wanasubiri nini? mashabiki wanajitoa, wawekezaji wanatia pesa, lakini matokeo bado ni fedheha tupu. Hivi kwanini tusichukue hatua mapema? hata huu msimu hauna dalili nzuri, Msimu unaendelea kuwa giza, na bado tunaambiwa “subirini, ni mchakato.” Huu mchakato unatuua polepole.

Huwezi kuachana na klabu yako, lakini kila siku unajisikia majuto. kilichobaki ni kukumbuka mafanikioya Simba iliyokuwa peak 2018 hadi 2022, maana kama ni kufika fainali shirikisho hata Yanga walishafika hakuna kipya.

Ni fedheha. Ni mateso. Na ukweli ni kwamba tupo kwenye wakati mgumusasa hivi, Lakini hatuwezi kuachana na Simba. Tueipenda wenyewe acha itutese.

Tumegeuzwa timu ya kusikitikiwa lakini hatutaki huruma, tunataka ushindi. Simba tunahitaji Reforms, tunahitaji sajili nzuri, uwajibikaji kwa viongozi, vinginvyo hawa Yanga watatubabua mpaka 2030
Kwa nini huwezi kuachana na klabu yako??
Mbona Diamond ameachana na Simba akajiunga Yanga?
Pia Ally Kiba ameachana na Coastal Union akajiunga Simba
 
Ushabiki wa timu sio kama sufuria ya kuipua maharage uchemshe njegere

Hata Yanga walifikia hatua ya kutembeza bakuli lakini mashabiki wa kweli hawakuhama
 
Ni wewe tu na ushamba wako na mahaba ya kijuha, watu wanahama dini itakuwa klabu ya mpira.
Simba sio baba yako wala mama yako useme eti huwezi kuihama.
 
Back
Top Bottom