GE2025 Mashabiki wa Simba wagoma kumshangilia Rais Samia akitoa salam katika tukio la Simba day

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,871
Reaction score
39,881
Suala la mashabiki wa Simba kuzomea wakati Rais akitoa salam katika tukio la Simba day

Watanzania wameamka hawapo hapa kupumbazwa, watu wanataka haki katika sura mbalimbali

Yaani tukio la leo limezidi hata maandano ambayo polisi huzuia Kwa nguvu kubwa, Sasa ni dhahiri ujumbe umefika kuwa Watanzania wanataka uongozi Bora, uwajibikaji, uwazi na haki

Mimi kama shabiki wa Yanga nawapongeza watani wamekomaa na wanataka siasa ijitenge na football

Eng Hersi Said siku yetu ya wananchi tutaiga Kwa mtani na sisi tutazomea mno, tunaomba hekima ikuongoze usilete mambo ya kupiga simu,

Mtakuja kumdhalilisha mtu wenu

Watanzania hatutaki

Your browser is not able to display this video.
 
Wakuu

Kama mnavyojua sherehe za Simba Day zinaendelea hapa kwa mkapa na ninafuatilia kwa ukaribu sana. Jambo moja nimeliona hapa baada ya Msemaji wa serikali Gerson Msigwa kumpigia Simu Rais Samia, na Msigwa akawatasha mashabiki wamshangilie Rais Samia lakini hali imekuwa tofauti mashabiki wa Simba wamekaa kimya sana kama wamemwagiwa maji ya baridi kali.

Je hii inamaanisha ndiyo amepoteza mvuto kwa watanzania?


Your browser is not able to display this video.
 
 
Hapana mkuu Mimi naona ni hatua nzuri kuelekea huko tunapotamani
Hata Rome haikujengwa siku 1
 
Hapana mkuu Mimi naona ni hatua nzuri kuelekea huko tunapotamani
Hata Rome haikujengwa siku 1
Hamna hatua hapo watanzania hakuna kitu kichwani ijumaa mengine yatajaa uwanjani kama kawaida na msigwa atamnadi mama kama kawaida na hata usipoitikia utajua mwenyewe wao hawajali kwani huyo msigwa amecha kukaliwa kimya Leo mbona msimu uliopita watu pia walikaa kimya mtanzania ni maiti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…