GE2025 Mashabiki wa Simba wagoma kumshangilia Rais Samia akitoa salam katika tukio la Simba day

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
 
Sasa usiende uwanjani kuangalia soccer kisa siasa?una -mute tu wakianza salamu zao halafu we unaangalia soccer,we unadhani hapo hakuna wafuasi wa CCM ,kila mtu ana itikadi zake zomea zomea zikiendelea hivi wataacha kuleta siasa uwanjani maana wataogopa aibu.
 
Yani ccm. Waone aibu kisa kuzomewa hivi we uko timamu kweli yaani wasione aibu kula mabilioni ya pesa waone aibu kuzomewa hao Kila siku watakuja tu uwanjani sababu simba na yanga sio Mali ya mwananchi aliye nje ya CCM
 
Unaelewa maana ya kukiwasha yaani unataka kudanganya umma mtanzania alikiwasha mwaka Gani halafu kwenye mambo ya taifa ukiingiza chama hufanikiwi kama wewe umeshaanza kuitaja chadema sahau kukuta mtu barabarani
 
Nchi zingine wanaajili akili kubwa ili ziongoze taasisi zao na zitunge sera,ndio maana zinapiga hatua kubwa katika maendeleo.

Sisi dunia ya tatu tunaajiri watu wanaoweza kujipendekeza kwa watawala aiseee tusahau kitu kinachoitwa maendeleo kwa sasa.

Ningekuwa Raisi yule Msigwa asingestahili hata kuwa afisa habari wangu maana hana analojua zaidi yakusifia.

Tukio la jana Msigwa anastahili lawama maana alilazimisha jambo aliloona tangu mwanzo kuwa watu haliwavutii.

Angekuwa na akili angesikiliza wakati MO anasifia utawala je kelele zilikuwa nyingi kama ambavyo akitaja maneno mengine.

Kwa upande wangu namsifu sana Aweso yule alisoma mazingira akaona kabsa asitoe boko.

Ila kiukweli wa mambo mimi ni mwanaCCM ila CCM haipendwi katika jamii na watu wengi huo ni ukweli mchungu.Wengine walichagua kuwa CCM maslahi kwasababu za kibiashara,siasa,uchawa n.k lakini moyoni haipo.

Sisi tunayoipenda kutoka moyoni ndio wenye uwezo wakusema ukweli tunaouona.

Mimi ni mwanaccm nilietamani Tundu Lissu awe mwenyekiti wa Chadema ili siasa zetu zibadilike japo sijawahi kuelewa kwanini Lissu aliwapa wenzie sababu ya kumkamata mapema kabsa.Yaani alikuwa kama anawaambia kabsa nikamateni nao wakamuelewa.

Sasa sijui ni bahati mbaya au makusudi,maana yule OMO wa zanzibar ana siasa kama za Lissu lakini yeye alitulia kwanza ili uchaguzi ufike ili aone nini kitaendelea.
 
Mkuu umeongea vizuri sana hasa hapo kwa Lissu hata mimi naona ni Mistake kubwa alifanya kutamka Maneno kama yale na huku akijua kabisa Mazingira ya Nchi zetu hizi za Kiafrika.

Naenda Mbali zaidi na Kuamini Kosa la Awali kabisa lilikuwa kuja na huo uamuzi wa NRNE kwa Kipindi hiki (Awamu ya huyu Mama). Wengi hawaoni hapa lakini ni Mistake Kubwa sana.

THE issue ni kwamba SLOGAN ilikuwa sahihi ila si katika wakati sahihi. Wenye Akili kubwa watakubaliana na Mimi hapa.
 
Lissu Yuko sahihi laZima tuupinge uchaguzi wa utapeli, hata kama watashinda na kijiweka madarani lakini Nina hakika watatawala Kwa shida mno na watajua Watanzania wapo aware na utapeli wao.
Hii ni hatua nzuri kupinga uchaguzi na naamini hatua kubwa na muhimu zaidi zinakuja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…