nyakubonga
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 7,088
- 12,837
kuna dada mmoja amenifurahisha hapo...Gerson Msigwa analazimisha watu wamuitikie Mama Samia kwenye Simba Day 2025 ila Raia zikakausha.. No unafiki
View attachment 3469244
Kuna muda huwa naona Lissu aliona akiwa nje kuhamasisha NRNE aliona hatafanikiwa.Mkuu umeongea vizuri sana hasa hapo kwa Lissu hata mimi naona ni Mistake kubwa alifanya kutamka Maneno kama yale na huku akijua kabisa Mazingira ya Nchi zetu hizi za Kiafrika.
Naenda Mbali zaidi na Kuamini Kosa la Awali kabisa lilikuwa kuja na huo uamuzi wa NRNE kwa Kipindi hiki (Awamu ya huyu Mama). Wengi hawaoni hapa lakini ni Mistake Kubwa sana.
THE issue ni kwamba SLOGAN ilikuwa sahihi ila si katika wakati sahihi. Wenye Akili kubwa watakubaliana na Mimi hapa.
Hatutaki siasaSuala la mashabiki wa Simba kuzomea wakati Rais akitoa salam katika tukio la Simba day
Watanzania wameamka hawapo hapa kupumbazwa, watu wanataka haki katika sura mbalimbali
Yaani tukio la leo limezidi hata maandano ambayo polisi huzuia Kwa nguvu kubwa, Sasa ni dhahiri ujumbe umefika kuwa Watanzania wanataka uongozi Bora, uwajibikaji, uwazi na haki
Mimi kama shabiki wa Yanga nawapongeza watani wamekomaa na wanataka siasa ijitenge na football
Eng Hersi Said siku yetu ya wananchi tutaiga Kwa mtani na sisi tutazomea mno, tunaomba hekima ikuongoze usilete mambo ya kupiga simu,
Mtakuja kumdhalilisha mtu wenu
Watanzania hatutaki
Kelele za kuzomea haziwezi kusikika. Azam wenyewe wameshaandaliwa. Kwanza zinaweza kuzimwa na mavuvuzela na zinaweza kusikika kama mnashangilia. Au wameandaa kukata matangazo iwapo kutaonekana viashiria vyovyote vya kuzomewa.Wananchi msiniangushe. Yeyote atakaye jitokeza kuwaletea siasa zao za maji taka za "mamaa! Mamaa!" kwenye tamasha lenu; mzomeeni! Awe ni Zuchu, Injinia Hersi, Msigwa, and CO. LTD! Wazomeeni mwanzo mwisho.
Hili wazo lako ni zuri mnoKelele za kuzomea haziwezi kusikika. Azam wenyewe wameshaandaliwa. Kwanza zinaweza kuzimwa na mavuvuzela na zinaweza kusikika kama mnashangilia. Au wameandaa kukata matangazo iwapo kutaonekana viashiria vyovyote vya kuzomewa.
Mngekubaliana kutoa ishara fulani ya mikono au hata kusimama na kugeuka upande wa pili kutowaangalia. Wenzetu wanatuzidi hapa, wanaweza kukaa kubuni njia za kuonyesha umoja wao na ujumbe ukafika.
Muda umeshakwenda mkuu. Ila kuna njia nyingi mtu unaweza kufanya kuvuruga mipango yao. Nyingine anahitajika mtu mmoja tu aliye na utayari, kama hiyo ya kuvaa tshirt yenye ujumbe tofauti halafu unakaa katikati yao. Mkijipanga watu 10 au zaidi ni bora zaidi maana mnaweza kutawanyika au mkakaa kwa vikundi, kila camera ikiwamulika mnaflash tshirt zenu.Hili wazo lako ni zuri mno
Nadhani ungeliandikia Uzi kabisa kila mtu aone kwamba ikifika wakati wa simu za Kizimkazi kila shabiki ageuke nyuma asitazame huo upumbavu
Nadhani Leo haitatumika simu labda anaweza kutoa hata ahadi kubwa.Muda umeshakwenda mkuu. Ila kuna njia nyingi mtu unaweza kufanya kuvuruga mipango yao. Nyingine anahitajika mtu mmoja tu aliye na utayari, kama hiyo ya kuvaa tshirt yenye ujumbe tofauti halafu unakaa katikati yao. Mkijipanga watu 10 au zaidi ni bora zaidi maana mnaweza kutawanyika au mkakaa kwa vikundi, kila camera ikiwamulika mnaflash tshirt zenu.
Halafu leo msitegemee tena simu ila zitatumika njia tofauti ili tu mpate kumshangilia.
Acha usenge wewe,Kama wamepangwa basi tarajia na WA yanga kupangwa pia ijumaa huwezi kutofautisha simba na yanga na ccm utakua umechelewa sana kitendo Cha kujaa uwanjani ni uthubitisho watanzania ni wajinga na wataendeshwa sana
Haitatumika simu. Ni kama Simba Day ile aliyokwenda uwanjani ila hakwenda kwenye siku ya Yanga.Nadhani Leo haitatumika simu labda anaweza kutoa hata ahadi kubwa.
Ila huyu mama watu wamemchoka aisee
Watu wanakosea sana kuweka focus kwa Samia. Shida haipo hapo. Hakuna jipya analofanya ambalo halikufanywa na wengine kabla yake.Nadhani Leo haitatumika simu labda anaweza kutoa hata ahadi kubwa.
Ila huyu mama watu wamemchoka aisee
Dogo wa Bahari Beach ,alitekwa Tegeta Kibo Complex pale pale alipotekwa Late Mohamed Kibao.ni yule mushi?