Huko nyuma nilidhani Mashabiki wa Simba SC wana uelewa mkubwa wa Masuala mazima ya Kimpira kuliko wale Mashabiki wa ‘ hovyo hovyo ‘ wa Yanga SC kumbe taratibu sasa naanza kuona hali ni tofauti na huenda wakawepo wengi kuliko vile nilivyokuwa nadhania.
Jana wakati mchezo kati ya Simba ya Tanzania ( Third World Country ) dhidi ya Sevilla ya Hispania ( First World Country ) ulioisha kwa Simba Kufungwa Goli / Mabao 5 kwa 4 nilishangaa mno n asana kuwaona Mashabiki ‘ Wapuuzi ‘ wa Simba jinsi Mishipa ya Shingo ilivyokuwa ikiwatoka kwa Kulaumu na Kukasirika kwanini tumefungwa wakati Sisi ndiyo tulikuwa tukiongoza Kipindi cha Kwanza.
Ninaposema kuwa kuna Mashabiki wa Simba uwezo Wao wa akili hasa wa Kuchambua Mpira ni sawa na wale tuliowazoea wa Yanga ambao ni mdogo mno au ni wa ‘ hovyo hovyo ‘ muwe mnanielewa tafadhalini kwani jana ndiyo nimethibitisha rasmi japo huko nyuma nilikuwa nikihisi tu pekee.
Hivi kweli kwa akili ya Kawaida tu kuna mwana Simba ambaye Kiukweli kabisa jana alijua kuwa Simba tungeshinda ile mechi? Hivi mnajua ya kwamba wakati Simba yetu ikichezesha Vikosi vyake viwili vipana na tukamaliza kabisa Wenzetu Sevilla waliwacheza Wachezaji wao wengi ambao hata huwa hawapati kabisa nafasi ikiwemo Yule Kipa japo baadae waliwaingiza Wachezaji Wao mahiri Watatu tu?
Nyie wana Simba wenye akili za ‘ hovyo hovyo ‘ kama za wana Yanga hivi mnatambua ‘ Thamani ‘ ya Klabu ya Sevilla, Uwekezaji wake na Mafanikio yake hasa katika Soka la Ulaya Bara ambalo kila Mwafrika kila Siku ‘ anaota ‘ kama si ‘ Kutamani ‘ pia kwenda Kuishi huko?
Je nyie wana Simba wenye akili za ‘ hovyo hovyo ‘ kama za wana Yanga hivi mmeshajiuliza tu ‘ Kiufundi ‘ ni kwanini jana Kipindi cha Kwanza Sevilla walikuwa wanapooza mpira lakini Kipindi cha pili wakabadilika na kupelekea Kutufunga yale Magoli yao mazuri na ya ‘ Kiutaalam ‘ kabisa ambayo nina uhakika kama muda ungeongezwa pale basi hata Wiki ( Goli / Mabao 7 ) pengine hata 10 ‘ tungeyakoga ‘ pale Kwa Mkapa / Taifa?
Yote Kenda / Tisa ila Kumi ambapo ndiyo nilichoka kabisa na kuona kuwa kumbe kuna uwezekano huku Simba kukawa na Mashabiki wa ‘ hovyo hovyo ‘ hata kuliko wale wanaopatikana kwa uwingi kule Yanga. Kitendo cha wana Simba ‘ Kukasirika ‘ kwanini Kocha Patrick Aussems alifanya ‘ Mabadiliko ‘ ndiyo kimenithibitishia kuwa kumbe Tanzania kuna Mashabiki wa Mpira tu na hakuna Wanamichezo.
Hivi ni nani asiyejua kuwa lengo Kuu la Kampuni ya Kubashiri Michezo ya Sports Pesa lilikuwa ni Kwanza kuileta tu Klabu ya Sevilla kwa dhumuni Kuu la Kiutalii nchini, Kujenga Uhusiano mwema na Klabu ya Simba lakini kubwa zaidi kuwapa Wachezaji wetu wa Simba ‘ exposure ‘ kubwa na pengine hata ‘ Kuwatamanisha ‘ na Wao Siku moja waende Kucheza huko Ulaya / Dunia ya Kwanza?
Alichokifanya Kocha wetu wa Simba Patrick Aussems jana ni kuhakikisha kuwa anampa kila Mchezaji nafasi ya Kucheza na pia kuweka rekodi katika Maisha yake kuwa aliwahi Kucheza na Klabu Bingwa ya Kihistoria ya Kombe la UEFA ya Sevilla Kitendo ambacho Mimi GENTAMYCINE namsifu / nampongeza sana Kocha wetu kwani lengo Kuu limetimia japo Watu wasiojua mpira kwa marefu na mapana yake Wao lengo lao Kuu ile jana ilikuwa ni Kuiona tu Simba ikishinda halafu waanze ‘ Kujisifu ‘ huku mtaani kuwa wana Timu bora ya kuweza ‘ Kupambana ‘ na hadi Klabu Kubwa na Bingwa za Ulaya jambo ambalo Kiuhalisia ni Kinyume kabisa na ukweli wenyewe uliopo.
Binafsi kama GENTAMYCINE na mwana Simba lialia / kindakindaki nina uhakika pamoja na Kufungwa kule jana na Sevilla ila najua tayari ‘ Scouts ‘ wengi wa Kihispania na hata wale wa nchi zingine ambao jana walikuwa wakiutizama ule Mchezo kwani ulitangazwa sana Mitandaoni na Dunia nzima basi kuna uwezekano mkubwa Klabu ya Simba ikauza Wachezaji wake wengi tu ambao jana walifanya vyema pale lakini hata kama wasipouza sasa ila kuna ‘ Fursa ‘ nyingi ambazo Klabu itaipata na hata Wachezaji Vijana wa Simba watakuja kuipata hapo baadae.
Acheni kuwa na Upeo wa kuona mambo ya karibu karibu na jifunze kuwa na Jicho la Tatu katika Masuala mazima ya Mpira. Nimesikitika sana kuwaona Mashabiki wa Simba ndiyo wana huu Upeo kwani ninavyojua wenye huu Upeo ni wale Mashabiki wa Yanga ambao kama kawaida yao jana Simba ilipofungwa walishangilia kabisa badala ya Wao kuona ‘ Wivu ‘ kwa Simba kupata Mafanikio kila Kukicha na Wao wakibaki tu Kulia njaa.
Nawasilisha.