Mashabiki wa timu za Ulaya waliopo Afrika wamepatikanaje?

Mmmmh...
Hili gumu sana chief..!
Ila wapo watakao husisha popularity ya wanamuziki wengi wa Merikani na nguvu za "freemasons"
Kama kutumia u freemason ni rahisi kiasi hicho. Basi ndugu zetu wa Kigoma wangeshatumia Kemia ya Kiafrika kuunda ndege za kwenda mabara mengine na zenye kubeba watu wengi zaidi.
 
mimi ni mtoto wa miaka ya tisini hivyo sijui sana, ila katika pita zangu humu jamiiforums nilipata kusoma mwanajamii mmoja akisimulia jinsi walivyokuwa wakisoma gazetini habari za kina beatles na timu za ulaya

kwa nionavyo asili ya mashabiki wa kiafrika wa mambo ya ulaya ulianza na magazeti

yani tangu enzi za ukoloni, magazeti na magazines ya ulaya, ya london, times ama marekani kama vile newsweek huko yaliletwa huku kusomwa na wazungu ama waafrika wasomi.

wazungu walitaka magazeti ya kwao ili wasome yanayoendelea kwao ulaya

matokeo yake waafrika wakawa nao ni wasomaji ya hayo magazeti,

humo magazetini kukawa na habari za mastaa na wanasiasa na wanamichezo wa ulaya wa enzi hizo

yamkini magazeti yalisifu na kupamba sana performance za wanamichezo wa ulaya

halafu kukawa na sinema ambapo moja ya vitu vilivyoangaliwa ilikuwa ni marudio ya recorded matches zilizochezwa huko ulaya, nayo waafrika wakajumuika kuangalia hapo ndio mashabiki walipoanza kupatikana na utamaduni huo ukaendelea kizazi hadi kizazi hadi leo hii ni mazoea yetu kupenda vya kizungu

kwahiyo chanzo cha mashabiki wa timu na miziki na bendi hata bendi za ulaya ni uwepo wa magazeti na magazines za ulaya hapa afrika miaka hiyo ya zamani, jumlisha na sinema, ambazo zilijaa content za wazungu tu
 

Ushabiki wa timu unaweza kuja na njia nyingi lakini mtazamo wangu ni kwamba ushindi wa mara kwa mara unachukua asilimia zaidi ya 70.

Issue zingine zinaweza kuwa:-
  • Kufata mchezaji unayemkubali, mfano ni jinsi ambavyo Ronaldo na Messi watu wanawafatilia.
  • Ushabiki kwa influence ya mtu, mfano unapokuwa na mzazi au mshikaji akawa anakusimulia ubora wa timu yake unapoanza ushabiki unajikuta umefata.
  • Kuwa tofauti na wengi, yaani kuchagua timu ambayo siyo ile inayopendwa na wengi au na mtu wako wa karibu ili tu kuleta upinzani.
  • First time impression: kwamba mara ya kwanza kuangalia unajikuta unaiangalia hiyo na inashinda.
  • Timu za maeneo unakoishi, mfano kuna wabongo waliosoma nje, na wanajikuta hizo timu zilikuwa mtaani (% ndogo).
  • N.k
All in all, kila mtu ana sababu ya kwa nini timu hii na si ile.
 
Duuuuh...
Inaonekana ndivyo ilivyokuwa chief...
Ila kwakweli Muzungu alituroga vibaya sana...
Ni rahisi kusikia Mtanganyika amejiua kwasababu ya matokeo mabovu ya Man Utd kuliko kusikia amefanya hivyo kwaajili ya YANGA au simba..!
Hata mimi huwa najisikia vibaya sana Man City ikifungwa kuliko Yanga ikifungwa..!
😆😆😆😇
 

Ligi ya Bongo tumeanza kuiona hivi karibuni, nadhani miaka 5 haijapita, na sababu kubwa tuliwahi kuambiwa ukionesha live watu hawataenda uwanjani.

EPL, UEFA, Seria A, nk tumekuwa tunaziangalia kuanzia miaka ya 1995, leo nikikutana na watu kama kina Lunyamila, Mohammed Mwameja, Mohammed Hussein Machinga, George Masatu nk siwajui. Lakini nikimwona Andy Cole, Cantona, Paul Ince najua huyu ni fulani.

Kwa hiyo automatically unakuta tu ushabiki wa timu hizo ni mkubwa.

Marketing, wenzetu wanafanya michezo kuwa biashara, kuna kuuza vifaa vya michezo, na mostly unawauzia washabiki wako, hivyo mbinu za kimasoko kuhakikisha una washabiki wa kutosha ni za lazima.
 
Daaah...
Umeamua kuufunga uzi wangu kabisa Chief..!
😂😂😂
Sidhani kama kuna sababu za kuanza kuishabikia timu tofauti na hizzi ulizozitaja Broh...
Sababu uliyoiweka katika bullet namba nne (4) ndio iliyofanya nianze kuishabikia Golden State Warriors,ilikuwa wanacheza na OKC,kipindi hicho Durant yupo OKC,msimu huo GSW walipoteza kwenye finals dhidi ya Cavaliers,ndio maana hadi leo namchukia Lebron vibaya sana..!
Bullet number tatu (3) ndio sababu iliyonifanya niishabikie Man City..!
 
Kwa nini hao watu wa Ulaya wasiwe kama watu Tanzania, kwa kuishabikia Simba/Yanga kwanza hata kama wanakutana na timu ya nyumbani(kwa mashabiki eg Lipuli) kwao?
 
Mimi nilianza kumshabikia Beckham yeye kama yeye kabla ya kuanza kuipenda Man United, nilikuwa napenda sana kumuangalia akicheza, nikajikuta taratibu nakuwa shabiki wa timu
 
Mimi nilianza kumshabikia Beckham yeye kama yeye kabla ya kuanza kuipenda Man United, nilikuwa napenda sana kumuangalia akicheza, nikajikuta taratibu nakuwa shabiki wa timu

Itakuwa ni kipindi kile anafuga nywele, miaka ya 1997-2001.
 
That Night at instabull huenda ndo ilifanya niipende Liverpool, enzi hizo 2005 nikiwa darasa La 4 , ile fainali nilienda kuangalia na baba( yeye ni man utd) nikatokea kumkubali Steven Gerrard kwa hiyo mpaka nakuakua nikawa naipenda liver, nakumbuka fainali ya 2007 enzi hizo niko darasa la sita niliwekeana sh 50 na rafiki yangu yeye alikua Ac Milan wa kutupwa sababu ya Ricardo kaka, daah nakumbuka sh 50 yangu ililiwa, soka nilianza kulijua kitambo sana sababu baba ,kaka walikua watu wa mpira
 
Mimi ni under mtu mzima
 
Katika miaka fulani ilikuwa kidogo kuna unafuu enzi za kina Pamba, Majimaji, Reli Moro, CDA, RTC Kigoma, Tukuyu, Milambo na zingine ilianza kuleta upinzani na team hizi mbili kubwa lakini tumeruudi zero tena. Ili tuendelee kikweli lazima tushabikie kwa nguvu team zetu tunakotoka. Napenda sana EPL watu wanapenda team zao hata za wilaya tu tena kwa nguvu. Juzi nilikuwa naangalia Charlton sijui wako Div 2 uko South London na ilikuwa Premier wakati fulani lakini watu wamejaa na wanashangilia team yao. Tukibadilika kwa hili basi na mpira utakuwa ila inakera kuona simba au Yanga wanaenda mikoani halafu watu wanaandamana kuzishangilia haiko sawa kabisa. sijui kama linawezekana lakini naomba siku nione haya na hizi team kubwa ndio zitapata adabu.
 
Full stop mkuu... umemaliza
 

Tulikuwa na timu ya kuunga unga kipindi kile, ila Crouch kutoanza pia ilitugharimu sana.

Gerrard alilalamika swala la jamaa kunyimwa muda wa kutosha.
 
washabiki wa ukweli ni wa arsenal na man u, hao wa timu nyingine ni bendera fuata upepo
Chief...
Swali ni jepesi sana..!
Hao mashabiki wa Arsenal na Man Utd wamepatikanaje..?
Pia unataka kutuaminisha kuwa mtu aliyeanza kuangalia mpira mwaka 2010 ataishabikia Arsenal..?
Ahahaaaah..!
Acha utani aisee...
 
Kwani wa Kagera amewezaje kushangilia simba na sio kagera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…