LICHADI
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 4,491
- 12,560
Moja kati ya mashabiki feki na waajabu kutokea ulimwenguni ni mashabiki wa Yanga, Wakati timu yao ikiwa kwenye kipindi kigumu cha kutembeza bakuli la michango ya kuendesha timu wao kama kawaida yao wameendelea kuonyesha ushabiki wa mdomoni na sio vitendo
Siku ya leo katika mchezo wa Yanga na Simba Sc ambapo katika mchezo huo Yanga ndio alikuwa mwenyeji, nilishangazwa na idadi kubwa ya mashabiki wa Simba waliojitokeza na huku wanayanga wakiwa wachache hadi kushindwa kujaza jukwaa lao
Na kilichonishangaza zaidi ni kitendo cha Simba Sc ambaye ni mgeni kujaza karibia asilimia 65 ya uwanja wote, wanasimba walijaza jukwaa lao lote na wengine wakaamia jukwaa la Yanga huku Yanga viti vyao asilimia kubwa vikiwa wazi kabisa
Ikumbukwe kuwa mapato yote ya leo ni ya Yanga sc, Na timu ili iweze kujiendesha haya ndio moja ya mapato ambayo yanaisaidia timu kujiendesha lakini wanayanga wamebakia kupiga mdomo tu mitaani lakini uwanjani wanakimbia na timu yao inakosa mapato hadi wanafikia hatua yakuomba kuchangiwa.
Mashabiki wa yanga mnatakiwa mbadilike kwani nyie ndio mnaoifanya timu yenu iendelee kuwa na hali ngumu, jifunzeni kwa mechi za simba jinsi mashabiki wanavyojitoa kwa moyo wote, angalieni timu za ulaya yani ikiwa ni mechi za nyumbani tena derby huwezi kuta hata siti moja inabaki na ticket huwa zinaisha kabisa ndio maana timu zao zina maendeleo.
Sent using Jamii Forums mobile app