Mashabiki wanne wa Simba wafungiwa

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imewafungia kwa miezi sita kuingia viwanjani kwenye michezo ya michuano yote ya TFF, mashabiki wanne walioonekana kupitia video kwenye mitandao ya kijamii wakimshambulia shabiki mmoja aliyekuwa amevaa jezi ya klabu ya Yanga katika mchezo tajwa hapo juu.

Kupitia taarifa yake kwa umma TPLB imewataja Mashabiki hao kuwa ni Hassan Khatibu, Hamza Dafa, Patrick Shelukindo na Shaban Anga ambao walifanya tukio hilo katika mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Ihefu FC uliomalizika kwa Simba kushinda 2-1.

Bodi imewataka mashabiki kujiepusha na vitendo vya vurugu na kupigana viwanjani ili kudumisha upendo na umoja michezoni.





 
Klabu ya Yanga SC imetozwa faini ya milion tano kwa Kosa la kuingia uwanjani kupitia mlango usio rasmi kwenye mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Yanga SC, Nov 5, 2023.

Simba SC nao wametozwa faini ya million moja kwa kosa la wachezaji wake kuchelewa kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kupelekea mchezo kuchelewa kuanza kwa dakika 4.

#sokaonlineupdates
 
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemfungia michezo mitatu (3) na faini ya shilingi 500,000 (Laki tano) Mchezaji wa Yanga SC, Khalid Aucho kwa kosa la kupiga kiwiko Mchezaji wa Coastal Union, Ibrahim Ajibu kwenye mchezo wa NBC Premier League uliozikutanisha Coastal Union na Yanga SC.

(Imeandikwa na @anoth_paul)

#UamuziwaKamati #NBCPremierLeague #TPLB
 
Hiyo waliyofanya washabiki wa Simba sio ya kufungiwa kuingia viwanjani. Hiyo ni Police case na inatakiwa wawe rumande saa hizi kenge Hao
Yaaah mkuu sio ustaarabu ....but nahisi nao wanajutia
 
Ujinga usio na kipimo kumpiga shabiki mungine eti Kwasababu ana mrengo tofauti na wewe hao hawana tofauti na wahalifu wengine .
Wakati sisi tuliwakaribisha kupiga soup
 
Nimefurahishwa sana na adhabu iliyotolewa kwa Kibu Dennis, Henock Inonga na Djugui Diarra kwa kushangilia maeneo yasiyowahusu.
Hii tabia inaweza kumsababishia mchezaji kutupiwa mawe, makopo ya maji, na kuumizwa kwa sababu tu ya upumbavu wake.

Ila pia sijafurahishwa na hiyo adhabu kwa mwamuzi Emmanuel Mwandembwa. Kwa sababu alijitahidi kuchezesha kwa kufuata sheria 17 za soka! Ukiondoa mapungufu madogo ya kumpa kadi ya njano mchezaji asiyehusika.

Na kama sababu ya kufungiwa kwake ilikuwa ni kutompa kadi nyekundu Aucho, kutokana na kitendo cha kitoto kilichofanywa na Ajibu, na kusababisha Aucho amsukume na kiwiko chake cha mkono! Bado nitaendelea kuamini hiyo Bodi ya Ligi ipo kwa ajili ya kuinufaisha timu fulani, huku Yanga ikiwa si sehemu ya hiyo timu.
 
Kiukweli Ile mechi inaonekana ushindi wa Yanga ulikuwa mwiba Kwa mamlaka
 
Izi simba na yanga bana ukiwapiga faini ya 5k au 5m ni ndogo sana wataendelea tu na ujinga wa kuingia uwanjani kupitia milango ambayo siyo sahihi dawa yao wapigwe hata faini ya 50m watanyooka
 

Aucho kafanya makosa,kwahiyo asiadhibiwe ? Mnapenda sana kuchukulia kila kitu mnaonewa ili kunufaisha timu flani,badilikeni basi bodi ya ligi ipo sahihi,hata kama Ajibu alifanya utoto lakini Aucho kama professional footballer hakustahili hizo reaction zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…