Mashabiki wavunja mageti uwanja wa Benjamin Mkapa

Mashabiki wavunja mageti uwanja wa Benjamin Mkapa

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Kwa mujibu wa Yahaya Mkazuzu wa Clouds Fm anadai kuwa mashabiki waliokuwa wamechoshwa na kukaa kwenye foleni huku utaratibu wa kuingia uwanjani ukiwa haupo vizuri, basi mashabiki wakavunja geti na kuingia uwanjani.

20230528_144039.jpg

Mvua kubwa inayoendelea hapo kwa mkapa, ikawafanya watu washindwe kuvumilia wakawazidi nguvu polisi na kuingia uwanjani.

Mliopo kwa mkapa hali ipoje njooni mtujuze.

====

UPDATE;
Kumetokea fujo na vurugu kubwa Uwanja wa Mkapa kwenye Mechi ya Mkondo wa Kwanza wa Fanaili kati ya Yanga Vs USM Alger, geti lavunjwa. Maelfu ya mashabiki waingia uwanjani.

Video: Bongo 5
 
Kwa mujibu wa Yahaya Mkazuzu wa Clouds Fm anadai kuwa mashabiki waliokuwa wamechoshwa na kukaa kwenye foleni huku utaratibu wa kuingia uwanjani ukiwa haupo vizuri, basi mashabiki wakavunja geti na kuingia uwanjani.

Mvua kubwa inayoendelea hapo kwa mkapa, ikawafanya watu washindwe kuvumilia wakawazidi nguvu polisi na kuingia uwanjani.

Mliopo kwa mkapa hali ipoje njooni mtujuze
Wacha yauane tu hayo makwasukwasu
 
Historia zinaendelea kuandikwa,
1. Yanga kucheza fainali Shirikisho kwa mara ya kwanza , no bahasha Makolo mpo?
2. Diarra kutoka Mali hadi kuifikisha Yanga fainali kwa best footwork na kuwanyima sifa mastraika wa timu pinzani , anadaka mishale, mabomu, makombora, risasi, Mawe, manati, kombeo hata mikuki ya Maasai🤪!
3 Nabi kufukuzwa ukocha huko machokoroni alikokuwa hadi kuwa profesa wa kusoma mchezo na kufanya super sub
4. Mayele kuletwa mbadala wa Makambo anapochemka au kuchoka hadi kuwa straika hatari zaidi Afrika kwasasa hata umchunge vipi kama hujaroga kama Simba , anakubutua tu
5. Taa za uwanjani Mkapa kuzimwa makusudi Kila Yanga inapocheza usiku na timu kubwa! Stupid beans!
6. Mashabiki Utopolo Lia Lia kuvunja mageti Mkapa na kuingia uwanjani Bure kabla ya fungulia mbwa! Kwani wametumia zana Gani? Magreda?
7. Yanga ... (Endeleza...)
 
Wakulaumiwa ni CAF officers na management nzima ya uwanja, haiwezekan unajua tiketi zimeisha bado unawaweka watu nje ya uwanja mpaka Sasa 5, sababu hasa n zipi?. Upuuzi tu
 
Back
Top Bottom