Mashairi ya oh baby (kuchi kuchi) by jodie


Asante TANMO.....
Naupenda huu mwimbo kama ninavyokupenda wewe....hujui tu.
 
Last edited by a moderator:
Baby......

ngoja tuugeuze huo wimbo sasa!! unaonaje baby uwe wewe...!! halafu mimi ndo nikudedketie huo wimbo as a man who has been chasing you for so long! achana na mawazo ya mzazi na mwanae tena bana!! now its a lover and loved one!
 
Last edited by a moderator:
Tehtehtehteh.... haya nidedketi basi


ngoja tuugeuze huo wimbo sasa!! unaonaje baby uwe wewe...!! halafu mimi ndo nikudedketie huo wimbo as a man who has been chasing you for so long! achana na mawazo ya mzazi na mwanae tena bana!! now its a lover and loved one!
 
Tehtehtehteh.... haya nidedketi basi

hahahaaa!! naubadilisha sasa rasmi huu wimbo!!

'' when i wekap wekap in the moniii, i see th pm of ram!! eeenhh..!!

imediately after opening, i see her smiling faaaaace... tiiiiliiii!! liii!!

duluuuluul... mamaaaa!! you are my sunshine RAMMmmm!!!

'' when i started to read it, i got 100 kisses from RAMMmm!!

mmmhhh...!!
 
Last edited by a moderator:
Reactions: ram
Yaani mie mtu akiniimbia huu wimbo nasinzia usingizi wa pono!!! thax @kobun
c.c TANMO

mapenzi tele
 
Last edited by a moderator:
Aiseee, thanks sana
Utanikuta huko huko

 
Last edited by a moderator:
Kama Joy Odiete maarufu kama Jodie akitua nchini leo, atashangaa mno kusikia wimbo wake wa mwaka 2011, Kuchi Kuchi (Oh Baby) ukichezwa kwenye mitaa ya mikoa karibu yote ya Tanzania.


Atakachoshangaa zaidi ni kwamba hata watu wa kijijini kabisa wanaufahamu wimbo wake na wengi wameuweka kwenye simu zao za mkononi kama muito wa simu ama kama wimbo wa kuwaburudisha wanapokuwa wamejituliza sehemu. Kama umesafiri na mabasi ya kwenda mikoani utakuwa umeiona video hiyo ikichezwa kwenye screen ndogo ya basi ulilosafiria.Kwa maeneo ya vijijini, hakuna pikipiki ya abiria (bodaboda) isiyoucheza wimbo huo kwenye redio ndogo zilizofungwa kwenye pikipiki hizo za kichina. Kwa sasa haiwezi kupita siku bila kuusikia wimbo huo ukichezwa kwenye kituo cha redio unachopenda kusikiliza.Hizo ndio sifa za hit single. Wimbo unaopata umaarufu na kupendwa na watu wa aina mbalimbali na tena bila kuzingatia umetoka zamani ama mpya. Pamoja na kuwa wimbo wa mwaka 2011, kwa masikio ya wengi, wimbo huo ndio kama umetoka jana.Kwa ufupi ni kuwa, wimbo wa Jodie ni mkubwa nchini Tanzania kuliko hata ukubwa wa jina lake mwenyewe. Nina uhakika, watu wengi hata hawamjui sura yake, labda tu kwa wale waliokwisha kuiona video.

Hata kwa Jodie, msichana aliyeshiriki mashindano ya Nigerian Idol na kuingia fainali japo hakushinda, Kuchi Kuchi ulikuwa ni wimbo uliomshangaza kwa jinsi ulivyokubalika na ilimchukua muda kiasi kuachia wimbo mpya.Katika mahojiano aliyofanya na gazeti la Daily Independent mwaka 2012, Jodie alisema baada ya Kuchi Kuchi wengi walikuwa na matarajio makubwa kutoka kwake. "Watu walianza kutarajia mengi kutoka kwangu, walianza kutarajia makubwa. Na sikuwaangusha. Baada ya hit kama ile, sikutakiwa kuja na album mbovu. Si tena kuhusu mimi, ni kuhusu maelfu ya watu waliovutiwa na nyimbo zangu na brand yangu.Fikiria kununua album sababu ya wimbo wa Kuchi Kuchi na unakuta ni Kuchi Kuchi pekee unaoeleweka na zingine zote sio nyimbo nzuri, lazima utakuangushwa."Baada ya Kuchi Kuchi, Jodie aliachia wimbo mwingine uitwao ‘Under the Mango Tree' ambao nao ulihit. Kwa mujibu wa Jodie, Kuchi Kuchi ni sauti na sio neno na ni wimbo maalum kwa mtoto japo hakuimba kwaajili ya mtoto wake kwakuwa hana mtoto bado. "Ni sauti inayoeleza upendo kati ya mama na mtoto."Jodie anasema pamoja na Kuchi Kuchi kumpa mafanikio makubwa ya kiuchumi, wimbo huo umemkuza kiakili pia.

 
Last edited by a moderator:
Hii nyimbo nilikuwa nikiusikia naupotezea sasa nikaanza kuwa curious na hii nyimbo baada ya kuona kila ukipigwa sehemu za starehe kila mtu anasimama.
Lakini binafsi nimelazimishwa kuusikiliza kwa makini kutokana na muitikio wa watu na media lakini si nyimbo iliyonistua siku ya kwanza kuusikia.

Alafu mabaamedi na hii nyimbo na wanavyoimba lazima mbavu ziume!!!!
 
Kuna mdada mchaga anasema huo wimbo ni wake,na hata sauti inayosikika ni yake pia.
 
Kuna mdada mchaga anasema huo wimbo ni wake,na hata sauti inayosikika ni yake pia.

Yap nilisikia akiongea kupitia Clouds FM,anasema aliurekodi sikunyingi Uganda akauacha Studio,alichofanya huyo dada ni kutoa video tu coz sauti siyo yake.Na baby aliyemaanisha yeye ni mwanaume,sio mtoto kama video inavyoonyesha,sijui kuna ukweli hapa au ni njia ya kupata kiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…