Mashamba ya kulima Ruvu

Mashamba ya kulima Ruvu

Twin_Kids

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
3,692
Reaction score
5,647
Habari zenu.

Nimewahi kuuliza swali kuhusu mashamba ya kulima Ruvu,nikabahatika kupata maelezo,nikaenda na nimeanza.

Lakini,uzi ulioniongoza nimeutafuta sijauona,ila nimetumia muongozo niliopewa.
Ruvu kwa kweli kama una nia ya kulima ni pazuri,maji yapo ya uhakika,mito ni miwili,Ruvu na Msuya.

Pamoja na hayo lakini kuna changamoto kubwa mbili:
1.Usimamizi unahitajika na kama umeamua,hamia au tafuta mtu wako wa karibu.Wajanja huku ni wengi,tena bora niwaite wahuni.Ukituma hela kwamba kazi utafanyiwa utaishia kulia tu.

2.Upatikanaji wa mashamba:
+255 658 899 195.Kuna mtu siku za nyuma alitoa hii number kwamba atafutwe mwenye nayo,atawapa maelezo.Hakika aliyepost hii number wanashilikiana asilimia mia.
Jamani,mtu kama yule unawezaje kuomba watu,walioacha familia zao,wampelekee pesa,awatapeli?

Nawasihi sana,nimeona mengi.
Kama unataka shamba huko,kuna sehemu mbili.Kuna kilimo cha mpunga,kinafanywa na shirika,huyu anawapeleka watu na kuwauzia mashamba ya watu,mwisho wa siku mnaishia kugombana na hela unapoteza.Anauza shamba lililopandwa mpunga kwa laki 5,na lisiti atakupa.Za kughusho,mwisho wa siku unakumbana na mwenye shamba sasa.

Kama umeamua kulima huko,nenda ofisini,gharama za ofisi ni 442,000(pesa ya kukodi shamba kwa mwaka,unalimiwa,unapewa maji,mbegu ya mpunga ni ya kwao unauziwa kiasi kidogo si kama madukani nje,mbolea ni za ruzuku,ukihitaji utapewa kwa gharama nafuu)Ukipita pembeni shauri yako.Labda uonane na mwenye shamba mtajuana wenyewe lakini kupitia mtu mwingine utalia.

Mashamba mengine unakodi kwa watu,na kama utakodi la hivo,hakikisha mnaandikishana kwenye uongozi wa kijiji.Tofauti na hapo,utajua mwenyewe.

Ukihitaji maelezo zaidi,nambie,kama kukusindikiza ntakusindikiza,ugjaramie usafiri.Ila,kama hujajipanga kulima,usiharibu hela yako.
 
Cjakuelewa cty hunter....mwenye hio namba ndo tapel?
 
Kilimo kinaanza mwezi wa ngapi poti?

Kwa sasa hivi wanaolima wameanza mwezi huu mwanzoni,na ni sehemu iliyoathilika kwa kujaa kwa mito,hivyo wanarudia,wengine wanavuna.Ila kwa anayehitaji kulima huko,tembelea ofisi yao kabla ya mwezi wa kumi ujue taratibu,iwapo utahitaji kukodi tu au kuwa mwanachama
 
Aksante
 
+255 713 467 930
Number hiyo ya mwenyekiti wa chama, CHAURU(Chama cha ushirika wa wakulima wa umwagiliaji-Ruvu), huyu atakupa maelezo yote,ukiridhia nenda ofisini,kama gharama kubwa,panga issue nyingine,sitopenda mwana jf ajikute anatapeliwa tena.Na ukiridhia,bora tafuta mtu wako mweke maeneo hayo,ukitafuta msimamizi ilimradi tu ulime,utayakumbuka haya
 
Namba moja apo kwenye usimamizi ukichukua vijana wa kazi pwani ndo zao .maneno mengi kazi hakuna.tafuta msukuma Mtoe kijijini uko mpatie unga kiasi.dagaa na maharage alafu mwambie malipo yake baada ya kipindi flani.wanapiga kazi sana
 
Cityhunter1, asante kwa taarifa hii njema.. ungeweka namba yako hapa kwa ajili ya consultation mkuu
 
Habari zenu.
Nimewahi kuuliza swali kuhusu mashamba ya kulima Ruvu,nikabahatika kupata maelezo,nikaenda na nimeanza.
Lakini,uzi ulioniongoza nimeutafuta sijauona,ila nimetumia muongozo niliopewa.
Ruvu kwa kweli kama una nia ya kulima ni pazuri,maji yapo ya uhakika,mito ni miwili,Ruvu na Msuya.
Pamoja na hayo lakini kuna changamoto kubwa mbili:
1.Usimamizi unahitajika na kama umeamua,hamia au tafuta mtu wako wa karibu.Wajanja huku ni wengi,tena bora niwaite wahuni.Ukituma hela kwamba kazi utafanyiwa utaishia kulia tu.
2.Upatikanaji wa mashamba:
+255 658 899 195.Kuna mtu siku za nyuma alitoa hii number kwamba atafutwe mwenye nayo,atawapa maelezo.Hakika aliyepost hii number wanashilikiana asilimia mia.
Jamani,mtu kama yule unawezaje kuomba watu,walioacha familia zao,wampelekee pesa,awatapeli?
Nawasihi sana,nimeona mengi.
Kama unataka shamba huko,kuna sehemu mbili.Kuna kilimo cha mpunga,kinafanywa na shirika,huyu anawapeleka watu na kuwauzia mashamba ya watu,mwisho wa siku mnaishia kugombana na hela unapoteza.Anauza shamba lililopandwa mpunga kwa laki 5,na lisiti atakupa.Za kughusho,mwisho wa siku unakumbana na mwenye shamba sasa.Kama umeamua kulima huko,nenda ofisini,gharama za ofisi ni 442,000(pesa ya kukodi shamba kwa mwaka,unalimiwa,unapewa maji,mbegu ya mpunga ni ya kwao unauziwa kiasi kidogo si kama madukani nje,mbolea ni za ruzuku,ukihitaji utapewa kwa gharama nafuu)Ukipita pembeni shauri yako.Labda uonane na mwenye shamba mtajuana wenyewe lakini kupitia mtu mwingine utalia.

Mashamba mengine unakodi kwa watu,na kama utakodi la hivo,hakikisha mnaandikishana kwenye uongozi wa kijiji.Tofauti na hapo,utajua mwenyewe.
Ukihitaji maelezo zaidi,nambie,kama kukusindikiza ntakusindikiza,ugjaramie usafiri.Ila,kama hujajipanga kulima,usiharibu hela yako.
Mkuu vipi gharama ya kutaka kununua kwa heka na taratibu zote zikoje huko
 
Mkuu vipi gharama ya kutaka kununua kwa heka na taratibu zote zikoje huko

Kwa kukusaidia labda niulizie,japo ukivuka mto Ruvu kati ya Ruvu sasa na mto unaitwa Msua nasikia zinaenda kati ya 1.2 na 1 Million,ila ukiwabamba msimu wa kilimo unaweza punguziwa.Kwa kulima kama umeamuwa ni pazuri sana. We kama uko tayari nikuunganishe na mtu nimesikia ana heka 50,ila hata wanaohitaji vipande anawakatia,japo sijamuuliza bei.
Taratibu si nyingine shirikisha uongozi wa kijiji,maana nadhani utakuwa na uhakika wa ardhi kuwa yako kihalali
 
Kwa kukusaidia labda niulizie,japo ukivuka mto Ruvu kati ya Ruvu sasa na mto unaitwa Msua nasikia zinaenda kati ya 1.2 na 1 Million,ila ukiwabamba msimu wa kilimo unaweza punguziwa.Kwa kulima kama umeamuwa ni pazuri sana. We kama uka tayari nikuunganishe na mtu nimesikia ana heka 50,ila hata wanaohitaji vipande anawakatia,japo sijamuuliza bei.
Taratibu si nyingine shirikisha uongozi wa kijiji,maana nadhani utakuwa na uhakika wa ardhi kuwa yako kihalali
Hii bei ni kwa Heka mkuu au ni kukodi
 
Hii bei ni kwa Heka mkuu au ni kukodi

Siyo kukodi mkuu,kukodi ni kati ya laki moja na laki na nusu kwa mwaka mzima;hatua za miguu 70*70 unanunua unaimiliki inakuwa ya kwako.Siyo story ya kuambiwa niliongea na mtu akiwa anatafuta mteja,bahati mbaya plan yangu ilikuwa kukodi haikuwa kununua.Lakini zipo ukihitaji utapata,maelewano yako na mwenye shamba
 
+255 713 467 930
Number hiyo ya mwenyekiti wa chama, CHAURU(Chama cha ushirika wa wakulima wa umwagiliaji-Ruvu), huyu atakupa maelezo yote,ukiridhia nenda ofisini,kama gharama kubwa,panga issue nyingine,sitopenda mwana jf ajikute anatapeliwa tena.Na ukiridhia,bora tafuta mtu wako mweke maeneo hayo,ukitafuta msimamizi ilimradi tu ulime,utayakumbuka haya
Tofauti na mpunga wanalima mazao ganiengine huko?
 
Back
Top Bottom