Habari zenu.
Nimewahi kuuliza swali kuhusu mashamba ya kulima Ruvu,nikabahatika kupata maelezo,nikaenda na nimeanza.
Lakini,uzi ulioniongoza nimeutafuta sijauona,ila nimetumia muongozo niliopewa.
Ruvu kwa kweli kama una nia ya kulima ni pazuri,maji yapo ya uhakika,mito ni miwili,Ruvu na Msuya.
Pamoja na hayo lakini kuna changamoto kubwa mbili:
1.Usimamizi unahitajika na kama umeamua,hamia au tafuta mtu wako wa karibu.Wajanja huku ni wengi,tena bora niwaite wahuni.Ukituma hela kwamba kazi utafanyiwa utaishia kulia tu.
2.Upatikanaji wa mashamba:
+255 658 899 195.Kuna mtu siku za nyuma alitoa hii number kwamba atafutwe mwenye nayo,atawapa maelezo.Hakika aliyepost hii number wanashilikiana asilimia mia.
Jamani,mtu kama yule unawezaje kuomba watu,walioacha familia zao,wampelekee pesa,awatapeli?
Nawasihi sana,nimeona mengi.
Kama unataka shamba huko,kuna sehemu mbili.Kuna kilimo cha mpunga,kinafanywa na shirika,huyu anawapeleka watu na kuwauzia mashamba ya watu,mwisho wa siku mnaishia kugombana na hela unapoteza.Anauza shamba lililopandwa mpunga kwa laki 5,na lisiti atakupa.Za kughusho,mwisho wa siku unakumbana na mwenye shamba sasa.
Kama umeamua kulima huko,nenda ofisini,gharama za ofisi ni 442,000(pesa ya kukodi shamba kwa mwaka,unalimiwa,unapewa maji,mbegu ya mpunga ni ya kwao unauziwa kiasi kidogo si kama madukani nje,mbolea ni za ruzuku,ukihitaji utapewa kwa gharama nafuu)Ukipita pembeni shauri yako.Labda uonane na mwenye shamba mtajuana wenyewe lakini kupitia mtu mwingine utalia.
Mashamba mengine unakodi kwa watu,na kama utakodi la hivo,hakikisha mnaandikishana kwenye uongozi wa kijiji.Tofauti na hapo,utajua mwenyewe.
Ukihitaji maelezo zaidi,nambie,kama kukusindikiza ntakusindikiza,ugjaramie usafiri.Ila,kama hujajipanga kulima,usiharibu hela yako.