Mashambulizi dhidi ya Magufuli: Michezo au upepo wa kisiasa?

Mashambulizi dhidi ya Magufuli: Michezo au upepo wa kisiasa?

CCM wana watu wamesomea siasa mkuu.
Wameamua kuanzisha hiyo ligi maksudi ili wanasiasa wa vyama vingine wasiendelee na mambo yao ya siasa wawasikilize CCM kwamba wana mgogoro.
Na wamefanikiwa 100%
 
Katiba imetoa haki ya kuishi, ndiyo maana wale kina jebra walivyoenda mahakamani kuhoji adhabu ya kunyongwa walitumia Katiba na Penal code,na mikataba ya kimataifa inayotoa haki ya kuishi, Penal code inasema mtu akikutwa na hatia ya kosa la kuua kwa kukusudia atanyongwa, wakati Katiba inatoa haki ya kuishi hence mkanganyiko
Nini maana ya maisha?
 
Nini maana ya maisha?
Hujui maana ya maisha kumbe? Simu yako Ina Google hebu jaribu kugoogle, usipoteze muda Kasome Katiba uielewe,kasome na Penal code uelewe acha kapoteza muda,sheria hujui, Katiba hujui
 
Niliwahi kusikia wakwer(l?)e wanatajwa sana. Magufuli alikuwa msukuma!!?
Wakwele walitajwa tu kwakua Rais alikua madarakani na lazma angejulikana kinaga ubaga Ila jakaya hakupata kufanya upendeleo huoo kwa wakwele wenzie yeye alithamini Sana watu aliochanga nao karata awe mpare mkindo mmatumbi aliwanufaisha na hoahao walitunufaisha sisi wenzi wao kwa hiyo wote tulipata tofauti aliochofanya jiwe alisahau ata waliomchangia karata nini kuchanga nao ......piaJk wala hakua mfedheheshaji Kama jiwe ufedheheshaji ni moja Kati ya ukatili mkubwa sana akifanyiwa mtu mzima.
 
Watetezi wa mungu mtu, dikteta, mnyanganyi asietaka kushaurika mwisho wa sku ubishi wake ukaondoka nae
mungu mtu wa hovyo kuwai kutokea ktk historia ya Tanzania

Rai yangu kwa Roman Catholic wasije mfanya mtakakifu km wanavyotaka mfanya Baba wa mataifa
 
Hakuna atakayemkashfu JPM na akabaki salama.
Kwa sababu wote tupo hapa hapa Tanzania, tutaona kwa macho yetu.
Maana Mungu huwa hadhihakiwi.
 
Ninajiuliza:

• Ni kwamba mama ameona hajafanya chochote ndani ya mwaka wake mmoja as compared na mwaka mmoja wa Magufuli; hivyo akaamua ku-divert attention ya watu kutoka kujadili upungufu wake hadi kumtetea na kumshambulia Magufuli?

• Ni wazi hakuna Waziri ambaye hapendwi tangu tupate uhuru kama January. Je, Zitto (swahiba na mpigaji mwenzie) na wenzao wameona wabadilishe mjadala kutoka kujadili uzembe unaoendelea Wizarani hadi kumshambulia Magufuli knowing Wananchi wata-concentrate zaidi kumtetea Magufuli kuliko kuwashambulia wao?

• Kama ni report ya CAG; mbona mwaka jana, ambapo awamu ya tano ilikuwa inahusika 100%, mashambulizi hayakuwa ya level ya uongozi wa juu kama mwaka huu ambapo pia serikali ya awamu ya sita inahusika kwa zaidi ya 30%?

• Sote tunajua wanaojiita watoto wa mjini siyo smart sana kama wanavyojidhania; au ni upepo tu umewapitia na hivyo bahati ipo upande wao?

Vyovyote iwavyo, wanastahili pongezi. Wamefanikiwa kutuhamisha kwenye mijadala yenye masilahi ya nchi kuanzia uendeshaji hovyo wa wizara ya Nishati na Madini, matumizi mabaya ya rasilimali kwa waziri kwenye suala la anuani za makazi, mpaka ziara ya mkuu nje ya nchi kwa zaidi ya week sasa, and still counting.

Mpaka sasa Sukuma Gang 0 - 3 Msoga Gang

Hongera zao sana. 😁

Muwe na Alhamisi njema.
Mama anafufua uchumi na kukaribisha uwekezaji unasema hajafanya kitu??!
 
Hujui maana ya maisha kumbe? Simu yako Ina Google hebu jaribu kugoogle, usipoteze muda Kasome Katiba uielewe,kasome na Penal code uelewe acha kapoteza muda,sheria hujui, Katiba hujui
Wewe unayejua tujuze.
 
Wakwele walitajwa tu kwakua Rais alikua madarakani na lazma angejulikana kinaga ubaga Ila jakaya hakupata kufanya upendeleo huoo kwa wakwele wenzie yeye alithamini Sana watu aliochanga nao karata awe mpare mkindo mmatumbi aliwanufaisha na hoahao walitunufaisha sisi wenzi wao kwa hiyo wote tulipata tofauti aliochofanya jiwe alisahau ata waliomchangia karata nini kuchanga nao ......piaJk wala hakua mfedheheshaji Kama jiwe ufedheheshaji ni moja Kati ya ukatili mkubwa sana akifanyiwa mtu mzima.
Tuna hasara kubwa sana kuwa na Watanzania kama wewe.

Kwa taarifa yako na wajinga (siyo tusi) wenzio, Magufuli siyo msukuma.
 
Watetezi wa mungu mtu, dikteta, mnyanganyi asietaka kushaurika mwisho wa sku ubishi wake ukaondoka nae
mungu mtu wa hovyo kuwai kutokea ktk historia ya Tanzania

Rai yangu kwa Roman Catholic wasije mfanya mtakakifu km wanavyotaka mfanya Baba wa mataifa
Magufuli alikufa katika hali ya neema ya utakaso, alipokea sakramenti zote kabla ya kifo chake; Wakatoliki hatuna wasiwasi yupo mbinguni. Na mchakato wa kumsimika rasmi mtakatifu upo underway.
 
Mama anafufua uchumi na kukaribisha uwekezaji unasema hajafanya kitu??!
Kwa mujibu wa data za World Bank; amekuta tupo uchumi wa kati, ameturudisha uchumi wa chini. Hakika definition yako ya kukuza uchumi inastaajabisha.
 
Wakenya wana katiba mbovu?
Baadhi ya watanzania wa kupuuza. Pamoja na mapungufu hapa na pale, katiba ya Kenya ya kupigiwa mfano- hasa kuhusu madaraka ya rais, mgawanyo wa madaraka pembe tatu za serikali, ugatuzu/serikali ya majimbo.
 
Tuna hasara kubwa sana kuwa na Watanzania kama wewe.

Kwa taarifa yako na wajinga (siyo tusi) wenzio, Magufuli siyo msukuma.
Mimi nakubali mjinga maana tushaambiwa elimu haina mwisho kwa hiyo hata wewe ni mjinga pia.....Ila jifunze nidhamu maana Ukienda kumwambia babako mjinga halafu ukamuaminisha sio tusi hata kuelewa...tulio wengi tunajua yeye ni msukuma Kama anakabila lake ndani ya huko usukumani kwake anajua yeye kama tulivyojua mwinyi ni mzanzibar na mwanae Leo ni Rais wa Zanzibar suala la yeye ni mzaramo tumeskia Kama tulivyosikia magufuli ni msukuma.....kandamizo langu juu yule bwana nielewe kuwa alikua mkabila na aliekosa utu.
 
Mama anamalizia miradi iliyoachwa na mtangulizi wake ambaye aliiacha ikiwa chini ya asilimia 10 kiuendelezo,unaposema eti ndani ya mwaka mmoja ajafanya kitu ni KICHEKESHO,kumbuka miradi ni MINGI na nimiradi mikubwa yenye uhitaji wa fedha nyingi sana,mlitaka aiache aanzishe mipya?, kumbukeni baadhi ya miradi iliyoachwa baadhi imekamilishwa na mingi imefikia katika hatua nzuri sana kwa kuifikisha juu ya asilimia 50%.
MNAPOSEMA HAJAFANYA KITU MNATUSHANGAZA SANA WENYE AKILI TIMAMU.
Ndio machozi hayo yanakutoka.

Kweli una huruma kali
 
Na huu uzi unakaribia kuunganishwa na uleeee

Kudos Jamiiforums
 
Back
Top Bottom