Mashambulizi Mazito ya Mizinga ya Saudia Yaripotiwa huko Saada, Kaskazini Magharibi mwa Yemen

Watakipata wanachokitafuta.

Yemen walishaapa, kwa namna yoyote Saudi Arabia ikiivamia au kuzuia mashambulizi yao wanayoyafanya kuzuia meli zinazoelekea Israel watarudisha mapigo!

Nipo pamoja na Yemen.
Unavyo andika mtu anaweza kufikiri wewe ni bonge la gaidiii, kumbe bonge la mshamba mwenyeji wa sitimbi ndani ndani huko,ambaye akisikia mngurumo wa gari anakimbilia ndani kwa kasi ya mwanga,ila akishika kiswaswadu na kuandika sasaaa........!!!!???
 
Hawa vijana wakisha jiona wametoka nje ya Tanzania wanatuona watanganyika wote kama tunacheza.

Huyu kijana hata CCM hawawezi kumuunga mkono.
Mpuuzi mmoja huwa anaandika makorokocho sana!

Stress zao wanatuletea sisi!

Wao wanadhani kila mtu ana shida kama mazingira waliyokulia wao!
 
Unavyo andika mtu anaweza kufikiri wewe ni bonge la gaidiii, kumbe bonge la mshamba mwenyeji wa sitimbi ndani ndani huko,ambaye akisikia mngurumo wa gari anakimbilia ndani kwa kasi ya mwanga,ila akishika kiswaswadu na kuandika sasaaa........!!!!???
Nimezaliwa Dar na nimekulia Dar ila...

Sitimbi sipajui na sijawahi kufika. Ni wapi kwanza? Huwa napasikia tu!

Gongo la Mboto sijawahi kufika na sipajui napasikia tu!

Mbagala sijui Mbagara nilifika siku moja tu tangu nizaliwe kumsindikiza jirani kwenda kuoa na sijawahi kufika mpaka sasa hivi!

Vingunguti Alhamdulillah nilifika juzi! n.k

Enhee! Nitoe ushamba huko sitimbi ni wapi?

Hahahah!

Halafu ulivyosema kiswaswadu umenikumbusha 2009 nasoma mama alinipatia simu ya Nokia. Nikaikataa!

2009 nikataka ninunuliwe LG ya touch nikaona haya mzee akaninunulia Nokia na brother wangu akanipa ipod.
------------------
Unataka tuendelee tena? Au unataka tujadili mada husika/Uzi?
 
Hakuna taifa la Kiislam lenye linaweza kurusha makombora Saudia, wana amini Saudia ni taifa takatifu kwao. Hata Iran akitaka kuipiga Saudia, atapiga visima vya mafuta nk, hawezi kupiga mji wowote
Kumbe hujui kitu wewe saudia sio taifa takatifu taifa miji mitakatifu ni makka na madina tu, huo ufalme wenyewe uliingia madarakni kwa kuipindua ufalme wa wakati huo saudia inaitwa hijaz
 
Kwani inakuwaje wapigane wao kwa wao maana kama wamelogwa kweli ubinadamu kazi pigeni marekani ndiyo kirusi cha dunia. Maana kila vita naye yupo.
 
Ripoti za awali zinaonyesha mashambulizi makali ya mizinga ya Saudia yakilenga Saada, eneo linalodhibitiwa na Ansar Allah kaskazini magharibi mwa Yemen.

Sambamba na hilo, ripoti zinaonyesha Baraza la Mpito la Kusini mwa UAE (STC) linaloungwa mkono na UAE limeanzisha mashambulizi ya kushtukiza katika eneo la kusini mwa Taiz. Mapigano makali yameripotiwa huko al-Janad, kusini magharibi mwa Yemen, na kuzidisha hali ambayo tayari ni tete nchini humo.

View: https://x.com/DD_Geopolitics/status/1871320123811979398?t=dmKAXGGJiBxJ7Q17hpdY2A&s=09

Hii habari haionekani popote
 
Hii habari mbona haipo kwenye vyombo vya habari kama BBC, CNN, Al Jazeera nk?
 
Mimi nilisha waeleza Saud Arabua na UAE lazima watamsaidia US na Israel. Viongozi wa kiarabu ndio madui wa nchi za kiarabu.

Lakini mpaa mda hu sidhani Saud Arabia ataingia vita na Al Houthi anawajua hao ni balaa. UAE anaweza lakini akisha tandikwa Missiles 6 tu, atainua bendera.
 
Watakipata wanachokitafuta.

Yemen walishaapa, kwa namna yoyote Saudi Arabia ikiivamia au kuzuia mashambulizi yao wanayoyafanya kuzuia meli zinazoelekea Israel watarudisha mapigo!

Nipo pamoja na Yemen.
Makundi hayo ya kigaidi , yanachukiwa na mataifa yote ya Kiarabu kwa sababu yanadhoofisha Serikali za mataifa yao. Na hicho ndicho chanzo cha Iran kuchukiwa karibia na mataifa yote ya Mashariki ya kati.

Kwa sababu sasa mataifa haya yamejiridhisha kuwa Israel imefanya kazi kubwa ya kuyadhoofisha makundi haya, haya mataifa ya Madhariki ya kati lazima yatainuka na kuhakikisha haya makundi yote ya kigaidi ya Iran, yanapotea ili Serikali na wananchi wao waishi kwa amani.

Haya makundi yakipotea, Iran haitaleta chokochoko kwa Taifa lolote.

Uwezo wa Israel wa kupambana na makundi haya ya kigaidi umekuwa ndiyo sababu kubwa ya Israel kuungwa mkono na mataifa karibia yote ya kiarabu. Hiyo ndiyo sababu ya Israel kutoshutumiwa na mataifa haya yote inapoyatwanga haya makundi ya kigaidi.
 
Kwani inakuwaje wapigane wao kwa wao maana kama wamelogwa kweli ubinadamu kazi pigeni marekani ndiyo kirusi cha dunia. Maana kila vita naye yupo.
US ndie kiranja wa dunia lazima awepo kila pahala kutoa dozi na miongozo,magaidi na dini yao ya kishenzi ndio ttzo.
 
Kumbe hujui kitu wewe saudia sio taifa takatifu taifa miji mitakatifu ni makka na madina tu, huo ufalme wenyewe uliingia madarakni kwa kuipindua ufalme wa wakati huo saudia inaitwa hijaz
Umesoma ukiwa tayari umejipanga kwa ubishi. Nani kasema Saudia haipinduliki? Iran anaichukia Saudia hadi leo, akitaka kuipiga huaga hajaribu kupiga miji, anapigaga visima vya mafuta tu. Anyway, kuhusu miji "mitakatifu" ya Saudia, I know better than you think, nimewahi kuandika humu kwamba, nimefanya kazi Saudia kwenye kampuni moja kubwa la kimataifa, hiyo miji uliitaja kuna baadhi ya mitaa kama wewe sio Muislamu huruhusiwi kwenda kabisa. Tupo hapa, sio Houth wala Iran mwenye anaweza kuupiga mji wowote wa Saudia. Muda utaongea
 
Watakipata wanachokitafuta.

Yemen walishaapa, kwa namna yoyote Saudi Arabia ikiivamia au kuzuia mashambulizi yao wanayoyafanya kuzuia meli zinazoelekea Israel watarudisha mapigo!

Nipo pamoja na Yemen.
Huu ndio mwisho wa Houth kutawala Yemen Usifikir kwamba Saudia Yuko peke yake, huo ni mpango wa US, Israel na nchi za MAGHARIBI wakishindwa kumuondoa Houth mara hii basi wasahau daima.
 
Ripoti za awali zinaonyesha mashambulizi makali ya mizinga ya Saudia yakilenga Saada, eneo linalodhibitiwa na Ansar Allah kaskazini magharibi mwa Yemen.

Sambamba na hilo, ripoti zinaonyesha Baraza la Mpito la Kusini mwa UAE (STC) linaloungwa mkono na UAE limeanzisha mashambulizi ya kushtukiza katika eneo la kusini mwa Taiz. Mapigano makali yameripotiwa huko al-Janad, kusini magharibi mwa Yemen, na kuzidisha hali ambayo tayari ni tete nchini humo.

View: https://x.com/DD_Geopolitics/status/1871320123811979398?t=dmKAXGGJiBxJ7Q17hpdY2A&s=09

Saudia walishashindwa kuwang'oa wahouthi madarakani hapo awali......vipi waweze sasa?

Inashangaza namna mteja wa mabilioni ya silaha za kisiasa kutoka Marekani kashindwa kuwadhibiti wahouthi.

T14 Armata
 
Mimi nilisha waeleza Saud Arabua na UAE lazima watamsaidia US na Israel. Viongozi wa kiarabu ndio madui wa nchi za kiarabu.

Lakini mpaa mda hu sidhani Saud Arabia ataingia vita na Al Houthi anawajua hao ni balaa. UAE anaweza lakini akisha tandikwa Missiles 6 tu, atainua bendera.
Waarabu haqana akili.
 
Back
Top Bottom