Kwenye nchi nyingi kuelekea kipindi cha uchaguzi, siku ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi kuna mambo mengi hutokea. Mojawapo ya mambo hayo ni mashambulizi/udukuzi ya mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano na hata database mbalimbali au vitu vingine vinavyohusiana na hivyo.
Mfano kwenye uchaguzi wa Tanzania wa 2015 simu za mkononi za baadhi ya viongozi wa chama cha chadema zilidukuliwa na hivyo walishindwa kufanya mawasiliano kwa muda fulani.
Jamiiforums nayo ilipata mashambulizi ya kimtandao ambapo watumiaji wake tulishindwa kupata huduma ambazo tumezoea kuzipata.
Je, kwa mwaka huu vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi vimechukua tahadhari gani juu ya uvamizi wa kimtandao?
Je, JamiiForums mmejiandaa tayari? maana huenda yaliyotokea mwaka 2015 yakajirudia tena mwaka huu.
Je, mwanaJF mwenzangu umejiandaa? maana huenda siku kadhaa kabla ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi kunaweza kutokea udukuzi/mashambulizi/kuathirika kwa mtandao wa internet na mifumo kadhaa ya mawasiliano na hivyo hii inaweza athiri mawasiliano na utendaji kazi wa kila siku.
Je, mitandao ya simu/makampuni ya huduma za internet na mamlaka za serikali mf TCRA zimejiandaa?
Je, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imejiandaa dhidi ya mashambulizi/udukuzi ambayo yanaweza ikumba mifumo yake siku za uchaguzi?