Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mtaalamu wa uzalishaji na biashara za mafuta na gesi wa Abudhabi bw Said Albakr amebainisha kuwa iwapo nchi za Ulaya zitaendelea kujizuia kununua gesi ya Urusi basi wasitarajie kupata mbadala kutoka nchi za mashariki ya kati na kokote kwengine duniani katika kipindi cha miaka ya karibuni ijayo.
Katika uchambuzi wake huo mtaalamu huyo amebainisha sababu kadhaa zitakazopelekea hali hiyo.Alisema ni kweli nchi za mashariki ya kati ni wazalishaji wa zaidi ya nusu ya nishati itumikayo duniani ikiwemo gesi lakini kwa sasa nchi hazina uwezo wa kufidia pengo litakalotokana na kukatika kwa gesi ya Urusi katika nchi za Ulaya.
Sababu kubwa kati ya hizo aliitaja ni kukosekana kwa miundombinu ya kuzalisha na kusafirisha kiwango kitakachohitajika kwa mataifa hayo.Nchi hizo ili ziweze kufidia gesi ya kutoka Urusi kwa kipindi kifupi kijacho itabidi wakatishe mikataba ya kuyauzia mataifa ya Mashariki ya mbali ikiwemo China jambo alilosema litazigharimu nchi za mashariki ya kati kwa kukatisha mikataba na kuhatarisha biashara zao hapo baadae.
Ukiondoa Saudi Arabia ambayo imekataa tu lakini Zipo nchi 4 zingeweza kufidia gesi hiyo lakini tatu kati ya hizo kutokana na vikwazo vya muda mrefu walivyowekewa na nchi hizo za Ulaya kwa kushirikiana na Marekani hazina uwezo wa kuzalisha gesi hiyo.Nchi hizo tatu ni Venezuela,Iraq na Libya.Kwa upande wa Iran ina gesi nyingi iliyokwisha kujazwa kwenye meli zilizoelea baharini,lakini ni lazima mataifa hayo yaiondoshee vikwazo vya kiuchumi ili iweze kuwauzia.
Kikwazo kingine alichokitaja mtaalamu huyo ni kuwepo kwa makundi yanayopingana katika nchi hizo ambayo yamechipuka kutokana na mizozo iliyopandikizwa na mataifa hayo ya Ulaya na Marekani.Alitolea mfano wa nchi ya Libya kwamba visima vya mafuta na gesi havina usalama wa kutegemewa kuzalisha na kusafirisha chochote kutokana na kila eneo kudhibitiwa na makundi yanayopingana.