Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kenya ameingia mkenge, hakujua janja ya China. Hata mradi wa kujenga Bagamoyo port kama tungeukubali bila marekebisho ndio ungekuwa mbaya sana kama utumwa mamboleo. Na sisi tukiendekeza misifa ya kujenga miradi mikubwa bila uchambuzi yakinifu na baadae kukwama kifedha na kuja kutegemea China, kuna uwezekano wa kushindwa kulipa.Mkuu
Hakuna nafuu yeyote...lazima waje kubakwa on the day light
Waulize Kenya na Sri Lanka,wananyang'anywa bandari zao na tako wanatoa
Hua nawashangaa sana CCM kushangilia oppressors,wote ni oppressors tu,eti CHina this,China that..etc
Kenya ameingia mkenge,hakujua janja ya China.
Hata mradi wa kujenga Bagamoyo port kama tungeukubali bila marekebisho ndio ungekuwa mbaya sana kama utumwa mamboleo.
Nasisi tukiendekeza misifa ya kujenga miradi mikubwa bila uchambuzi yakinifu na baadae kukwama kifedha na kuja kutegemea China ,kuna uwezekano wa kushindwa kulipa.
China ya sasa siyo China ya Mao na rafiki yake Nyerere.
Kumbuka siku hizo China ilikuwa imetengwa na dunia,ikatumia urafiki wake na Tanzania ya Nyerere kujitangaza kwa kutupa misaada mikubwa ya Mawasiliano,Uchukuzi, Kijeshi,viwanda,Afya,Utamaduni,Elimu,Kilimo n.k
China ya sasa ipo kileleni kiuchumi kwa kutumia njia hizo hizo za mabeberu tena kwa ujanja zaidi.
Labda Raisi Magufuli ana jibu kama alivyogunduwa udhahifu kwenye mradi wa Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, uliokuwa ukisifiwa na kupigiwa upatu na Spika Ndugai.
Masharti nafuu ni kutokuhoji demokrasia na Utawala bora. Masharti magumu ni kuhoji mambo ya demokrasia na Utawala bora.Tumeambiwa ana masharti nafuu kuliko marekani je unayajua masharti nafuu ya china
Usharti nafuu wa Kichina ninaoujua na ambao nimejaribu Kuufuatilia ni Kukujengea haraka nchi yako, ila Wao Kuchukua Rasilimali zako Miaka 100.Wakuu habari:
Mara kwa Mara viongozi wetu wamekuwa wakituambia tumepata mkopo kutoka China wenye masharti nafuu.
Swali langu ambalo natamani kila mtanzania ajiongeze na aweze kufikiria nje ya box je mkopo wa masharti nafuu ukoje je masharti nafuu ni yapi?
Mara nyingi tumesikia kauli kuwa hatutaki mikopo ya mataifa ya kibepari yenye masharti magumu je ugumu wa masharti yao unakuja vp?
Je urahis upi huo tunaoupata kutoka China?
Je marekani ikitaka kukupa mkopo huwa inazingatia vigezo gani kukupa mkopo?
Nawasilisha
falcon mombasa
Nasikia Wachina wanamazingaombwe unashtukia unaweka signature bila kutaka,baadae unagundua wametutapeli,ndio malimwengu.Mfumo wa BOOT unatumika sehemu nyingi duniani ambapo mwekezaji anajenga na kumiliki kwa muda mpaka atakaporudisha gharama zake. Cha msingi ni kuangalia Maslahi ya kila upande yaani kila mmoja ashinde.
Kwa upande wetu ni kuwa labda hatuna watu mahiri wa kufanya majadiliano na mikataba. Wawekezaji mara nyingi wanataka kupata faida kubwa.
Hakuna mtu mbaya kama mchina linapokuja suala la mahusiano ya kiuchumi.China ni marafiki zetu wa enzi na enzi na kwa sasa wanajitanua zaidi duniani na wanaoushawishi mkubwa kuliko USA. Hawanaga kazi mbovu
Mkuu usijitutumue Sana kwa mambo yaliyokuzidi uwezo kufikiri.siyo kila jambo unaweka ushabiki wa kijinga.China ya leo haina urafiki na yeyote zaidi ya kujitanua kiuchumi.China ni marafiki zetu wa enzi na enzi na kwa sasa wanajitanua zaidi duniani na wanaoushawishi mkubwa kuliko USA. Hawanaga kazi mbovu