Masharti ya kuwekeza Zanzibar kwa Mtanzania bara na mgeni

Tuliwaambia zamani Sasa hata bado endeleeni Tu kulinda Uvamizi uitwao muungano
 
CCM inajuwa fika kama muungano ukivunjika na CCM pia inavunjika[emoji848]
 

Vipi hili jeshi lenu mlilolileta lililojaa kila kipembe Na usalama mliowamwaga kila street mtawaondosha lini ??
 
Anazungumzia nchi gani? Tanzania bara ndio ipo wapi hiyo?
 
Vipi hili jeshi lenu mlilolileta lililojaa kila kipembe Na usalama mliowamwaga kila street mtawaondosha lini ??

unafikiri muungani ukivunjwa hilo jeshi hapo litafanya nini zaidi ya kurudi kwenye mipaka ya bara....lipo kwa sasa kisheria..
 
Hicho kilikuwa kifanyike Zamani sana lakini kwa bahati mbaya Walichelewa. Pahali Popote duniani Nchi zinapoungana na visiwa lazima visiwa vipewe Special Status kwa vile visiwa ardhi yake ni ndogo. Lazima ilindwe Ardhi na ulindwe utamaduni wa visiwa. Kwa akili ndogo watafikiria ni upendeleo , lakini wenye akili timamu watajua kua huo ni Uhalisia. Kama kila mtu anayetaka kununua Ardhi ajenge Zanzibar ataruhusiwa, baadae Zanziba igeuka Jangwa jee madhara yatakayopatikana yataikumbwa Zanzibar Peke yake au na Tanganyika pia? Hapo ndipo Wanzanziabri wanapolalamikia Muungano huu kua nia ilikuwa ni kuimeza Zanzibar na kuifuta kwenye ramani ya Dunia. Hebu tujiulizeni kuna mzanzibari alipendekeza kua tanganyika ife? Au hata nyinyi watanganyika wakati Tanganyika inakufa muliuzwa mukatoa maoni yenu au ilkuwa na maoni ya mtu mmoja?
 
Kwenye hili hapana wewe mtanzania huna mamlaka ya kumiliki ila wao huku kwetu wananunua mitaa na hata ubunge mzanzibar anaweza kuja bara kugombea ubunge ila mbara haweze kugombea zanzibar kuna mambo ya ajabu sana katika haya mambo si bora huyo mkenya ananiruhusu mimi kununua property kwao kuliko huyu mtanzania mwenzangu wa karatasi nadhani hata kuowa hawakupi mke labda uje ufungie ndoa huku sio kwao.
 
Chukua chako mapema..dunii ina wenyew na haina huruma..mtu akikaa vibaya piga
 
Kati mambo ya hovyo ambayo Mwl Nyerere alituachia ni huu muungano chawa.
Kama huo uovu haukutosha; akapachika na hili la mgombea urais kuambatanishwa na makamu. Angetuacha na utaratibu uliokuwepo wa kufanya uchaguzi ndani ya siku 90 endapo nafasi ya rais inakuwa wazi.

Hovyo kabisa.
 
Hoja yako haina mashiko, unaenda visiwa vyovyote duniani na unanunua property na uraia wengine wanatoa ukiwekeza. Hoja yako ya Zanzibar kwani mtu kuuza ardhi analazimishwa? nchi ina sheria zake wapi unajenga wapi huruhusiwi akija mtu anataka kununua una hiyari ya kusema hapana siuzi. Huo utamaduni upi unaongelea? wao wamejazana huku kila sehemu na huo utamaduni wetu wanauchukuwa wenyewe kutoka huku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…