Masharti ya kuwekeza Zanzibar kwa Mtanzania bara na mgeni

Hatuna shida na wao peke yao kumiliki ardhi yao huko kwao.

Tuna shida wao kumiliki ardhi huku kwetu halafu sisi haturuhusiwi huko kwao.

Ndiyo maana tunasema, wao wamiliki ardhi huko kwao na sisi tumiliki huku kwetu, kila mtu amiliki kilicho chake tusileteane habari za chako nataka lakini changu sikupi
 
Ajabu, hii haijawahi kuwa listed kama kero za muungano.
 
zanzibar ni mke wa tanganyika anahaki ya kutumia mali ya mume wake ila kama inavyofahamika mali ya mke ni ya kwake ila ya mume ni ya familia
Alikuambia kardinal wako Pengo?
 
Wazanzibar sijui tutawabeba hadi lini. ningekuwa rais ningefanya juu chini muungano ufe hadi tuuzike. yaani wao wanapata ardhi hapa ya kumiliki lakini mimi Mtanzania mwenzao nikienda kwao naonekana mwekezaji? wao wanapata kazi bara lakini sisi tukienda kwao hatutakiwi kupata kazi, ujinga gani huu?
 
Rais Mwinyi ni Mzanzibar na anamiliki ardhi bara. Watanganyika sijui nani katuloga
jamani zanzibar ni nchi kamili na si sehemu ya tanzania bara.kama kweli hizi nchi zimeungana mbona tunabaguliwa kwenye ardhi wakati wanzanzibari wamejazana huku bara na wanamajengo na maardhi kibao.mm ninapoishi kuna wanzibar kama saba hivi wamejenga huku na wanamashamba ya kutosha tu sasa kwa nn sisi tunabaguliwa zanzibar.tuungane tuibadilishe katiba hii dhalimu pia tuufumue huu mfumo wa muungano.wazee wetu akina warioba mtusaidie katika hili la sivyo nchi yetu itaporwa yote na ss tutabaki watumwa ndani ya nchi yetu.
 
Suala la udogo wa ardhi siyo hoja! Hoja hapa ni usawa baina ya wananchi wa pande mbili. Kwa udogo huo huo wangeruhusiwa wachache kupewa kama ambavyo wao wanapewa huku bara na ikiisha si imeisha tu.
 
Zanzibar wataingia kwenye maajabu ya dunia iwapo
samia akimaliza mda wake waanze kulia tena wanaonewa na kuomba kuvunja muungano.
Niwakumbushe mda ndio huu raisi wa jamhuri hatakuwa mzanzibar milele.
 
Zanzibar wataingia kwenye maajabu ya dunia iwapo
samia akimaliza mda wake waanze kulia tena wanaonewa na kuomba kuvunja muungano.
Niwakumbushe mda ndio huu raisi wa jamhuri hatakuwa mzanzibar milele.
Amengilia dirisha dogo atii. Futani nafasi ya umakamu wa Rais kuwa Mzanzibariiii! Kwa hiyo mwisho liniiii? 2025 yakhee.
 
sielewi kwanini watanganyika tunanyimwa kuwa na ardhi zenji ilihali wao wana aardhi hapa wamemiliki sijui tatizo liko wapi jamani
We kwa bara tu unamiriki ardhi mikoa mingapi?
Umefika Katavi,masasi,murongo,kyelwa?kwanini mnaona nongwa kuwa na ardhi Zenj?ka sehemu kenyewe kadogo kuriko hata mkoa wa Geita!!,Zenj nzima inaweza ikaamia Dar na Wala hutaona tofauti!!tuache unafiki
 
Zanzibar wana ardhi ndogo sana; na hata idadi yao ni ndogo sana. kinachotakiwa ni kuwapa watanzania wote haki sawa popote ndani ya Jamhuri kusudi wanazibari wavamiwe na watanganyika ili nao waamke kutumia raslimali zilizoko Tanganyika kujenga level ground.
 
We kwa bara tu unamiriki ardhi mikoa mingapi?
Umefika Katavi,masasi,murongo,kyelwa?kwanini mnaona nongwa kuwa na ardhi Zenj?ka sehemu kenyewe kadogo kuriko hata mkoa wa Geita!!,Zenj nzima inaweza ikaamia Dar na Wala hutaona tofauti!!tuache unafiki

😳 lugha gongana mkuu naona unasakata kabumbu
 
Sema haka kakisiwa tunakanyonya sana embu tuwaachie watambe na hilo


Zinjiberi ni wake zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…