figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Shura ya Maimamu Tanzania
KUTOKA MAHAKAMA KUU LEO TAREHE 4/3/2025
MASHEIKH 12, WATOKA GEREZANI. WATANO NI FAMILIA MOJA YA ULATULE.
MASHEIKH 12, walio kaa gerezani miaka 10, (2015-2025), kwa tuhuma za Ugaidi wameachiwa huru leo. Uamuzi huo umetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Kirekiano.
Kabla ya hukumu hiyo Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP, aliambia Mahakama upande wa Jamhuri hauna haja ya kuendelea tena na shauri hilo.
Akitoa uamuzi huo mheshimiwa jaji amesema amekubali ombi hilo la Mwendesha Mashtaka wa serikali.
Kwa muda mrefu Shura ya Maimamu Tanzania imekua ikimuomba Mkurugenzi wa Mashtaka DPP kulifuta shauri hilo kwa sababu za upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha tuhuma dhidi ya Masheikh hao.
Walioachiwa huru ni:
1. Ali Mohammed Ulatule (70).
2. Khamisi Mohammed Ulatule (61).
3. Nassoro Suleiman Ulatule (41),
4. Rajab Ali Mohammed Ulatule (34).
5. Na Ramadhani Khamisi Mohammed Ulatule (29).
Wengine ni:
6. Saidi Abdallah Chambeta.
7. Fadhili Shaabani Lukwembe.
8. Mnemo Qassim Mwatumbo.
9. Abdallah Bushiri kalukula.
10. Khamisi Ally Masamba.
11. Omari Abdallah Makota.
12. Na Mohammed Hassan Ungando.
Katika kundi la Masheikh walioachiwa leo, 5, ni wa familia moja ya Ulatule. Wao walikamatwa familia moja watu 16, na baada ya masiku kadhaa (ya kutofahamika walipo), hatimaye 7, walikutwa katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam baada ya kufikishwa Mahakamani na kusomewa shtaka la ugaidi.
Aidha wenzao 9, hawajulikani walipo mpaka leo. Kati ya 7, waliokua gerezani 2, Sheikh Suleima Mohammed Ulatule (99), na Sheikh Saidi Mohammed Ulatule (79), wamefariki dunia wakiwa gerezani.
Kufuatia kuachiwa kwa masheikh hao 12, idadi ya mahabusu wenzao waliobaki katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam ni 39.
Shura ya Maimamu Tanzania inawashukuru wale wote wanaoshiriki ipasavyo harakati za kutetea haki za binadamu.
JamiiForums imewasiliana na Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda kuhusu maamuzi hayo ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar, amesema
“Tunaendelea kuwasiliana na DPP kuhusu wale 39 waliosalia ndani, tumefanya hivyo kwa njia ya maandishi na hata Watuhumiwa wamekuwa wakiwasilisha maombi yao ya kutaka kesi ifutwe pia,
Ni mashauri ya muda mrefu n ahata hoja zinazotolewa hazina mashiko, zinakuwa nyepesi sana, mfano unakuta inaweza kupangwa mashahidi 70 watoe Ushahidi ndani ya wiki mbili lakini wanaotoa ushahidi unakuta ni wawili tu, hivyo inafanya kesi kwenda mwaka mzima bila kuwa na mwendelezo unaoeleweka.”

=======================