Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mungu Akulipe Mara Mbili Ya UnAchokiwaza.AMEN.Tujiandae kwa lolote mtaani
Ndiyo ili uwe una cha kuwambia USA na EUROPEAN UNIONDuh miaka 10 unasota gerezani tena bila hatia
Hii nchi inapitia kipindi kigumu Sana
Na ndio laana inayosababisha jua linakuwa kali sana nchi nzima,uonevu na kupora haki za watu ni kitu kibaya sana,Duh miaka 10 unasota gerezani tena bila hatia
Hii nchi inapitia kipindi kigumu Sana
Naunga hojaNani kakuambia hawana hatia?? Mpaka uje uthibitishe kuwa hawana hatia, utakuta makanisa yameschomwa, mapadri wameuliwa na ushenzi kibao.
Namna ta kudeal na religious fundamentalists ni hivyo tu. Hata USA pale Guantanamo ndivyo walivyowasomba.
Dini ni kama bangi ukiipokea ndivyo sivyo. Hawa wameshikishwa adabu. HAWATOFURUKUTA tena
Shura ya Maimamu Tanzania
KUTOKA MAHAKAMA KUU LEO TAREHE 4/3/2025
MASHEIKH 12, WATOKA GEREZANI. WATANO NI FAMILIA MOJA YA ULATULE.
MASHEIKH 12, walio kaa gerezani miaka 10, (2015-2025), kwa tuhuma za Ugaidi wameachiwa huru leo. Uamuzi huo umetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Kirekiano.
Kabla ya hukumu hiyo Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP, aliambia Mahakama upande wa Jamhuri hauna haja ya kuendelea tena na shauri hilo.
Akitoa uamuzi huo mheshimiwa jaji amesema amekubali ombi hilo la Mwendesha Mashtaka wa serikali.
Kwa muda mrefu Shura ya Maimamu Tanzania imekua ikimuomba Mkurugenzi wa Mashtaka DPP kulifuta shauri hilo kwa sababu za upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha tuhuma dhidi ya Masheikh hao.
Walioachiwa huru ni:
1. Ali Mohammed Ulatule (70).
2. Khamisi Mohammed Ulatule (61).
3. Nassoro Suleiman Ulatule (41),
4. Rajab Ali Mohammed Ulatule (34).
5. Na Ramadhani Khamisi Mohammed Ulatule (29).
Wengine ni:
6. Saidi Abdallah Chambeta.
7. Fadhili Shaabani Lukwembe.
8. Mnemo Qassim Mwatumbo.
9. Abdallah Bushiri kalukula.
10. Khamisi Ally Masamba.
11. Omari Abdallah Makota.
12. Na Mohammed Hassan Ungando.
Katika kundi la Masheikh walioachiwa leo, 5, ni wa familia moja ya Ulatule. Wao walikamatwa familia moja watu 16, na baada ya masiku kadhaa (ya kutofahamika walipo), hatimaye 7, walikutwa katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam baada ya kufikishwa Mahakamani na kusomewa shtaka la ugaidi.
Aidha wenzao 9, hawajulikani walipo mpaka leo. Kati ya 7, waliokua gerezani 2, Sheikh Suleima Mohammed Ulatule (99), na Sheikh Saidi Mohammed Ulatule (79), wamefariki dunia wakiwa gerezani.
Kufuatia kuachiwa kwa masheikh hao 12, idadi ya mahabusu wenzao waliobaki katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam ni 39.
Shura ya Maimamu Tanzania inawashukuru wale wote wanaoshiriki ipasavyo harakati za kutetea haki za binadamu.
Dunia Haina HurumA.Uzuri kila anayetoka anaanza maisha upya. Toka wale wa UAMSHO akina Farouk na Mselem, hakuna tena anayeendekeza UJINGA.
Kweli gereza ni chuo cha mafunzo au ulaya wanaita correctional centre.
Hongera Kikwette kwa kuwadhubiti hawa "Siasa Kali wa Kiislamu. La sivyo nchi yetu ingekuwa kichaka cha Alshabab
Ndiyo muache kufuga ndevu sasaPia kuna wajinga wenye dhamana, wakiona tu mtu anandevu wanajua ni gaidi, ujinga wa hali ya juu.
Hii Inaweza Kuwa Ndo Chanzo Cha Chuki Dhidi Ya Kile Ulichokitaja.Nani kakuambia hawana hatia?? Mpaka uje uthibitishe kuwa hawana hatia, utakuta makanisa yameschomwa, mapadri wameuliwa na ushenzi kibao.
Namna ta kudeal na religious fundamentalists ni hivyo tu. Hata USA pale Guantanamo ndivyo walivyowasomba.
Dini ni kama bangi ukiipokea ndivyo sivyo. Hawa wameshikishwa adabu. HAWATOFURUKUTA tena
Kumbe JK hakuwaonea!!Ulatule mitaa ya kivule ccm walitesa na kuua nikiwa kwenye 15yrs walikua wanaogopeka. Tuhuma si za uongo
Kwani hamjui kama tunatawaliwa na mkoloni mweusi. Yena yeye ndio ana balaa zaidi. Mana ana kiburi na ulafiSheria za hovyo sn! Unamtesa mtu hivyo halafu humpi fidia! Mkoloni mweusi?
Hao muamsho issue yao ilikuwa kisiasa zaidi na wala sio udini.Uzuri kila anayetoka anaanza maisha upya. Toka wale wa UAMSHO akina Farouk na Mselem, hakuna tena anayeendekeza UJINGA.
Kweli gereza ni chuo cha mafunzo au ulaya wanaita correctional centre.
Hongera Kikwette kwa kuwadhubiti hawa "Siasa Kali wa Kiislamu. La sivyo nchi yetu ingekuwa kichaka cha Alshabab