Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Ndio wao walikuwa wanaleta itikadi kali za kiislamuKuna Masheikh wa Arusha? Wako rumande pia miaka kadhaa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio wao walikuwa wanaleta itikadi kali za kiislamuKuna Masheikh wa Arusha? Wako rumande pia miaka kadhaa?
Umemaliza Kila kituIpo hv mkuu, uzuri nilikuwepo unguja kipindi sakasaka hili linatokea, masheikh wa miadhara (uhamsho) wao walikuwa na ajenda yao kubwa ya kuamsha wazanzibar waliolala juu ya swala zima la nchi yao, wao kipindi wapo walikua wanawakumbusha wazanzibar kuwa si ccm wala chadema wala cuf itakayowakomboa kutoka kwenye maisha ya dhiki bali ni kufata mwenendo wa quraan na sunna za mtume.
Hawa masheikh hawakuvutiwa na cuf wala chadema wao walikuwa na sera yao kuwa demokrasia ni ukafiri ndio maana kila walipokuta bendera ya cuf au ccm wao walikua wakizishusha na kupandisha zao ambazo zina rangi nyeupe tupu na maandishi meupe kati yaliyosomeka kwa kiarabu hakuna mola anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na muhammad ni mjumbe wa mwenyezi mungu, wao wao walikuwa wanaamini kuwa kwa umoja wao basi walikua na uwezo wa kuiforce serikali ya ccm kutoka madarakani na wao kuchukua mamlaka kamili, nakumbuka wakati huo mambo mengi yalijitokeza wanawake waliovaaa nusu uchi walipigwa fimbo sn mitaani na vijana wafuasi wa uhamsho, walipinga sn siasa ndani ya zanzibar maana wao hawakuwa na chama, wakawa wanadamana kudai mamlaka kamili ndiipo serikali iliposhtuka na kuona hawa watu wakiachiwa mambo yataharibika Muda si mrefu ndio ikabidi wakamatwe.
Na ndio wakati huo huo viongozi baadhi wa makundi ya kijihad waliwakebehi uhamsho kwa style yao ya kutaka utawala utolewe na kuuita style za kizamni bimana kwenye uislam hakuna maandamano , hvy walitakiwa washike silaha na kuutoa udhalimu. Note sina uhakika sn inavyosemekana kukamaktwa kwa wale watu agizo lilitoka marekani na kusema hao watu ni htr sn hvy wakamatwe kwa makosa ya ugaidi wapo wanaodai kuna viongozi wa uhamsho walifanya training kandahar, na wakati huo raia wa kigeni huko zenji kipindi cha uhamsho walikutwa na madhira mengi sn like kumwagiwa tindi kali na kufanyiwa vitendo visivyofaa. hayo ndio yaliyowasibu uhamsho hadi leo America wanatazama kwa jicho la mwewe if watatoka au laa kesi ngumu.
View attachment 1750626View attachment 1750627
Jee wale waliokuwa wanaenda kugongewa usiku usiku na kukamatwa kisha kupandishwa ndege na kupelekwa magereza ya bara hadi Leo nao pia muamsho!?Nilikuwa kule mkuu so nimeandika nilichokiona na kukijua na hizo ndio bendera zao na hiyo ni picha walikuwa wakiandamana mjini kutaka mamlaka kamili zanzibar na kudai tanganyika inaikalia kimabavu zanzibar, serikali ilipoona kuundi linazidi kupata nguvu siku baada ya siku ndio ikabidi wakamatwe.
Kwa nini sasa!!?? Izo silaha mzito kwa ajili ya nini?Aisee jana niliona walivokua wanapelekwa Mahakamani msafara magari ya polisi kama 25 hivi na wana mitutu mizito.
Ila kheri hupatikana kwenye matumbo ya shari.Kama ndiyo hivyo acha wateseke.
😂wakifanyaga huu upuuzi, ma sheikh wenzao huwa wanajitokeza na kuukana hivyo mchuma janga hula na wa kwaoNdio wao walikuwa wanaleta itikadi kali za kiislamu
Vizuri.wasitoke wakae huko huko
1.kuchukua tahadhari, wanaamini linaweza kutokea kundi likataka kuwauwa hao ma sheikh au likatokea kundi likataka kuwadhuru askariKwa nini sasa!!?? Izo silaha mzito kwa ajili ya nini?
Tatizo mpo shortsighted Sana na maisha ya kijamii n kuheshimu dini za wengine.Vizuri.
Wazidi kuwasilimisha watu kuingia katika uislam. Wanaagiza majuzuu na msahafu kwa wingi. Hasa kipindi hiki cha Ramadhan.
Tabarakallah
Waache tu waendeee kukaa.Tatizo mpo shortsighted Sana na maisha ya kijamii n kuheshimu dini za wengine.
Kama mnaona wakikaa huko jela wanaeilimisha watu zaidi acheni kubwatuka kwamba waachiwe
Sababu:Kwanza kabisa hawa Masheikh wakati wanakamatwa Marais walikuwa ni Kikwete Muislam na Dkt. Shein muislam. Sasa hadi leo Marais ni Samia muislam na Dkt Hussein Mwinyi Muislam.
Lakini kila siku tunasikia hawa Masheikh 'wanaonewa' Kwa kukaa rumande miaka mingi bila kesi yao kupelekwa mahakamani.
Kuna mtu mwenye 'ukweli halisi' Atusaidie? Nini hasa kinaendelea?
Kumbe kuna mengi, basi waendelee kuwa huko tu....Sababu:
1. Walitaka kuvunja muungano ndio maana ya uamsho.
2. Zanzibar iwe na utawala wa sharia badala ya sheria ( mtu akiiba akatwe mkono)
3. Kuchochea vurugu
4. Inasemekana kati ya hao masheikhe kuna vibaraka wa waarabu na wangefanikisha tu issue ya kuvunjaa muungano basi wanarudi kuchukua kisiwa chao.
Mambo ni mengi na kesi yao ni ngumu sana ila kwenye media huku watu wanatetea vitu wasivyovijua
Wakae jela mileleKumbe kuna mengi, basi waendelee kuwa huko tu....
Wewe sema umeandika ulichotaka kuona. Wangewezaje kuiangusha hio Serikali ya CCM ikiwa wao sio Chama cha Siasa na kwa sheria za Uchaguzi za Tanzania kwa jumla kuingingia kwenye Uchaguzi wowote? Nilijua tu utazungumzia suala la Islamic state, nilijua utazungumzia suala la kutiwa Tindikali kwa Padri. Suala kujiuliza ni hili Baada ya kutiwa Tindikali sio mbio mbio mulileta wataalamu wa FBI kutoka marekani? Mbona walirejeshwa kimya kimya na ripoti ya nini kilitokea haikutolewa mpaka leo? Sio wewe unaijua sababu ya wao kutiwa ndani? Mbona miaka saba imepita na Upande wa Serikali wameshinda kuwakilisha ushahidi?.
Sasa nikueleze ukweli na utabaki kubakia ukweli mpaka dunia itamalizika, Uamsho wametiwa nddani kwa sababu kama walivyo Wazanzibari walio wengi wanapinga na wataendelea kupiga dhulma inayoitwa Muungano. Na kuwatia ndani Uamsho hakuwazuii wazanzibari kudai khaki yao ya msingi, kama unaelewa hivi sasa kuna kesi UN ya wazanzibari kuhusu Mungano. Kama munakataa kuurekebisha Muungano kwa maelewano, utavunjika kisheria ni wakati tu ndio utakaosema. Kuna Theory moja ya Physics inasemaWater is incompressiblemaana yake nguvu ile ile unayotumia kuyakandamiza ndio nguvu hio hiyo inayotumia kutaka kutoka
Their issue is very complicated..but sababu kubwa ni kwamba jamaa walikuwa ni tishio kwa ustawi wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar...na kwa kipindi kile walikuwa wanatumia jina la 'Dubwasha linaloitwa Muungano'. Na walikuwa tishio kwa Muungano kwa sababu walikuwa wanapigania Zanzibar yenye mamlaka kamili..Hakika walifanikiwa katika kuamsha fikra za Wazanzibari wengi na ilibaki kidogo tu Zanzibar ikomboke, yaani sijui kwanini Mungu aliwapa mtihani wa kudakwa mapema vile, laiti Allah angeruhusu wapate walau miezi mitatu tu ya hamasa kabla ya kukamatwa kwao, basi leo hii tungekuwa na Zanzibar yetu yenye mamlaka kamili na Tanganyika inayoonekana iliyojificha kwenye shuka la Muungano.
Kiukweli hatuzijua nafsi zao kiundani, ila hawakuwa na nia nyengine ovu ukiachia mbali kutaka kuikomboa Zanzibar kutoka katika mikono ya Tanganyika. Na ndio maana utakuta mpaka kesho kesi ya ugaidi waliyopewa haina ushahidi... Na hata kwa upande wa Zanzibar ambako nako walikuwa na mashtaka kadhaa ya Kufanya vitendo vinavyoweza kuleta uvunjifu wa Amani, mashtaka hayo yalifutwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar - Vuga, mbele ya Jaji Fatma Hamid...kwa kuwa siku zilishakuwa nyingi na mashahidi hawapelekwi mahakamani na wakati mwengine washtakiwa hapelekwi Zanzibar kuhudhuria kesi yao, kisa wapo Bara kwa kesi yao ya ugaidi iliyopo Kisutu...mheshimiwa Jaji akawaambia msinitanie.nafuta kesi dhidi yao, bakini nao nyinyi mfaidi.
Kwanini yeye ndio muhusika mkuu wakati hakuwahi kuwa Rais?kwenye list ungelimuweka kwanza balozi seif ali iddi, ndiye muhusika mkuu wa hiyo kadhia
Alubadili huwa inafanya kazi ? Kivip?Tumeshawaombea msamaha humu mitandaoni weee, sasa naona dawa wasome alubadili wazinguane tu.
Kabisa. JK alivyopenda kuwa fair wasingeliwekwa ndani. Kuna danger line walivuka.Hawa jamaa inaonekana walifanya kosa ambalo sisi wananchi hatujui. Maana kelele zoote za kuwaachia hamna anayezisikia