Masheikh wa Uamsho wafutiwa kesi, warejea uraiani
Mkawashauri sasa hao Masheikh wenzenu waishi kama dini yenu inavyotaka. Yale masuala ya kuhamasisha vurugu, utengano kwa kuwaumiza watu wasio na hatia, kumwagia watu wa imani tofauti tindikali, nk. Yalikuwa yanakiuka kabisa uvumilivu wa kiimani.
Kama u mwenye Uhakika huo Mkuu...Thibitisha hapa JF...
 
Wewe ni msengerema? Hakuna mtu aliyetaka hawa waachiwe ila watu walitaka hukumu itoke maana kama wana makosa wafungwe kama hawana waachiwe full stop, kama wamemwagia watu tindikali wafungwe tu
Hawa jamaa wanajifanya hamnazo
 
na wenye roho mbaya kama nyinyi. Hata Sabaya alikuwa na kibri kama nyie sasa hivi kakonda kama ana ngoma vile. Endeleeni kucheza na uhai wa watu wengine.
Pamoja na roho yangu mbaya ila mimi sina uwezo wa kumshinikiza rais wa nchi,inajulikana Shein ndio kawakamata na kumletea Kikwete,sasa aliyemshinikiza Shein ni Kikwete au nae Kikwete alishinikizwa?
 
Mimi binafsi namshukuru Mungu kwa hao ndugu kufutiwa mastaka yao, hata kama kweli walikua na sababu yoyote ya kuwa hapo walipokua lakini ninaamini kabisa mwanadamu ameumbwa kwa namna ya kujifunza.

Yamkini Kama sio wao hao mashaikh basi yupo ambae kwa kesi yao atakua amejifunza chochote kitu.

Siku zote ukiwa mtenda haki hata kama jamii itakuhukumu lakini haki itakutetea. Hii Ni kwa mamlaka na hata raia.
Paragraph ya mwisho nimeipenda.

Tutende haki jamani
 
Nadhani kama ulishazaliwa kipindi cha 2012 na kuendelea utakuwa umeshuhudia mateso waliopata bainaadam na vifo kupitia vuguvugu za lililoanzishwa na hao jamaa, lakini kama utaona waliopata madhar walikuwa ni kunguni tuu na sii bunadamu utona poa tu wakiwa uraiani wakate waliowasababishia wanaozea makaburini
Hao waliopata madhara ni kina nani?? Mbona hamuwataji???
 
Msiione haki kwa upande mmoja tu kutaka nyie mpewe zaidi ya wengine, huo ni ubinafsi, aina ya mahubiri mliyotoa yalihamasisha chuki zilizowaumiza wengine ambao nao wana haki zao, baada yenu kuwekwa ndani hali ikatulia.

Mkajifunze kuheshimu haki za wengine kama nyie mnavyotaka haki zenu ziheshimiwe, msijione bora zaidi ya wengine mpaka kuwasababishia maumivu ya aina yoyote.

Mmefurahi kutoka jela, ila mjue sasa mna jukumu la kulinda raia wengine wasio wa imani kama yenu, muache mihemko, fanyeni yenu muwaache wengine wafanye yao kwa uhuru wao, hii Tanzania ni yetu sote, hakuna alie juu ya mwingine wala hatakuwepo.
Good point.
 
Ni umbea kwamba huko jela kuna watu wengine ambao nao wameshikiliwa huko isivyo haki? kwamba ni hao masheikh tu ndio hawakuwa wakitendewa haki?

Hebu nielezee una maana gani unaposema umbea?
Ndugu,

Maana yangu ni kwamba, tuletee hayo majina ya watu walio jela wameshkiliwa huku kesi zao nikiwa na miaka 8 na kuendelea sasa hivi.

Niliposema usilete umbea nilimaanisha usilete story story tu. Lete majina!

Samahani kama nimekukera mkuu
 
Chadema tumepiga kelele sana kuhusu uonevu waliofanyiwa Mashekhe wa Uamsho.
Hakika mkuu.

Hata ikawa ni moja ya ahadi kutoka kwa mgombea wenu wa Urais kwamba akishinda tu anawaachia.

Katika hili Sisi hatuangalii CCM wala CDM tunaangalia haki ya masheikh na tunawashkuru CDM na CCM na wengine hata wasio na vyama wote waliopaza sauti kuhusu hii issue.
 
Mkuu umesahau maneno aliyowahi kusema Mh Mwendazake Samwel sitta? Alisema mambo ya sheria unaweza ukauua mtu na kisu ukapata mwanasheria mzuri wa kukutetea ukaachiwa huru ,hoja yangu ya msingi sio kuachiwa bali kama hawakutenda hayo mambo ya ugaidi kama ni kweli....Unaweza ukaachiwa huru lakini ukawa umetenda ugaidi.

Ni kama Babu seya rufaa zao zote ziligonga mwamba kwamba walikuwa na hatia ya ubakaji lakini wao kama wao walisema hawkutenda ila JPM alivyokuwa aliwatoa,je ni kweli walibaka kama mahakama ilivyosema au hawajabaka ndio maana JPM aliwaaachia? Ukweli wanaujua wao.

Mtuhumiwa ndio anajua ukweli 100% kama alitenda kweli au lah regardless maamuzi ya mahakama ,kushinda au kushindwa mahakamani kuna mambo mengi....si uliona mwanzoni sabaya alikamatwa na vitambulisho feki vya TISS lakini DPP akasema hana nia ya kuendelea na kesi,je ukikamtwa wewe mwenzangu na mimi kwa kesi kama hiyo DPP atasema hivyo hivyo kwa precedent.
Nimekuelewa mkuu.

Thanks sana kwa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom