Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
MASHEIKH WANASIASA WAZALENDO WALIOPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
Historia ya Waislam waliopigania uhuru wa Tanganyika ukisoma maisha yao utawakuta masheikh ambao wao usomeshaji wa dini iliku wa ndiyo jukumu lao kuu mfano wa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Yusuf Badi (Lindi) na Sheikh Mohamed Ramiya (Bagamoyo) kwa kuwataja wachache.
Halikadhalika kulikuwa na akina mama walimu wa Qur'an walioendesha madras mfano wa Bi. Halima Khamis.
Kulikuwa pia na masheikh wapigania uhuru lakini walikuwa na kazi nyingine wengi wakijiajiri wenyewe mfano wa Sheikh Suleiman Takadir na Sheikh Haidar Mwinyimvua.
Sheikh Suleiman Takadir alikuwa anaendesha mnada wake nyumbani kwake wakati Haidar Mwinyimvua alikuwa fundi bingwa wa kushona suti.
Kulikuwa pia na masheikh wapigania uhuru ambao walikuwa wakimiliki viunga vikubwa vya minazi mfano wa Mwinjuma Mwinyikambi na Jumbe Tambaza pia walikuwa na madrasa na waliweka walimu kusomesha.
Hawa wote walikuwa masheikh na kazi zao mbalimbali wakajumuika na Waislam na wananchi wengine katika kupambana na ukoloni.
Katika kuwaenzi kwa mchango wao wa kupigania uhuru hakuna mwenye haki ya kutaka kuleta ubaguzi kusema kuwa sheikh huyu ni bora kuliko yule kwa sababu yeye hakufanya kazi nyingine ila kusomesha tu na kinyume chake.
Uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa na Waislam wa kawaida na masheikh wanasiasa.
Soma kitabu cha Abdul Sykes (1998) utakuta historia hii yote kwa urefu.
1. Baraza la Wazee wa TANU, 1957
2. Mshume Kiyate na Julius Nyerere, 1964
3. Masheikh na Julis Nyerere Shambani kwa Sheikh Chaurembo, 1956
4. Sheikh Hassan bin Ameir
5. Sheikh Suleiman Takadir, 1958
6. Sheikh Haidar Mwinyimvua
7. Sheikh Mwinjuma Mwinyikambi, Max Mbwana, Julius Nyerere na Mshume Kiyate, 1962
8. Mtaa wa Sheikh Yusuf Badi, Lindi
9. Sheikh Abdallah Rashid Sembe
Hawa ni baadhi tu ya masheikh hawa waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Wengi historia zao hazijafanyiwa utafiti kwa hiyo hawajulikani.