Dubai ipo uarabuni but imejengwa na watu kutoka sehemu mbali mbali mfano hao wazungu wana mahotel yao makubwa dubai na masupermarket, hata wahindi wamejenga huko hao waarabu ukifanya utafiti utaone majengo machache ndio wanamiliki wao na ndio maana kama hujui dubai christmas ni kama ulaya dubai kama yote wanasherekea christmas ndipo ujue wageni ni wengi sana kuliko wazawa wa huko ukitaka kuhakiki hilo nenda christmas hii kajionee yaani kote wanapamba miti christmas na makanisa yapo kibao tu
Kwanzaa Mkuu ufahamu hao Raia wa UAE na Nchi nyengine za gulf gdp per capita ni $50,000 mpaka $100,000 wao ndio wamewaleta hao wahindi na wazungu sababu local wana hela nyingi za kuspend. Average mtu dubai Ana hela kuliko Nchi za marekani ama majority ya Nchi za ulaya. Why wasije Tanzania ama Nigeria why wakajenge Dubai?
Na kama Logic ni kujenga na ku own biashara basi Bidhaa nyingi kubwa Duniani zinamilikiwa na hao waarabu kwa asilimia kadhaa ama Biashara nzima,
Mifano ya Biashara ni kama Global foundry wanaotengeneza Chip za Amd kama unatumia ps4 ama Xbox unahusika, prince WA Saudi ni mmiliki mkubwa WA Twitter baada ya founder, vevo ambayo karibia wasanii wote YouTube wanaotumia ku upload video nk
Kasome Investment funds kama Mubadala ya Uae wana share Hadi telegram huko.
Bado Kuna Funds nyingi sana Eneo hilo, Ile ilionunua Newcastle tu ni zaidi ya Trilioni 1000 pia ina hisa kubwa makampuni kama Facebook, Uber, Boeing, General motors, Disney na makampuni mengine Mengi.
Kifupi Mkuu ni Almost impossible kukuta kampuni kubwa ambayo hela za waarabu hazijaingia.
Jiulize kwanini Marekani Mwarabu na Muiran anatambulika kama White, bila kujali alipotoka ila wengine ataitwa Mhindi, mlatino etc. Hata sensa za Marekani Mwarabu ni white, Biashara zao nyingi kubwa zimeanzishwa na hao watu, ndio maana leo mtu kama Carlos slim ama Steve job wanaonekana tu kama wazungu na sio waarabu.