Mashimba Ndaki, Waziri wa kwanza wa mifugo tangu Uhuru kuanzisha utambuzi wa mifugo kielektroniki

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2021
Posts
2,128
Reaction score
1,896

Mashimba Ndaki Waziri wa kwanza wa mifugo Tanzania tangu Uhuru kuanzisha utambuzi wa mifugo kielektroniki apongezwe na kutiwa moyo zaidi​


Nawasalimu kwa Jina la JMT,

Tangu Tanzania ipate Uhuru wake Dec 1961, Nchi hii haijawahi wala kujaribu kutambua mifugo yake kama ilivyo kwa Mataifa yaliyoendelea ya Uholanzi, Marekani, Norway etc ila Sasa Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wake Mashimba Ndaki.

Kwamsiofahamu mpaka naandika waraka huu kuna zaidi ya halmashauri asiliamia 50 zinaendelea na utambuzi wa mifugo yao kwa kuzivisha ngo'mbe, mbuzi, kondoo na punda hereni za kielectronic. Hii ni heshima kubwa kwa Rais na Taifa kwa ujumla wake.

Tofauti na Mawaziri wengine wengi waliotangulia Mashimba Ndaki ni mtu mnyenyekevu na mpole sana tena sio mtu wa kujivuna wala kujiona bora kutokana na cheo wala kujikweza kwa chochote zaidi ya unyenyekevu alionao kwa Mungu wake.

Huenda ni kutokana na upole wake huu na kutopenda mambo ya media sana Waziri huyu amekuwa akifanyiwa hujuma nyingi hasa humu mitandaoni kama nilivyoonesha hapo chini ili kuoneshwa kwa Rais kuwa Waziri huyu hafai ila Dkt. Kalemani au mwingine kama hayo mabandiko yanavyotanabaisha.

Tujiulize tu, Hivi hao walioshindwa hizo wizara nyingine wataiwezaje hii?

Kwa unyenyekevu mkubwa, naomba wasaidizi wa Mhe. Rais wetu kipenzi mmwambie kuwa Waziri Mashimba Ndaki ndio Waziri wa kwanza wa mifugo hapa Tanzania tangu tupate uhuru anayetambua mifugo kielectronic ili iweze kukidhi sharti la kuuzwa nje hasa baada ya Rais Samia Suluhu Hassan mwenyewe kufungua biashara ya mifugo na nchi za Falme za Kiarabu.

Kama kuna mtu anatamani Waziri Mashimba aondolewe hiyo wizara, asahau, sisi wafugaji na wavuvi tunamuhitaji sana kuliko pengine yeye anavyouhitaji huo uwaziri wake na ndio sababu ya kupaza sauti kukanusha nia hizi ovu za wasaka madaraka hawa.

Tunahitaji maendeleo sio maneno maneno, tunahitaji watu waadilifu na waaminivu kama huyu.

Pili, tukiacha chuki, hebu angalia Waziri Mashimba Ndaki alivyoituliza na kuimaliza kabisa migogoro ya wakulima na wafugaji kama hujui hili nenda mkoa wa Morogoro utaelewa ninachosema hapa.

imeandikwa "Nanyi mtanyamaza kimya kwakuwa mtetezi wenu yu-hai "

Mungu ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki Rais Samia
Mungu Mbariki Waziri Mashimba
 
ONA HAYA MAJUNGU,HIZI NYUZI ZOTE NI ZA MTU MMOJA ANAYETAKA NAFASI YA UWAZIRI KWA UFITINI NA UONGO.

πŸ‘‡πŸ‘‡







 
Naona Chawa wake mnajitahidi kumtetea asitumbuliwe 😁😁.

Siasa na ucha Mungu wapi na wapi?
 
Hamna chochote kwa huyo Bwana simkubali na napenda kujitutumua sana lakini Hana lolote, mheshimiwa rais Kama vipi apigechini huyu mtu ili tupate mwingine anayefaa kukamata hii wizara
 
Hamna chochote kwa huyo Bwana simkubali na napenda kujitutumua sana lakini Hana lolote, mheshimiwa rais Kama vipi apigechini huyu mtu ili tupate mwingine anayefaa kukamata hii wizara
Nani anapenda kujitutumua, Are serious?

Unamfahamu huyu Mzee?
 
Yes huyu Mzee ni Mtu sahihi Sana,
 
Mashimba tunaye Sana, Mungu ibariki Tanzania,
 
Mashimba yule mchamungu Sana aise, aishi milele
 
Zoezi hilo limefanyika kwa mujibu wa sheria ya bunge nambari 12 ya mwaka 2010.

Sheria ya UTAMBUZI, USAJILI na UFUATILIAJI wa MIFUGO.
Kwa kimombo inaitwa Livestock Identification, Registration and Traceability Act, 2010.
 
Naona Kalemani anavizia uteuzi tayari,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…