Mashindano ya kimataifa yatumike kama jukwaa la biashara kwa vilabu vyetu

Mashindano ya kimataifa yatumike kama jukwaa la biashara kwa vilabu vyetu

El Chapito

Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
63
Reaction score
65
MICHUANO YA KIMATAIFA KAMA JUKWAA LA FURSA YA KIBIASHARA KWA VILABU VYETU NCHINI
Kuelekea kuanza kwa michuanao ya kimataifa ngazi ya vilabu barani Afrika mwishoni mwa juma hili Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mashindano ya Klabu Bingwa tutakua tukiwakilishwa na vilabu vya Simba , Yanga na KMKM(Zanzibar) huku katika kombe la Shirikisho tukiwa na AzamFc ,Geita Gold Fc na Kipanga Fc(Zanzibar).

Pamoja na ugumu na ushindani uliopo katika michuano hii barani Afrika vilabu vyetu nchini pia vina nafasi nje ya ufundi na mapambano ndani ya uwanjani kutumia fursa ya kusafiri katika mataifa mbalimbali kama jukwaa la kibiashara ya kimataifa ambayo ikitumika ipasavyo inaweza kuleta tija na faida kubwa.Hii inawezakana kupitia mambo yafuatayo ambayo yanaweza kuchagiza kutengeneza soko la kibiashara kimataifa kwa vilabu vyetu:

1)Kutengeneza ushirikiano wa kibiashara baina ya vilabu(InterClub partnership)
Ushirikiano wa kibiashara kupitia partnership bond inaweza kutengenezwa kama fursa baina ya vilabu vyetu na vilabu pinzani tutakavyokabiliana navyo katika mashindano haya. Hii ni kupitia shughuli mbalimbali ambazo zitatengeneza ushirikiano huu katika namna ya kibiashara itakayoleta faida kwa pande zote mbili kwa mfano kupitia kubadilisha maono na mawazo , wataalamu pia na katika usajili wa wachezaji.Fursa hii ya kushirikiano itachangia urafiki na uaminifu pia ata kuinua chapa ya klabu kupitia nchi za vilabu washirika.

2) Kutengeneza soko la mauzo ya Jezi
Pia vilabu vyetu vinaweza kutumia nafasi hii ya ushiriki katika michuano ya kimataifa kama fursa ya kutengeneza soko la mauzo ya jezi kimataifa . Hii inawezekana kupitia ushawishi wa idara ya masoko ya klabu pamoja na wasamabazaji wa jezi kutengeneza ushirikiano katika nchi hizo ili kutengeneza namna ambayo mauzo ya jezi yanaweza kufanyika kupitia ushawishi kwa mashabiki wa soka kuweza kununua hivyo kuleta mapato Klabuni. Hatua hii ya kupata soko nje ya Nchi itakua chachu kupanua wigo wa kimapato kwa vilabu pia ata katika kuitangaza nchi kiujumla na kuweza kuvutia udhamini na uwekezaji nchini.

3)Kutengeneza misingi ya kiushabiki nje ya nchi
Misingi ya ushabiki yaani “Fanbase ” katika nchi zitakazokwenda vilabu vyetu inaweza kutengenezwa kupitia mvuto wa chapa ya klabu kupitia ushawishi wa kama klabu zetu zina wachezaji ambao wanatoka nchi hizo kwa mfano katika mechi ya Simba dhidi ya Nyasa Big Bullets kutoka Malawi, Simba inaweza kumfanya mchezaji kipenzi aliyepo kikosini yaani Peter Banda kutoka Malawi kama Balozi wa klabu nchini humo kupitia ushawishi wake na mashabiki zake hivyo Klabu itapata fanbase mpya. Hivyo kupitia msingi huu mpya wa mashabiki kimataifa inaweza kuwa fursa kuongeza wafatiliaji wapya kupitia mitandao ya kijamii kwa vilabu.

Aidha kupitia mambo hayo yanaweza kuleta tija katika namna ya kupata masoko nje ya nchi yatakayoinua mapato ya vilabu vyetu ata pia kuitangaza nchi yetu kiujumla katika nyanja ya kiutali na kiuwekezaji.
C.C - El Chapito
 
Back
Top Bottom