Mashindano ya kufuturisha: Waislam are you happy?

Mashindano ya kufuturisha: Waislam are you happy?

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,734
Reaction score
140,476
Kila ukigeuka huku unakuta waislam wanafuturishwa. Na huku wanasema kesho watafututisha.
Ni kama mashindano fulani hivi au kuna maagizo kutoka ngazi za juu kila taasisi ifuturushe?
Nakuja kwa upande wa waislamu, mko happy kufuturishwa? Je nyinyi ni wahitaji? Kwa nini ufuturishwe?

Mbaya zaidi hata watu wanaowafuturisha sio kwa nia njema, bali kuwatumia kama ngazi ya kisiasa. Na nyingi mwajua yote hayo.
 
Kila ukigeuka huku unakuta waislam wanafuturishwa. Na huku wanasema kesho watafututisha.
Ni kama mashindano fulani hivi au kuna maagizo kutoka ngazi za juu kila taasisi ifuturushe?
Nakuja kwa upande wa waislamu, mko happy kufuturishwa? Je nyinyi ni wahitaji? Kwa nini ufuturishwe
Hao wanatafuta political capital hawana lolote, uislamu hauko hivo wanafuturisha masikini uko vijijini na mjini kwa sehemu za masikini.
 
Na mm nashangaa mtu anafuturisha watu wenye uwezo wa kula milo 6 kwasiku ni maajabu
Wangekuwa na nia hiyo nzuri, wangekuwa wanapishana kwenye kambi za watoto yatima. Wangekuwa wanatatua changamoto za watoto wanaosoma madrasa kwenye mazingira magumu bila vitabu vya dini na nyezo zingine.
 
Paragraph ya mwisho nimekuelewa sana ..kiufupi lengo la kufuturisha halifikiwi kabisa , mtihani sana kwa kweli yaani ..Siasa nyingi sana kila kona .
 
Kila ukigeuka huku unakuta waislam wanafuturishwa. Na huku wanasema kesho watafututisha.
Ni kama mashindano fulani hivi au kuna maagizo kutoka ngazi za juu kila taasisi ifuturushe?
Nakuja kwa upande wa waislamu, mko happy kufuturishwa? Je nyinyi ni wahitaji? Kwa nini ufuturishwe?

Mbaya zaidi hata watu wanaowafuturisha sio kwa nia njema, bali kuwatumia kama ngazi ya kisiasa. Na nyingi mwajua yote hayo.
Muongozo inajulikana kua wanapaswa kufuturishwa ni wenye uhitaji masikin mafukara mayatima
....ila kwenye dunia ya ushindani ni vizuri kilamtu akachagua njia yake kama mtu anafuturisha matajiri mwengine anaweza kwenda kwa yatima mwengine anaweza kwenda kwa maskini akawalisha na asipige picha .... uzuri kilamtu ana malengo yake na mwisho wa siku kilamtu atabeba mzigo wake
 
Back
Top Bottom