Mashindano ya LIKES kwa WAANDISHI

benny gilbert

Senior Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
110
Reaction score
65
Habari wana JF. Bado natamani kufanya mashindano ya waandishi na kupata pesa, round hii nakuja na FORUMS kama JAMIIFORUMS ila yenyewe inakuwa kama group la facebook linavyofanya kazi wasomaji hawapost threads zaidi ya kucomment na kulike.

Waandishi wanakuwa kama MODERATOR facebook group inavyofanya kazi. Wanashindana LIKES kwenye POST ZAO. Ninakuwa natoa idadi ya LIKES kila mwezi wao wanapost vipande vyao vya hadithi kama wanavyofanya kwenye magroup ya fb kama njia ya kutafuta wasomaji wa kununua hadithi zao.

Vipande vya hadithi ni 20 tu kwa kila mwandishi na kwa kila hadithi, na inakuwa rahisi sana msomaji kumvisoma vipande vyote kwa urahisi inakuwa sio kama fb group vipande vinakuwa ni ngum kumvisoma kama umechelewa. Lengo ni kukuza jina ya mwandishi na kupata pesa. Mwandishi mwenye LIKES nyingi au alifikisha LIKES nilizoweka kwa mwezi ndio mshindi.

Hii pia itakuwa chachu kwa waandishi kuandika hadithi nzuri kwa lengo la kushindana na kupata pesa na kujenga jina miongoni mwao. Pia utapata wateja wa kununua hadithi zako kwa kuwa una hadithi nzuri na za kusisimua. BEST LIKES AUTHOR. Likes zinahesabiwa kwa hadithi zote unazopost , kwakuwa anapost sehemu moja ni rahisi kuhesabu , angalia hadithi zinavyopostiwa JAMIIFORUMS, ni rahis kusoma hadithi ya zamani yote bila kukosa kipande hata kimoja yote hiyo kwasababu zinapostia sehemu moja.

HII NI IDEA NIMEPATA JANA USIKU SANA , NINI MAONI YAKO , SHAURI WAKO KUHUSU HAYA MASHINDANO; JE YATASAIDIA KUKUZA UANDISHI NA KUBADILISHA MAISHA YAO?
 
Mkuu wazo lako ni zuri sana, humu pia tuna watu wanajua uandishi kama The bold, aina ya watu kama hao ndio wanaohitaji kupewa ushindani ili kukuza vipaji vyao, nimekuelewa
 
Mkuu wazo lako ni zuri sana, humu pia tuna watu wanajua uandishi kama The bold, aina ya watu kama hao ndio wanaohitaji kupewa ushindani ili kukuza vipaji vyao, nimekuelewa

Naona wengine wanapata tabu kunielewa, hongera kwa kunielewa.

"Thinking is the hardest discipline of all"
 
Binafsi nimekuelewa, kwa ufupi hiyo forum yako itakuwa kama group la facebook, ambapo wanachama wake wanakuwa ni watu wa kugonga like kwa hadithi au maandishi yoyote yatakayo wekwa / chapishwa na moderator (hapa tunasema kwa kifupi ma admin wa group au forum yako)
Kwa upande wangu sijashawishika mpaka hapa kujiunga huko, maana mimi kama mwanachama sitakuwa na uhuru wa kuwasilisha chochote huko zaidi ya kuyapa like mabwenyenye ya hiyo forum, kitu ambacho nakiona hakina faida kwangu wala kwao.
Au kwakuwa sijajua itakuwa inawasilisha na kuchapisha maudhui yanayohusu nini hasa, kama itakuwa siasa, mahusiano au umbea kama wa akina kigogo huko twita!
JF hapa tunaruhusiwa kuanzisha thread (ambapo wewe kwenye forum yako kuna watu au vichwa maalum watakuwa ndiyo waanzisha thread, hapa panaweza kuwa si tatizo)
Tatizo linakuja kuwa, mimi sina uwezo wa kujibu hiyo mada iliyoanzishwa, tatizo hilo tayari.
Ila anzisha mkuu, huenda ikaleta mapinduzi, huwezi jua.
 

Wasomaji hadithi wana comment na kulike tu. Like facebook group.
 
Kuandika kwa Aya ni mojawapo ya kanuni za uandishi, naona wewe hujaizingatia mkuu.

Kusoma andiko refu lisilokuwa na Aya inaboa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…