Mashindano ya Olimpiki Ufaransa 2024

Mashindano ya Olimpiki Ufaransa 2024

Sio mchangiaji humu lakini leo nitagusia kidogo tufanye nini ili nasi tuweze kushindana kwa ushindani
Wizara husika ifanye mkakati maalum wa kutafuta vijana kwenye kiwango cha kuanzia sekondari wenye muamko wa michezo kama riadha, kuwatafutia vyuo vikuu kwenye nchi zenye ushindani mkubwa wa mchezo husika, mfano America na Canada
Vyuo vingi huwa kuna ushindani wa michezo na serikali husika huwa wanafuatilia kwenye vyuo ili kupata wanamichezo wanaowahitaji
Ukiangalia wanariadha wengi wa Jamaica wana soma au wanaishi America au canada
Vile vile serikali itilie mkazo kwenye michezo kuanzia secondary na vyuo
Ahsanteni
 
Jioni hii nikiwa sehemu napata mbili moto huku nikiangalia moja kati ya michezo ya Olympic,nimeshangaa sana!
Huo mchezo siufahamu jina ila ni kama acrobatic lakini unafanyikia ndani ya bwana la kuogelea.
Aisee binadamu tuna uwezo mkubwa sana..mabinti wanazamisha vichwa vyao ndani ya maji kwa dakika kadhaa huku wakichezesha viungo vya mwili kwa ustadi mkubwa kama nyangumi.
 
Tatizo wanamuandama sana Imane Khelif, angekuwa ni mjerumani au mrusi wangeuchuna kama hawaoni vile.

Ubaguzi wa rangi bado upo sana duniani
 
Jioni hii nikiwa sehemu napata mbili moto huku nikiangalia moja kati ya michezo ya Olympic,nimeshangaa sana!
Huo mchezo siufahamu jina ila ni kama acrobatic lakini unafanyikia ndani ya bwana la kuogelea.
Aisee binadamu tuna uwezo mkubwa sana..mabinti wanazamisha vichwa vyao ndani ya maji kwa dakika kadhaa huku wakichezesha viungo vya mwili kwa ustadi mkubwa kama nyangumi.
Unaitwa sijui aqu nini sijui
 
Viunga vya jiji la Paris vimepangika si haba. Maeneo yaliplaniwa zaidi ya miaka 300 iliyopita, ila ukiyaangalia bado yanaendana na usasa.
 
Viunga vya jiji la Paris vimepangika si haba. Maeneo yaliplaniwa zaidi ya miaka 300 iliyopita, ila ukiyaangalia bado yanaendana na usasa.
Kuna economist alisema developing countries zinakua taratibu sana hatutakuja fikia nchi zilizoendelea bali gap itaendelea kuwa kubwa na nilijisikia vibaya sana aliposema hivyo ila kwa kweli ukiangalia miji ya Paris na Versailles yalivyopangwa tangia miaka hio bila shaka unaona kwa ukuaji wetu huu hatutoboi karne hii wala ijayo. Unashindwa kabisa kubisha .
 
Back
Top Bottom