Mashindano ya wazi ya Washika Dini na Wachawi. Mshindi kundoka na laki 5

Imeandikwa "usimjaribu Bwana Mungu wako....".
Kama wachawi watakuwa wanarusha makombora kwa watu wa Mungu, hao watu wa Mungu watakuwa wanarusha nini kwa wachawi au wao ni kukwepa tuu? Sasa hayo ni mashindano gani?
Kazi ni kukwepa tu
 
Mkuu siku 7/2025 ndiyo lini hiyo?
 
Mathayo 4:1–11

Yesu aliongozwa na Roho kwenda jangwani ili ajaribiwe na Shetani.

Baada ya kufunga siku 40 na 40 usiku, akawa na njaa.

Shetani akamshawishi abadilishe mawe kuwa mkate. Yesu akajibu β€œMtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu” (aya 4).

Kisha Shetani akampeleka katika kilele cha hekalu na kumwambia ajitupe chini maana imeandikwa malaika watamlinda.

Yesu akajibu: β€œImeandikwa pia, Usimjaribu Bwana Mungu wako.” (aya 7).

Mwisho Shetani akamwonyesha falme zote na utukufu wake, akimtaka Yesu amsujudie. Yesu akamkemea akisema: β€œUsimsujudie mtu ila Bwana Mungu wako.” (aya 10)
 
Watu wa Bariadi maeneo kama Gamboshi hawakufuzu kwenye kinyang'anyiro hiki?
 
Shindano litakuwa mbashara?

Kwanini wachawi wa Kigoma hawapo kwenye shindano mmmh au hawajafuzu kwenye mchujo?
 
Mkizikubali hizi conditions nitashiriki upande wa Nuru ( yesu kristo)
1. Shindano liwe mbashara
2. Mkinishinda nitakuwa kwenu
Ila Nikiwashinda nitawaongoza Sala ya toba mumpokee yesu kristo kila mtu akishuhudia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…