Na Gianna Amani
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanakwenda kasi, kutokana na changamoto mbalimbali zilizopo duniani, binadamu wameendelea kukuna vichwa na kutafutia ufumbuzi ambao umeleta tija katika maeneo mengi sasa. Teknolojia imechangia katika kurahisisha shughuli za binadamu, lakini kubwa zaidi ni kuongeza tija katika maswala mbalimbali, Kwasasa ambapo tupo katika mapinduzi ya viwanda ya awamu ya nne Teknolojia ya kidijitali na roboti zimeshika hatamu.
Ukizungumzia mapinduzi makubwa ya teknolojia huwezi kuacha kuitaja China, ambayo hivi sasa ndiyo mzalishaji namba moja duniani wa bidhaa za kidigitali, ukiuliza siri ya mafanikio unaweza kutajiwa mengi lakini ubunifu ndio sababu kuu.
Wakati ambapo hivi sasa binadamu wamekumbwa na shughuli nyingi za uzalishaji mali, wanakosa muda wa kutosha wa kufanya shughuli nyingine. Nchini China ubunifu wa teknolojia za kusaidia baadhi ya shughuli ambazo awali zilikuwa ni lazima zifanywe kwa mikono unasaidia wale wanaokosa muda wa kufanya shughuli nyingine.
Nchini China bunifu mbalimbali zimefanyika ya kusaidia kupika, katika picha inayoonekana hapo chini, mashine iliyovumbuliwa na kutengenezwa nchini China ina uwezo wake ni kupika vyakula tofauti mapishi zaidi ya aina 1000.
Hapa mashine hiyo zinatumika katika hoteli ya Shaxian Guangrong iliyopo katika mkoa wa Fujian, Mayai ya kukaangwa yanakuwa tayari ndani ya dakika tano, lakini pia mashine hiyo inaweza kupika rosti ya nyama na mboga mboga kwa muda mfupi sana tofauti na binadamu.
Mmoja wa watoa huduma katika Hotel hiyo alisema chakula ni halisi na kizuri, hakuna kuunguza, kuweka chumvi nyingi/kidogo au chakula hakijaiva, Mashine haikosei, na hii inaongeza ufanisi na kuokoa muda wa binadamu kufanya shughuli nyingine.