Mashine ya kuchimba visima Morogoro!

Mashine ya kuchimba visima Morogoro!

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Nilipokuwa ziarani Morogoro nilijulishwa kuwa, hakuna mashine/gari au niseme kampuni hata moja iliyopo mjini Morogoro yenye gari la kuchimba visima
Nilichokikuta pale ni madalali ambao hupatana na mteja halafu wao huenda kukodisha mashine/gari la kuchimba huko DAR na hivyo kufanya bei ya kuchimba kisima MORO KUWA GHALI SANA. Niliona kama kitu cha ajabu mkoa mzima tena maarufu kukosa mashine ya kuchimba Visima?
Kama kutakuwa na kampuni au Gari ambalo lipo stationed Morogoro ambalo labla sikulifaham naomba kujulishwa
 
Nenda pale magorofani PUMA, wapo stationed pale na magari yao kabisa
 
Yupo bwana mmoja anaitwa Ramadhan Senkondo amebuni mashine ya kuchimbia visima ya kwake hapa msamvu morogoro na inafanya vizuri sana,ni mfano wa kuigwa na ni mbunifu ambaye serikali ingetakiwa kimuwezesha huenda angefika mbali sana.
 
Cheki na DDCA
Ninavyo wafahamu hao wana ofisi nyngi ila mashine utakuta zipo stationed Dar au Dodoma
Nimetaka kujua kama kuna campuni ambayo MAGARI YAPO STATIONED MOROGORO; ndilo swali langu
 
Nenda pale magorofani PUMA, wapo stationed pale na magari yao kabisa
Hayo magari sikuyaona, labda yalikuwa yamepaki wiki hiyo Ila nitamjulisha mwenyeji wangu apitie tena hapo jumatatu kuangalia
 
Ninavyo wafahamu hao wana ofisi nyngi ila mashine utakuta zipo stationed Dar au Dodoma
Nimetaka kujua kama kuna campuni ambayo MAGARI YAPO STATIONED MOROGORO; ndilo swali langu
Ok Kama unahitaji hiyo huduma nijuze coz Nina experience nayo kitambo though nilibadili fani naweza kupa mtu sofar yupo Kongwa ukihitaji nijuze nikupe namba mkuu
 
Ok Kama unahitaji hiyo huduma nijuze coz Nina experience nayo kitambo though nilibadili fani naweza kupa mtu sofar yupo Kongwa ukihitaji nijuze nikupe namba mkuu
kiongozi, nipo interested ila kuwasiliana na mtu/kampuni iliyo na gari ya kuchimba visima lililopo stationed Morogoro
Sipendelei gari la kufanyia re allocation kwa mtrja wangu hiyo ni last option
 
Misufini mkabala na zile mashine za kusaga kulikuwa hizo ofisi kuchimba visima zamani sijui bado zipo.
 
Ok hebu cheki hizo petrol station za Moro Rd au Msamvu huwezi kosa Drill rigs ukichemka utasema
kiongozi, nipo interested ila kuwasiliana na mtu/kampuni iliyo na gari ya kuchimba visima lililopo stationed Morogoro
Sipendelei gari la kufanyia re allocation kwa mtrja wangu hiyo ni last option
 
Kama kweli hakuna kampuni ambayo ina-station vifaa vyake Morogoro basi nakushauri ufanye utafiti wa kina kujua nini kinasababisha hili isije ikawa uhitaji wa huduma hiyo ni mdogo au tenda(za kuchimba visima) ni chache sana.
 
I think wapo mkuu,sijawahi watumia lakini naju wana offices karibu na kihonda bima/samaki samaki,superbyte ilikua ofisi ya jti zamani
 
Puma Hapo Viwanda Wana Ofisi Na Gari Zao Zipo
 
Kuna jamaa flani na mke wake wamenunua vifaa vya drilling vya iliyokuwa Layne. Ukiulizia ilipokuwa yard na ofisi za Layne utawapata. Wako area moja na kiwanda flani wanadai kinatengeneza nguo za kuuza nje
 
Back
Top Bottom