KERO Mashine ya MRI Mloganzila Hospital ni MBOVU

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Habarini, naleta taarifa hii kwa masikitiko makubwa sana kwa mara nyingine tena kwa sababu jambo hili sio mara ya kwanza kuripotiwa

Mashine ya MRI (Magnetic resonance imaging) katika Hospitali ya Mloganzila ni mbovu takribani mwezi mmoja na nusu na hali ni mbaya, wagonjwa wengine inawapasa wapange foleni katika kupata huduma hii tena kwa kusubiri masaa mengi sana... Foleni hiyo sio hapo hapo hospitalini TU bali ni katika hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo Upanga

Ni aibu kwa Hospitali yenye hadhi ya TAIFA kama Mloganzila kukosa huduma hii muhimu, pamoja na jitihada za Mheshimiwa Rais kukuza sekta ya afya lakini kuna baadhi ya watendaji wanamuangusha. Kwa inavyoonekana kuna watendaji wazembe (Wakurugenzi na wakuu wa idara) hapo hospitalini wanasababisha Mashine hii kuharibika na kutofanyiwa matengenezo kwa wakati (Wakibisha ushahidi nitauweka hewani kwa sababu upo)

Wagonjwa wanahamishwa kutokea Muhimbili Mloganzila kwenda Muhimbili Upanga jambo ambalo ni usumbufu kwa wagonjwa wengine inawabidi wasile siku nzima kusubiria kipimo lakini mwisho wa siku hawafanyiwi, sasa kushindishana njaa siku nzima maana yake nini? Hii ni sawa kweli?

Vile vile wagonjwa wengine wanatoka mbali sana mwisho wa siku wanaamua kuondoka,kukesha hospitali na wengine kukata tamaa ya kupata huduma kwa sababu kunakuwa na mlundikano wa wagonjwa wanohitaji kipimo hicho kutoka Muhimbili Upanga na Muhimbili Mloganzila

Pia kwa kuwa Mloganzila wana mashine moja ya MRI napendekeza au kushauri waongezewe mashine nyingine ya MRI ili watoe huduma stahiki kwa wakati

Tunapaza sauti suala hili lifanyiwe kazi haraka na mashine ya MRI irudi kwenye hali yake ya kawaida.

ASANTE
Mama hatumdai, hana deni
 
Naomba niulize kwanza hicho kipimo cha MRI kinauzwa kiasi gani mpaka kiwepo kimoja hapo hospitalini na kazi yake kuu haswa ni ipi ? Mimi nimefikiri huwenda ni kipimo cha magonjwa makubwa na kinabai kwa uharaka zaidi , naombeni mnisaidie ? Alafu sekta ya afya mbona ina mipesa mingi.
 
Kuna mambo nchi hii yanaumiza sana kichwa,hayo ni mambo madogo ambayo wala hayahitaji nguvu kubwa

Tatizo kuna viongozi wazembe wa kufuatilia hiyo changamoto,kipimo kama hicho kweli ni cha kukosekana karibia mwezi au wiki mbili?

Watu hawawajibiki ipasavyo kwenye septa zao,na wanajua hakuna wa kuwajibisha,sijui ishu hiyo ingetokea Enzi za jiwe tungesikia upuuzi kama huo

Tutakukumbuka sana mwamba Jiwe
 
Hili linawezekana lkn hao jamaa huwa hawafanyi mambo pasina maslahi yao

Kwenye mboga mboga kule waametoa mpunga mnene kwakuwa wanajua mwisho wa siku mambo yao yataenda
Kama 20,000 za vibali vya wamachinga
Yaani kuna watu wamepiga nchi hii

Vyoo msaada toka US
Ila machine hakuna wa kutengeneza
 
Shida ni pale kiongozi wa juu atakuja kukanusha na atasema ni nzima, hii ndo new era ya uchawa.
 
Gharama ya MRI ni 3.5 bilioni hadi 7 bilioni inategemea na nguvu ya sumaku na mwaka wa utengenezaji

Gharama za kuandaa chumba cha kuweka hio mashine ni 1 .5 bilioni hadi 2 bilioni

Matengenezo ni 300 milioni Hadi 700milioni

Lakini sizani kama nchi tumeshindwa kuwa Nazo hata 100 tu hii ni makusudi tu
 
Ni makusudi
 
Hili linawezekana lkn hao jamaa huwa hawafanyi mambo pasina maslahi yao

Kwenye mboga mboga kule waametoa mpunga mnene kwakuwa wanajua mwisho wa siku mambo yao yataenda
Watu wa mipango wizara ya afya, wapambane na hili?
 
Wahusika waliangalie hili kwa hicho la tatu maana kukosekana kwa kipimo hiki ni hatari sana kwa wavonjwa wanaohitaki huduma hii ya MRI
 
Hizo MRI na CT Scan zitakuwa hazina wataalam wa ndani wa kuzifanyia matengenezo zikiharibika au shida ni spare parts tofauti na zile za X ray.
 
Gharama ya MRI ni 3.5 bilioni hadi 7 bilioni inategemea na nguvu ya sumaku na mwaka wa utengenezaji

Gharama za kuandaa chumba cha kuweka hio mashine ni 1 .5 bilioni hadi 2 bilioni

Matengenezo ni 300 milioni Hadi 700milioni

Lakini sizani kama nchi tumeshindwa kuwa Nazo hata 100 tu hii ni makusudi tu
Astàkafilulah mi nilihisi MRI Moja inagharimu tillion tatu mpaka sita kumbe ni b 3 mpaka 6
Basi mungu nifundishe kunyamaza zaidi
 
Maswala muhimu km hayo hawaoni,
Ila kwenye mambo ya kipuuzi hela inatapanywa haswa.
Hospitali kubwa km hiyo kulitakiwa machine hizo hata 3.
 
Back
Top Bottom